AN-NUUR
Na.156 Rabi' Awal 1419, Julai 4 - 9, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
BARUA
[Hongera Rais Mkapa] [Serikali iache kuhadaa wananchi
[Waislamu tumechoka kunyanyaswa] [Wahariri waenzi fani ya habari]

Hongera Rais Mkapa

Mheshimiwa Rais,

Katika barua yako iiliyotokea katika gazeti la Daily News la Mei 28,98 umetupatia mwanga mkubwa. Kwa sababu hiyo naomba upokee hongera zangu binafsi na wale wote wenye mawazo kama yangu.

Kwa kawaida usipowaambia unaowaongoza unachokifanya watakisia kwa yale mabaya yanayojitokeza na kuyahalalisha kwamba hiyo ndiyo kazi yako.

Mimi na wenye mawazo kama yangu tunakupongeza pia kwa kuifuta PAROLE kwa sababu ufutaji huo umethibitisha kauli yako kwenye barua yako kwamba unajali.

Mheshimiwa Rais wetu, naomba utufafanulie uliposema kuna uhuru wa kutoa mawazo ulimaanisha nini. Nasema haya kwa sababu katika Serikali ya awamu ya kwanza wewe ukiwa Waziri ulishuhudia kauli za mara kwa mara za Mwalimu Nyerere kwamba kuna uhuru wa kutoa mawazo, lakini kila aliyetoa mawazo yaliyopingana na ya Mwalimu aliishia kizuizini. Si hayo tu, mitaani walikuwepo mashushushu wengi waliotishia uhuru wa kusema. Kila mtu hakuwa na uhuru wa kutoa mawazo hali kila alichosema kilikuwa sicho alichoamini.

Katika serikali ya Awamu ya Pili wewe ukiwa waziri kulifanyika mabadiliko makubwa, nchi iliyokuwa inatamba ghafla ilianza kupata kasi kwa nyanja zote. Mzee ruksa aliwezesha kuweko kwa demokrasia ya kweli. Hakukuwepo mashushushu wala vizuizini. Alidhamiria kuondosha kero na akafanikiwa sana watu walikosa cha kusema baada ya kusema yote waliyotaka ya siasa, uchumi wa jamii mwishowe walitaka (paparazi) awaeleze kama ana mchumba mpya!

Kwa kweli Mzee Ruksa ana kumbukwa mitaani. Ni muungwana na anayaejali.

Serikali yako umeitangaza kuwa ya ukweli na uwazi. Hapa maana yake ni kuwa HAKUNA KUSEMA UONGO na pili hakuna kuficha jambo.Watu tukaona hii ni hatua moja mbele ya Mzee Ruksa.

Lakini tofauti na kauli vitendo vya serikali hii vinaashiria uongo na kuficha mambo:

Uchumi; wakati serikali yako iking’ang’ania kuuza viwanda na benki ya biashara kwa kauli ya kwamba benki inatia hasara wananchi wanaona si haki na maelezo hayatoshi kuhalalisha jambo hilo. Benki ilipata faida.

SIASA:

Watuwenye msimamo tofauti na wa chama chako huishi kwa wasiwasi kama wakati wa Nyerere. Huzuliwa mambo. Hadi sasa wananchi wa Tanzania hawaamini kwamba kuna watuwamepanga kupindua nchi hii maana mapinduzi hufanywa na askarivipi ni wanasiasa tu hakuna hata askari mmoja aliyetuhumiwa. Kweli watu hao hawanaubongo wa kuwajua vijana wa Generali Mboma kwambahawawezi kuvumiliavitendo hicho. Ni haki kuwepo kwao ndani?

DINI:

Mheshimiwa Rais wetu mtuanaposema Muhammad amekufa kwa ukimwi au akisema Yesu alisulubiwa kwenye mbao alizoiba huyu analenga kuudhi watu. Lakini mtu anaposema Muhammad si Mtume maana ukuta wa jengo ulikamilishwa na Yesu au akisema Yesu si Mungu maana Mungu hawezi kujililia mwenyewe. Mungu wangu mbona unaniacha. Hawana hatia hawa. KATIBA inaruhusu na sheria inaruhusu. Kinachotakiwa hapa ni wao wenyewe kukaa mahali ikiwezekana wanakunywa soda au kahawa huku wanajadili kwa kina tofauti za mitazamo hiyo. Ni njia ya kuelimishana tunayoisisitiza siku zote. Huo ndiwo uhuru wa kutoa mawazo. Mheshimiwa Rais. Huo ndiwo UWAZI na UKWELI Mheshimiwa Rais. Jambo hili linakubalikadunia nzima isipokuwa katika serikali yako na Ulya enzi za giza ambako walimhukumu Galiteo kwa kutoa mawazoyake leo wanajutia jambo lile. Waliimuua kwa njama za maasikofu.

Serikalii yako ina wakamata watu hao na kuwafungulia mashitaka siyo kwa kusema hayo baliwanazushiwa mapya ilimradi wawekwe ndani bila dhamana ili wateseke gerezani bila sababu. Kule wanakomolewa kama sehemu ya mchango wa mahakimuau majaji na wakuu wa polisi katika kupambana na Waislamu. Wanafanya si kwa kuongozwa na katiba bali na Imani zaoza kidini. Wanatoa mchango wao kuinusuru dini yao.

Kuwepo kwa Wakristo watupu na Maaskofu wao katika PAROLE lisingekuwa suala la kulalamikia kama usingeifikisha nchi mahali ambapo vyombo vya HAKI vinaongozwa na Imani zao za kidini na kisiasa. Wanacnhi wote wanafahamu kuwa kukataliwa dhamana mama zao, baba zao na watoto wao ni njia mpya ya kizuizini na ni mchango wa Mahakimu na Majaji kwa dini zao. MUNGU AKUSAIDIE upate washauri wazuri.

Ahsante.

MZALENDO H. KIMANGALE,

S.L.P. 605,

TANGA. 

 

Serikali iache kuhadaa wananchi

Ndugu Mhariri,

Serikali ieleze kisa cha kweli ili raia tujuwe. Serikali na Waislamu wana ugomvi gani? Ama sivyo tutaamini malalamiko yao wenzetu (Waislamu) kwamba hapa Tanzania wao wamebanwa mno, sasa yawezekana Serikali inatumia kuuwa, vitisho, propaganda za uwongo ili kufukia madai ya wapigania uhuru wenzetu, mumeusoma kwa makini waraka wa kamati ya kutetea haki za Waislamu uliochapishwa katika gazeti hili na katibu wa kamati hiyo Ponda Issa Ponda, nimegundua waraka huo unatoa picha ya kweli kwa asilimia 99, kuliko maneeo ya serikali. Hata ombi lao la kutaka kumkamata Ponda kwa mujibu wa waraka huo ni kitendo cha dhuluma.

Hivyo serikali kama ina ugomvi na Waislamu wa nchi hii, ituambie au watafute uwongo nzuri, sio kusingizia Mihadhara ya kashfa kwani hali tunayoenda nayo, itaunda matabaka, Watanzania tutakufa sana na nyinyi viongozi mtakimbia nchi za nje? Rudisheni haki za watu hata kwa kujiuzulu.

Mmesema mengi mara kuna mkono wa siasa, mara balozi zahusika, mara wafanyi biashara, mara wanakashifu dini za watu.

Tuelezeje? Serikali isituhadae wananchi kwa kila jambo hata haya ambayo tunayashuhudia kwa macho yetu.

Josephinah Mbwambo,

S.L.P osta 846, DSM
 

Waislamu tumechoka kunyanyaswa

Ndugu Mhariri 

Tunaomba utupatie nafasi katika gazeti lako tukufu ili nasi tutoe dukuduku letu kuhusu unyama uliofanywa na askari wa serikali ya CCM kwa kuingia kwa nguvu msikitini (mahali pa amani na salama) na kuwadhalilisha na kuwapiga mabomu Waislamu wasio ha hatia. 

Kitendo hichi kinaonyesha kana kwamba Waislamu wa Tanzania hatupo katika nchi yetu bali tupo katika nchi ya ukimbizi. Hata hao wakimbizi huwa wanatetewa na Umoja wa Maraifa, lakini Waislamu wa Tanzania hawana wa kuwatetea. 

Tulitegemea kuwa angalau vyama vya upinzani vingetutetea au hata kulaani tu mauaji yale lakini hakuna.

Tulitegemea labda vyama vya hiari (NGO's) vingetutetea lakini wapi.

Tulitegemea labda BAKWATA angalau ingetoa tamko hata la kutoridhishwa tu na mauaji hayo lakini wapi.

Kwa upande wa Serikali iliyofanya mauaji hayo sisi tunasema; tumehuzunishwa na kusikitishwa mno. Tumebakia na maswali mengi yasiyoweza kujibika kirahisi.

Je, sisi Waislamu wa Tanzania tumeikosea nini Serikali hii ya CCM?

Je, kuhubiri kwetu dini yetu tukufu na kuwaita watu kwenye njia ya "amani na ukweli" ndio imekuwa nongwa? Mbona walokole wanahubiri na kusema chochote wapendacho juu ya Uislamu lakini hawaambiwi wanakashifu? 

Je, Serikali hii inayodai kuwa haina dini ina agenda gani ya siri dhidi ya Uislamu na Waislamu? Au tuseme ina dini rasmi ila inajaribu kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa? 

Tunamalizia kwa kusema; mauaji ya Waislamu Mwembechai ni ukiukwaji wa Kitabu cha Allah (s.w), ni ukiukwaji wa sunnah ya Mtume (s.a.w), ni ukiukwaji wa mkataba wa haki za binaadam wa Umoja wa Mataifa ambao Tanzania imeuridhia, ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ni ukiukwaji wa maadili na heshima ya wananchi wa Tanzania.

Vijana wa Kiislamu

Itigi - Manyoni
 
 

Wahariri waenzi fani ya habari

Ndugu Mhariri, 

NAOMBA nafasi katika gazeti lako nitowe wasi wasi wangu.

Fani yahabari na vyombo vyao ni muhimu sana na hili si jambo linalohitaji maelezo marefu.

Jambo linalotisha ni kasi ya kuanguka kwa maadili katika fani hii muhimu.

Linalotisha zaidi ni kule kuona wahusi kakatika kuanguka kwa maadili ya habari si wana habari wenyewe.

Haya ninayo yasema kwa zama hizi hayahitaji mtu kuwa mtaalamu sana kuyaona.

Ni jambo la kawaida sasa Mwandishi kuandika habari ya uzushi; matusi, habari bila utafiti, uchochezi n.k.

Ni jambo la kawaida kumsikia Mwandishi anaahidi "Kama hanijui ngoja nikamkandie". Mwandishi anaandika hali ya kuwa anayakini kabisa kuwa anachokiandika ni uongo lakini anaamua kukirusha hewani.

Hali hii sasa inapelekea wananchi Tanzania kuanza kudharau fani ya habari kama walivyo dharau siasa kwa kusema "Siasa ni uongo".

Dhana ya Waandishi wa habari ni waongo, wambea, wachochezi ina komaa na bila shaka kizazi kijacho haitakua dhana tena bali itakuwa "hakika".

Lakini katika hali hii wakulaumiwa ni nani? Wakulaumiwa ni Wahariri wa Vyombo vya Habari na hasa wale wa magazeti. Binafsi taasisi za serikali za kudhibiti habari sizikubali kwa kuwa haziko kwa lengo la kutoa uhuru wa kweli na kuinda maadili ndio maana tegemeo langu kubwa ni Wahariri..

Sifa za Mhariri zinazothibitisha umahiri wake huonekana katika habari anazo ruhusu katika chombo chake, mwenendo katika upokeaji na utoaji wa habari.

Nimelazimikakushika kalamu kutokana na kasoro na kero nyingi zinazojitokeza katika magazeti yetu. 

Ni vema nikadondoa moja ya habari iliyochapishwa katika gazeti moja litolewalo kila siku Toleo Na. 1608 la Mei 29, 1998 Chini ya kichwa kisemacho KITWANA KONDO ANACHOCHEA VURUGU, AWAJIBISHWE.

Habari hii iliandikwa na Mwandishi Faustino Rwambali. Faustine alimshutumu KK kwa madai yake aliyoyatoa hivi karibuni dhidi ya serikali ya Tanzania.

Kwa kifupi Mwandishi baadaya shutuma zake alitaka mambo matatu yafanyike haraka:

A: Serikali imkamate KK mara moja. B. Mahakama imuingize kama shahidi wa kwaza katika kesi za Mwembechai. C. Chama cha CCM kimhoji kama kilivyomhoji hayati Kolimba.

Katika makala hayo Mwandishi aliueleza wasifu wa KK kwa sifa nne.

Mhaini Mnafiki Mropokaji Mchochezi.

Nikizungumzia mafungu A,B,C. Mwandishi anasahau alichokemea "Uchochezi" na yeye anarudia kwa "Kuichochea" serikali, Mahakama, na CCM kuwa vimkamate KK na kumuweka ndani.

Mwandishi pia alisema KK si msemaji wa Waislamu akasahau kuwa iliyoshutumiwa ni serikali na yeye si msemaji wa Serikali.

Mwandishi pia anauliza kwanini serikali haijamchukulia hatua KK wakati Mwandishi anajua serikali ipo hapa hapa Dar es Salaam na huko anaweza kupata jibu la swali lake ambalo sisi wasomaji ndio lingekuwa na maana kwetu.

Aidha, mwandishi anakiri kuwa KK hajaombwa ushahidi na serikali lakini yeye ana muhukumu kwa kumuita mhaini.

Lakini sahau ya Mwandishi isitushughulishe sana, jambo zito linalozua utata ni jinsi Mhariri wa gazeti letu alivyoridhika kuchapisha makala inayomuelekea mtu kwa lugha chafu za "Mnafiki, Mhariri, Mropokaji, mchochezi n.k.

Mtu anakuwa Mhaini, mchochezi na sifa kama hizi baada ya uchambuzi wa kisheria ambao hatudhani kama Mhariri aliletewa.

Picha inayojitokeza katika hali hii ni Mhariri kutoona tatizo katika lugha ya Mwandishi wake.

Hili ndilo linalotutia wasiwasi na mashaka juu ya fani hii ambayo ina uhusiano wa kila siku na wananchi.

Habari zilizochujwa vizuri huelimisha na kuleta mahusiano mazuri ndani ya jamii.

Kinyume chake huamsha hisia za chuki na malumbano ambauyo huenda yatakuwa na hatimae kuzihusisha koo.

Namaliza kwa kukumbusha kuwa Wahariri bado hawajachelewa wakijikomboa kutokana na kuchapisha au kutangaza habari kwa kuegemea sababu fulani kinyume na maadili ya habari, wanaweza kabisa kubadili kasi ya muelekeo mbaya wa habari nchini.

MFINAGA YUNUS,

NGARANARO ARUSHA.
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini 

Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani

Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke

Serikali kuzuia mahubiri ya Waislamu, kuvamia Msikiti, kukamata, kudhalilisha na kuua Wananchi ni kuvunja Katiba na Sheria za Nchi

Kujua lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Na Sadick M. Sadick"

Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi

Intifada ndio jibu (2)
Na Sheikh Pandukizi Dilunga

Kusema ukweli ni sehemu ya uadilifu
A.S. Chachika

Mafumbo ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Na J. Hussein

Majibu kwa Kamara Kusupa

Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai

Asiye na elimu kwa mujibu wa Biblia
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

TAMTA yaadhimisha miaka 36
Na Masoud Mohamed Said, Tanga

Muumini aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Na Muhibu Said

Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30

Habari za Madrasa

Barua 

Mashairi 

Lishe : Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili 
Na Dk. Ali. A. Mzige
  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita