AN-NUUR
Na.156 Rabi' Awal 1419, Julai 4 - 9, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Sisi wanawake wa Morogoro tunalaani mauaji ya Waislamu yaliyofanywa na Polisi Mwembechai, Dar es Salaam, tunalaani kudhalilishwa na kunyanyaswa kwaWanawake wa Kiislamu mikononi mwa polisi na magerezani.

Sisi wanawake wa Kiislamu wa Morogoro tunalaani matumizi ya mabavu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na hususan kitendo cha askari polisi kuvamia na kuunajisi msikiti, kuwapiga na kuwatesa Waislamu na raia wengine kinyume na taratibu za kisheria

Sisi wanawake wa Kiislamu wa Morogoro tunaunga mkono kwa dhati tamko na maazimio ya mkutano wa Wanawake wa Kiislamu wa tarehe 7/6/98, Masjid Nur-Sinza, Dar es Salaam na tunaitaka serikali iyafanyie kazi kwa kuwa roho za Waislamu na heshima ya wanawake wa Kiislamu si vitu vya kuchezewa.

Sisi wanawake wa Kiislamu wa Morogoro tunatamka ya kuwa tunaunga mkono juhudi za Kamati ya Kupigania Haki za Waislamu Tanzania (kamati ya Ponda) katika kusimamia na kufuatilia haki za wote walioathirika kutokana na kadhia hii

Sisi wanawake wa Kiislamu wa Morogoro tunatamka ya kuwa tunaungana na akina Wanawake wenzetu wa Kiislamu kote nchini katika juhudi za kufuatilia haki za Waislamu kufuatia kadhia hii na tunatoa ahadi yakuwa hatutarudi nyuma wala hatutohofu mpaka haki ipatikane na wote waliohusika na mauaji ya Waislamu na waliowaadhiri Wanawake wa Kiislamu watakapochukulia hatua za kisheria. 

Sisi Wanawake wa kiislamu wa mkoa Morogoro tunaunga mkono Kauli na Hoja ya mbunge wa Kigamboni Mh. Kitwana Kondo alizozitoa mbele ya Waandishi wa Habari na kule Bungeni. Na tunaitaka Serikali ifanyie kazi Kauli hizo. 

Sisi Wanawake wa Kiislamu wa Morogoro tutakuwa nyuma ya Maimamu na Masheikh wetu watakaosimama kueleza dhulma dhidi ya Waislamu na upendeleo kwa Wakristo hasa wa kanisa Katoliki unaofanywa na Serikali ya nchi hii. Na tunamuunga mkono Sheikh mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Omar Bafadhil kwa jitihada anayoifanya hivi sasa ya kutetea Haki za Waislamu.

Wanawake wa kiislamu Mkoa Morogoro 
 

Juu 
 
YALIYOMO
 
TAHARIRI 

Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini 

Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani

Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke

Serikali kuzuia mahubiri ya Waislamu, kuvamia Msikiti, kukamata, kudhalilisha na kuua Wananchi ni kuvunja Katiba na Sheria za Nchi

Kujua lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Na Sadick M. Sadick"

Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi

Intifada ndio jibu (2)
Na Sheikh Pandukizi Dilunga

Kusema ukweli ni sehemu ya uadilifu
A.S. Chachika

Mafumbo ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Na J. Hussein

Majibu kwa Kamara Kusupa

Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai

Asiye na elimu kwa mujibu wa Biblia
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

TAMTA yaadhimisha miaka 36
Na Masoud Mohamed Said, Tanga

Muumini aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Na Muhibu Said

Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30

Habari za Madrasa

Barua 

Mashairi 

Lishe : Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili 
Na Dk. Ali. A. Mzige
  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita