|
|
| WALIOKAMATWA
MWEMBECHAI
Muumini aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
MUUMINI mmoja jijini, Bw. Ali Mohamed Mpanjile (44) ambaye ni mmoja kati ya watu 68 walioachiwa huru na mahakama ya Kisutu,jijini, hivi karibuni, amelaani vikali mateso wanayofanyiwa Waislamu walio mahabusu katika gereza la Segerea kwa chuki za kidini. Akiongea na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake, Manzese Sisi kwa Sisi, hivi karibuni, mwaka huu, siku chache baada ya kuachiwa huru na mahakama hiyo, Bw. Ali alisema, kutokana na suluba wanazozipata Waislamu gerezani hapo zimesababisha atolewe gerezani akiwa na ugonjwa wa ngozi mwili mzima. Mwandishi wa habari hizi aliyemtembelea nyumbani kwake, alimshuhudia Bw. Ali akipata taabu kwa kujikunakuna kutokana na mwasho anaoupata mwili mzima ulioenea upele wenye vidonda ambavyo kwa jinsi vilivyo, vimeigeuza ngozi yake na kuifanya kuwa mithili ya ngozi ya kenge! Akielezea jinsi alivyokamatwa na kupelekwa gerezani, Bw. Ali alisema, siku ya Ijumaa ya Februari 13, 1998, majira ya saa tisa mchana, mara baada ya kuvamia msikiti wa Mwembechai na kuua Waislamu, polisi walifika na kumkuta ameketi kibarazani kwa ndugu zake,hapo Manzese Sisi kwa Sisi na kumkamata,kumtesa na kisha kumtupa ndani ya karandinga la polisi. Alisema pamoja na kukana kuhusika vurugu. Hata hivyo, alisema utetezi wake huo haukusaidia kitu mbele ya mapolisi hao walimkamata na kuendelea kumpa mateso. Alisema mateso aliyoyapata baada ya kukamatwa na kabla yakupandishwa kwenye gari hilo la polisi ni pamoja na kupigwa vibaya mabuti, virungu sehemu za mgongoni, mbavuni na kichwani hatua ambayo alisema ilimsababishia maumivu makali mwilini hadi anaingizwa gerezani. "Polisi hao walinipiga sana kwa virungu sehemu za mgongoni, kichwani na mbavuni hadi kunichania kanzu yangu niliyokuwa nimeivaa siku hiyo huku wakinisimanga kwamba ndio Mujahidina wenyewe hawa. Hata baada ya kutusukumiza wakitutupa ndani ya gari (karandinga) walitutesa sana kwa kutukanyagakanyaga tumboni, wakati huo tulikuwa hatujiwezi kutokanana kuelemewa na kipigo hicho", alisema kwa uchungu Bw. Ali. Bw. Ali alisema mara baada ya kufikishwa gerezani walivuliwa nguo zote na kubaki uchi kama walivyotoka tumboni bila ya kuwatenganisha na watoto wenye umri mdogo na kuanza kupekuliwa kila mmoja. "Baada ya hapo tulianza kupewa adhabu ya kuruka kichurachura sisi wote, anayesita basi anapigwa virungu hovyo mwilini. Tulirukishwa kichurachura tukiwa uchi", alisema Bw. Ali. Pamoja na adhabu hizo, Bwana Ali alisema baba yake mzazi alipeleka gerezani vyeti vya Hospitali kuthibitishakwamba Bw. Ali aliingizwa gerezani hapo akiwa ni mgonjwa wa TB. hivyo anahitaji kupatiwa dawa lakini vyeti hivyo vilikataliwa bila maelezo yoyote yamsingi. "Hata huko gerezani hatukupewa dawa ya maradhi husika zaidi ya kupewa sote dawa ya aina moja bila kujali ugonjwa wa mtu", alisema. Bw. Ali ni mmoja kati ya Waislamu waliotuhumiwa kuhusika navurugu zilizotokea maeneo ya msikiti Mwembechai kwa awamu tatu tofauti, baada ya polisi kuvamia msikiti huo hapo Februari 12, na 29, mwaka huu. Hata hivyo, Bw. Ali pamoja na watuhumiwa wengine 67 waliachiwa huru na mahakama ya Kisutu mapema Juni 8, mwaka huu. |
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|