|
|
| Wakwama
kujenga msikiti kwa miaka 30
WANAFUNZI Waislamu wa Shule ya Sekondari ya Same wamekwama kujengea msikiti wao katika eneo la shule kwa miaka thelathini sasa. Awali mwaka 1968 wanafunzi Waislamu wa Shule ya Sekondri ya Same waliamua kujijengea msikiti hapo shuleni ili kurahisisha ufanyaji wa ibada. Matarajio na malengo ya awali yalikuwa kwamba wanafunzi wangejitolea kufanya kazi zote za ujenzi kwa mikono yao kama utengenezaji wa matofali. Katika barua yao Na.9/3/99 ya Septemba 12, 1968, wanafunzi hao Waislamu waliwaomba Waislamu wa mji wa Same kuchanga fedha za kununulia vifaa vya kujengea msikiti huo. Hata hivyo toka wakati huo mpaka leo msikiti huo haujajengwa. Wizara ya Elimu kupitia barua yake No. EDS.A1/63/90 ya Mei 14, 1968 na EDS/A1/68/99 ya Septemba 18, 1971 ilitoa ruhusa na kuhimiza ujenzi wa msikti huo. Hata hivyo mpaka leo haijulikani kulitokea nini kwani mpaka leo msikiti huo haujajengwa. Waislamu wa Same ambao walitarajiwa kutoa msaada mkubwa kwa msikiti huo wa Shule ya Sekondari Same wanyewe wamekwama kujenga msikiti mkuu wa mji huo na mpaka leo wanaswalia gofu la toka wakati wa Mkoloni ambalo laweza kuanguka wakati wowote. Katika hali hiyo ya kukwama Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Gladness Mziray ameamua kulipa shukrani kwa kura alizopewa kwa kusaidia ujenzi wa Msikiti huo wa Same. Mbunge huyo Mhe.Gladness amekuwa akiwasiliana na wafanya biashara wakubwa jijini Dar es Salaam kuwaomba wachangie ujenzi wa msikiti huo. Katika barua yake No. NWA/SAME/2/3/98 ya Machi 2, 1998 amemwomba Mkurugenzi wa Kampuni ya Farai Ginnery (DSM) na Marafiki zake watoe mchango kusaidia ujenzi wa msikiti huo. Mwandishi wa habari hizi hakuweza kujua mara moja iwapo kinachokwamisha ujenzi wa misikiti hiyo ni Waislamu wa Same kukosa fedha au ni ajizi tu na kutokuthamini misikiti huku wakijali zaidi maslahi yao binafsi. |
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|