|
|
| Mtoto
anyonye maziwa ya mama miaka miwili
Na Dk. Ali. A. Mzige WANASAYANSI wa kileo wanasema kuwa mama aliyejifungua amnyonyeshe mwanae kwa kipindi cha miaka miwili. Katika Uislamu hilo si jambo geni bali ni amri ya Mwenyezi Mungu. Hivi sasa kuna wimbi la kuwahamasisha wanawake duniani kote wawanyonyeshe watoto wao baada ya wanasayansi kubaini kuwa maziwa ya mama yana vitamini A na kinga ya mwili (antibodies) ya kumkinga mtoto asipatwe na maradhi yaliyozoeleka kuwasumbua watoto. Aidha, kumnyonyesha mtoto mfululizo kwa miaka miwili huweza kumwepusha mtoto na maradhi ya pumu, maradhi ya masikio (otiti media) na homa ya uti wa mgongo (meningitis). Lakini jingine ni kwamba watoto wanaopata maziwa ya mama kwa muda mrefu wamegundulika kuwa na kiwango cha juu cha akili (High I.Q). Kwa upande wa mama akinyonyesha kwa muda mrefu humsaidia asishike mimba maana wanawake wengine wakinyonyesha mfululizo hawapati hedhi. Watu wamepewa shahada za juu (Ph.D) kwa utafiti wao juu ya masuala haya
ya kumnyonyesha mtoto, utafiti ambao chimbuko lake ni aya ya Mwenyezi Mungu
isemayo, "Na wanawake waliozaa wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili…".
(2:233)
|
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|