AN-NUUR
Na.156 Rabi' Awal 1419, Julai 4 - 9, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Asiye na elimu kwa mujibu wa Biblia

Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

NIMESOMA kwa mshangao mkubwa maoni ya Ndugu John Maki aliyoyatoa katika gazeti la AN-NUUR No. 150, akimshutumu Ndugu Mohamed Said kuhusu ukosefu wa elimu kwa Waislamu. 

Nimeshindwa kuelewa lengo la Ndugu Mtaki ni nini. Je, ni kweli alichokisema anakiamini? Au hakiamini bali anataka kupotosha (distortion) "mashambulizi" ya Waislamu ambayo yameanza kuonyesha mafanikio, kwani sasa hata vizito ndani ya serikali wameanza kuyaunga mkono wazi wazi. Hivyo anataka badala ya Waislamu kuendeleza mapambano ya kudai haki zao zote, wabaki kupigia kelele suala la elimu tu ili wakandamizaji wapumue na kutafuta mbinu mpya za kuwakaanga Waislamu.

Kama ni kweli Ndugu Mtaki anakiamini alichosema, basi tatizo kubwa linalomkabili inaonekana ni kuto kuwa msomaji wa magazeti ya AN-NUUR . Kwani endapo angekuwa msomaji mzuri, asingeandika alichoandika, kwa kuwa majibu ya alichoandika kuanzia madai ya elimu na "hofu" ya kuvurugika amani kutokana na madai ya Waislamu, vyote vimejibiwa katika AN-NUUR No.147 Uk. 10-11. Katika kurasa hizo, ndugu yangu Maalim Mwalim alizungumzia propaganda zilizomwathiri kifikra bwana Mtaki, ndugu yangu Masoud M. Said akaeleza maana ya elimu na vituko walivyofanyiwa Waislamu ili wasipate elimu, nami nikafasiri neno "amani" kwa tafsiri ya kawaida (theoretical definition) na tafsiri kulingana na hali halisi (actual definition). Ama kama asingeridhika na maelezo yetu, basi angetuparamia sisi badala ya kumparamia ndugu yangu Mohamed Said aliyetueleza kwa ufasaha historia ya Mzee Tewa Said Tewa na mchango wake katika Uislamu. Elimu haikuwa ‘gender issue" ya Ndugu Mohamed Said. "Gender Issue" ilikuwa historia ya Mzee Tewa jinsi alivyotumikia taifa na Uislamu na mikasa iliyomkumba kutokana na harakati zake. Hivyo kama ni upinzani (dispute), Ndugu Mtaki ange-challenge hiyo "gender issue" badala ya kuvamia vitu visivyohusika. Angalau angesema "Hakukuwa na mtu aliyeitwa Tewa Said Tewa "au "Tewa Said Tewa hajawahi kuwa Waziri" au "Tewa alifukuzwa Uwaziri baada ya kuiba nyama ya nguruwe msikitini", n.k.

Tatizo lingine linaloonekana linamkabili Ndugu Mtaki ni kuangalia uislamu kwenye miili ya Waislamu hasa masheikh. Anadhani kila kitendo kinachofanywa na sheikh kina uhusiano na uislamu. Lakini hapa lazima nikiri kuwa, vituko, vitimbwi na viroja vya masheikh vinakwamisha sana watu kuukubali Uislamu na vinadhalilisha sana Uislamu. Mimi mwenyewe nimeukubali Uislamu baada ya kuuchunguza kwa miaka mitatu. Na nilisilimu baada ya kuhakikisha kuwa, hirizi, unajimu, ramli, kunywa kombe, kufuga majini n.k. havina uhusiano kabisa naUislamu. Bali ni maasi makubwa na ni njia ya baadhi ya masheikh ya kuwaibia watu. Aidha nilipogundua kuwa shughuli nyingi za pilau, halua, maandazi n.k. ni bidaa (uzushi) zinazong’ang’aniwa na baadhi ya watu kutokana na uroho wao wa ubwabwa na kuwatapeli watu pesa wakisingizia ni sadaka. Naomba wenye mchezo huo waache ili watu waukubali Uislamu kirahisi, kwani wataona Uislamu ni safi sana na mwepesi. Amesema Mwenyezi Mungu (s.w.) "…..Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini…." Qur. 22:78.

Nikirudi kwa Ndugu Mtaki namweleza kuwa, Uislamu umehimiza sana kutafuta elimu za ina zote. Zipo aya na hadithi nyingi sana za Mtume (s.a.w.) zinazohimiza hilo. Hapa nanukuu hadithi moja tu. Amesema Mtume (s.a.w.) "Itafuteni elimu ijapokuwa iko katika miji ya China, kwani kutafuta elimu ni wajibu (lazima) juu ya kila Mwislamu. Katika maneno hayo ya Mtume (s.a.w.),tunaona anawalazimisha Waislamu waende hata kwenye miji ya /china kusoma, na kwa wakati huo China hakuna hata harufu ya Uislamu wala elimu ya Kiislamu iliyoitwa na Ndugu Mtaki "elimu akhera". Kwa hiyo aliwataka wakasomee udaktari, uhandisi n.k. masomo yanayoitwanaNdugu Mtaki "elimu:.

Lengo la makala hii, sio kulumbana naNdugu Mtaki kuhusu elimu. Majibuyote ya ndaniyake, yako katika AN-NUUR Na. 147. Namshauri asome makala hizo. Aidha aangalie orodha ya watu waliochangia kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika AN-NUUR Na.150, aone kati ya Waislamu na Wakristo nani waliochanga fedha nyingi. Aangalie kati ya Mr. Salum Athumani na J.K. Nyerere nani katoa pesa nyingi. Japokuwa majina yanaweza kupotosha ukweli, kwani kuna Wakristo wenye majina ya Kiarabu, na kuna Waislamu wana majina ya Kiingereza, Kirumi, Kifaransa (kama langu) n.k. hata hivyo nadhani katika orodha hiyo wengi ni Waislamu. Ndugu Mtaki asiporidhika na maelezo hayo, basi awaparamie Ndugu Masoud au Maalim Mwalim, lakini kwa ushahidi (points) sio kwa propaganda.

Lengo la makala hii ni kueleza faida za elimu na kujua ni nani mjinga au mpambavu kwa mujibu wa maandiko matakatifu (Biblia).

Neno "elimu" kwa mujibu wa tafsiri aliyotumia Ndugu Masoud M. Said japo ilitolewa na mtu wa aina ya Ndugu Mtaki, ni ujuzi na maarifa yanayo mfanya mtu ayatawale mazingira yake. Nami sina sababu ya kufafanua ma-Encychlopaedia bali natumia tafsiri hiyo hiyo ya akina Mtaki. Ka mujibu wa tafsiri hiyo, faida kubwa inayotarajiwa kupatikana kutokana na elimu, ni kuyadhibiti mambo yote yanayomhusu mtu (kimwili na kiroho) na kutodanganywa kirahisi na watu wasio na elimu inayohusika.

Itakuwa ni kitu cha ajabu sana msomi wa geography alaumiwe na mtu asiye na elimu kama mimi kuwa, mkoa wa Dodoma umezungukwa na bahari ya Hindi, akakubali. Kisha mbumbumbu mimi nikamwomba msomi huyo anipe nauli ili nikapande Meli M.V. Bukoba katika bandari ya hapa Korogwe ili niende Dodoma nilikoitwa nikawe meneja wa shamba la chai Kongwa. Akanipa nauli na kuniongezea fedha ya kula nitakapofika katika bandari ya Iringa. 

Naye mtaalamu wa phisics and engineering science atashangaza sana akimwamini mtu aliyevaa joho la chuo kikuu akimwambia kuwa, formular ya kutafuta density ni Force times distance over work done, na kuwa unit ya density ni ampere. Wakati huo huo mtaalamu huyo akatamba kuwa ni engineer wa meli. Naye bingwa wa hesabu atachekesha sana akijiwa na mtu aliyevaa joho, kofia kubwa na msalaba uliolala tumboni na kumwambia kuwa, 1+1+1 = 1, alalina;o walato ueue mo nomgwa wa Quadratic equation. Kwa hiyo haitazamiwi kabisa mtu mwenye elimu adanganywe na mtu asiye na elimu hata kama huyo mwongo atatumia kisingizio cha dini kuhalalisha uongo wake.

Sasa tuone nani ni mtu mjinga kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Biblia inasema "mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara (elimu) huangalia sana aendavyo", Mithali 14:15. Hapo neno la Mungu linafafanua kuwa, mjinga (asiye na elimu) ni yule anayeamini haraka haraka kila anachoambiwa bila kutafakari kwa kina na kuhoji usahihi au uwongo wa anachoambiwa. Akiambiwa Dodoma kuna bahari anakubali, akimbiwa mlo kamili (balanced diet) unasababisha utapio mlo anakubali; akiambiwa 2 + 1 = 1 anakubali. Na mtu msomi (mwenye busara) ni yule anayehoji kila anachoambiwa. Akiambiwa maji ni mchanganyiko wa hewa mbili, hydrogen na oxygen (H2O) anakataa na kuhoji vipi hewa ziwe maji. Hadi apelekwe maabara (laboratory) ziunganishwe atom mbili za hydrogen na atom moja ya oxygen aone tone la maji linatokea ndio akubali. Akiambiwa umeme unatumika kwenye taa majumbani (alternating current) sio unaotumika kwenye radio humo humo nyumbani, anakataa nakusema "mwongo mkubwa mbona vyote vinatumia supply moja".Hataamini hadi umfungulie radio umuonyeshe rectifier circuit inayobadilisha umeme wa alternating current (AC) kwenda direct current (DC) ndio akubali.

Sasa tujiulize wenyewe nani mwenye elimu kwa mujibu wa biblia kati ya Mkristo anayekubali kuwa Mungu Baba + Mungu Mwana + Mungu Roho Mtakarifu ni Mungu Mmoja, na sisi Waislamu tunaohoji kwa nini awe mmoja na si watatu kwa mujibu wa kanuni ya kujumlisha? Na kwa kuwa haiwezekani tuwe na Miungu Watatu, ndio maana tunakataa uungu wa Mtume Yesu (a.s.) na Roho Mtakatifu ili tubaki na uungu wa Mwenyezi Mungu, Mungu peke yake. Au nani mwenye elimu kati ya mimi niliyeishia darasa la tatu kwa kupenda madogori ninayesema "Injili sio Agano jipya" (Angalia AN-NUUR No. 145 Uk. 10) Wanatheologia wakashindwa kukanusha, na mwenye "masters in trinity" anayeshindwa kufafanua vipi 1 + 1 = 1 = 1 badala ya 3 na kuomba "msaada" serikalini kwa kisingizio cha mihadhara ya kashfa?

Namaliza kwa maneno matakatifu yafuatayo:- "Akili za mwenye busara (elimu) ni kujua njia yake; lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu". Mithili 14:8. "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni njia ya mauti." Mithali 14:12. "Heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu." Mhubiri 4:13. "Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; upumbavu wake hautamtoka." Mithali 27:22.
 

Juu 
 

YALIYOMO
 
TAHARIRI 

Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini 

Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani

Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke

Serikali kuzuia mahubiri ya Waislamu, kuvamia Msikiti, kukamata, kudhalilisha na kuua Wananchi ni kuvunja Katiba na Sheria za Nchi

Kujua lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Na Sadick M. Sadick"

Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi

Intifada ndio jibu (2)
Na Sheikh Pandukizi Dilunga

Kusema ukweli ni sehemu ya uadilifu
A.S. Chachika

Mafumbo ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Na J. Hussein

Majibu kwa Kamara Kusupa

Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai

Asiye na elimu kwa mujibu wa Biblia
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

TAMTA yaadhimisha miaka 36
Na Masoud Mohamed Said, Tanga

Muumini aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Na Muhibu Said

Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30

Habari za Madrasa

Barua 

Mashairi 

Lishe : Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili 
Na Dk. Ali. A. Mzige
  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita