|
|
| TAMTA yaadhimisha
miaka 36
Na Masoud Mohamed Said, Tanga TAASISI ya TAMTA Almadrasat Shamsiyah mwaka huu (1998) imetimiza umri wa miaka 36 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1963 na Almarhum Sheikh Muhammad Ayoub. Maadhimisho ya mwaka huu ambayo yameachana kwa siku chache na siku ya maadhimisho ya Maulid ya Nabii Muhammad (s.a.w) ndiyo ya mwanzo kufanyika bila kuwepo muasisi wake huyo. Shamrashamra za sherehe hii maarufu kwa jina la "TAMTA Day" zilianza Jumamosi ya Juni 27. Wananchi waliokuwa bado hawajayasoma matangazo ya sherehe hizi, walielewa wakati vijana na wazee walipokuwa wakirejea kutoka Manyanjani kwa maandamano ya baiskeli na pikipiki huku wakiwa wameshika na kuchomeka kwenye vilemba matawi ya miti ya Pwani ambayo pia iliyoenea katika mitaa yote, kuanzia barabara ya 14 mpaka Msambweni yaliko Makao Makuu ya TAMTA. Wengi walidhani ni askari wakiwa kwenye operesheni fulani za kijeshi. Siku mbili zilizofuata zilikuwa ni za maonyesho ya kielimu ya wanafunzi wa zamani wa kike na kiume. Mnamo siku ya kilele Juni 30, ilikuwa ni zamu ya maandamano ya magari. Yakipishana kwa vitambo vifupi na yalionekana yakiingia mjini kutoka kila pembe ya mji, tangu mapema asubuhi. Wakati wa usiku, wawakilishi wa baadhi ya matawi 80 ya TAMTA walionyesha taaluma zao na kufuatiwa na Samai. Mudiir mpya Sheikh Muhammad Bakar baadaye alisimama kusoma historia ya marehemu Sheikh Muhammad Ayoub kwa njia ya mashairi ya Kiarabu ambayo yalitafsiriwa pia kwa Kiswahili. Akifunga sherehe saa 5.30 usiku, mlezi wa TAMTA, Sheikh Abdallah bin Ayoub alitoa shukrani nyingi kwa ushirikiano mkubwa uliopatikana kwa jina la Uislamu. Alisifu ushujaa na ukakamavu wa Mudiir mpya Sheikh Muhammad Bakar ambaye pamoja na mambo mengine imeelezwa kuwa alifanikisha sherehe za mwaka huu. Mwisho, alitoa wito kwa Waislamu popote walipo wasitoe
njia kwa Shetani kukaribia ibada na mambo yao.
|
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|