|
|
| Jibu
kwa Kamara Kusupa
Na Ismail Abdullah NINGEPENDA kumjibu Mwinjilisti Kusupa katika makala yake ya AN-NUUR Na. 152. NDUGU Kusupa badala ya kujibu hoja za Ndugu Mohamed Said kama angeona kuwa hoja za Ndugu Mohamed si yakinifu bali ni bunifu zenye kujenga dhana tu. Kitu ambacho, Muinjilist hakufanya, bali ameingia kumuhakiki Ndugu Mohamed kwa vigezo vya riwaya za fasihi simulizi au andishi. Ndugu Mohamed hakuwa ameandika riwaya bali yeye kama mwanahistoria mtafiti aliwakilisha utafiti wake tu. Na ndiyo anavyofanya Ndugu Mohamed katika makala zake zote, hata zile za awali. Haandikii hadhira ya aina mojahuandika hadhira mbali mbali kila mtu atatumia kinyake: wanahistoria watafiti wenzake, wanasiasa, viongozi wa dini, serikali n.k. Huu ndio mtindo wake na ndio mtindo mzuri wa kuwakilisha utafiti, bila ushabiki na jazbaa. Sasa Ndugu Kasupa, unataka Ndugu Mohamed atoe hitimisho kwa hadhira gani? Na kwa nini yeye kama msomi aliyebobea alalie upande mmoja, kwa jambo lenyefaida kwa wengi. Mtafiti katika maabara hospitalini, atafanya uchunguzi kwa mgonjwa na atamuacha mgonjwa apeleke uchunguzi wake kwa daktariyeyote yule, amuandikie dawa yoyote ile, itakayomfaa mgonjwa. Ndibvyo anavyofanya, Ndugu Mohamed Said katika makala zake. Ama ulivyosema Mwinjilist katika makala yako kuwa malalamiko ya Waislamu yasije yakawa ni malalamiko mithili ya uke wenza lakini hivyo ndivyo ilivyo hasa, usikatae. Mfano mzuri ni kutoka kwako, Waislamu wanailalamikia serikali, lakini anae jibu haraka haraka ni Mwinjilisti. Kama si uke wenza basi ni nini hiyo? Uke wenza hauna ubaya, ali mradi mume awe mwadilifu. Mambo ni Khamsini kwa Khamsini, Bungeni, Maofisini,Viwandani, Ijumaa na Jumapili n.k. Ndivyo ilivyo Mwinjilist, wewe huyajui hayo. Mambo ya mshale mrefu na mshale mfupi, mchezo wa saa, mchezo wa kitoto, hatuupendi mchezo huo, japo ni mchezo Mchezo wenu ndio mauti yetu. Etimshale mfupi,hanaruksa ya kwenda mpaka mshale mrefu aende hatua sitini, ndio yeye mshale mfupi aende hatua tano. Kwa betri ile ile. Si utaki mie mchezo huo. Hatuutaki. Kwa nini sote tusiwe mithili ya macho mawili. Pambo kamilifu namadhubutikwa mwanadamu? Ilisura ipendeze kwa kila mwenye kutazama. Kuna ubaya gani kuwa hivyo? Ka nini hutaki? Ama Ndugu Mwinjilist umejitahidi kuchora taswira kuwa Mwalimu Nyerere aliyo yafanya, aliyafanya kwa hulka yake yeye binafsi.Ukatoa ushahidi wa Wakristo walio athirika na hulak hiyo. Ningependa kukukumbusha, kuwa wazee wa Kiislamu, walimpokea Mwalimu kwa mikono yoe miwili, bila kumbagua kuwa alikuwa Mkristo. Lichaya kuwa Mwalimu hakuwa amewafundishia watoto wao. Mwalimu hana mtoto wa Kiislamu alie mfundisha. Kabla ya hapo, hakuwa amefanya kazi na Waislamu. Yeye licha ya kusomea shule ya serikali ya Tabora, alipokutana na Waislamu wachache wanafunzi wenzake, yeye alikuwa Mwalimukatika hsule za Misheni. Waislamu hawakulijali hilowalimpokea nakushirikiana nae. Leo anatuhumiwa kwa tuhuma nzito nzito dhidi ya Waislamu, yeye yupo hai jasiri wa kusema, hajibu bali amekaakimya. Huenda anakubali hizo tuhuma. Wewe Mwinjilist unakurupuka huko na kumsemea. Vipi? Tueleze basihizo sababu, za kuvunja chombo cha Waislamu kilicho kuwa kinajenga chuo kikuu cha Kiislamu miaka thelathini iliyopita hata mimba ya "Tumaini University" haijashika, si ajabu mama yake "Tumaini". Hata kuolewa alikuwa hajaolewa. Huu si ndio ule mchezo wa saa? Mshale mrefu na mshale mrfupi? Ndugu Mwinjilist? Mbwa mwitu wana tabia moja. Wanapokula mzoga wao, hawaruhusu mnyama mwingine yoyote asie kuwa mbwa mwitu kusogelea pale, na kula pamoja nao. Kwa sababu sio mbwa mwitu mwenzao. Na mbwa mwitu yeyote anaemega kipande chake cha nyama, akaenda kando akala, basi akimaliza sharti apanguze midogomo yake kabla ya kurudi kumega kipande kingine. Akirudi na damu midomoni mwake bila kujipangusa basi wenzakewatamshambulia nakummaliza. Lakini sio kwa sababu yeye si mbwa mwitu? La! Bali kwa sababu nyingine kabisa. Mwalimu aliwalima Wakristo kwa sababu tofauti na za Wailsamu kwa ajili yaya Uislamu wao. Ndugu Mwinjilist usiwalaumu Waislamu kwa kutowatetea wale wasio Waislamu, ambao nao hawakupata elimu. Sababu zao za kutopata elimu ni tofauti kabisa na uonevu wa wazi umeofanyiwa Waislamu. Baada ya kuwapora Waislamu hata hivyo nafasi hazikuwa tosha wote ndio wengine wakakosa. Kumbuka kuwa dhalimu,mbaguzi ana tabia iliyomvaa ithili ya ngozi na nyama. Akisha kubagua kwa misingi ya dini, akabakia na watu wa dini yake. Basinao huanza kuwabagua kwa rangi zao, kabila, ukoo, n.k. Amerika ya kusini,nchi kama za Brazil n.k. Idadi yao kubwa ni Wakatoliki. Lakini kuna malalamiko kuhusuubaguzi wa viongozi wa dini kuwapendelea weupe zaidi kuliko weuzi. Pia tazama Ruanda na Burundi idadi yao kubwa ni dini moja, lakini, dhalimu amewafunisha kubaguana na kuuana kwa ajili ya tofauti za urefu wa pua zao. Ndugu Mwinjilist kama unataka Waislamu watetee haki za watu wote dini zote, basi washaurihao unao wajua wewe kuwa wanadhulumiwa walete malalamiko yao ya kudai haki kwa wote. Ahsante sana kwa pole zako zimefika, na sisi tunasema Mungu si Athumani.
Mwinjilisti Kamara Kusupa umeachwa nyuma miaka mitano, kimbia BAADA ya kumuhimili Allah na kumtakia rehema Mjumbe wa Allah (Muhammad s.a.w.) napenda kuomba nafasi katika gazeti lako tukufu kuchangia hoja ya dhulma dhidi ya Uislamuna Waislamu kama ambavyo imekuwa ikijadiliwa katikamatoleo yaliyotangulia. Napenda kufikishaujumbewangu kwa hoja moja itakayofuata hivi punde. Mwandishi Kamara Kusupa inaonekana kwamba mpaka sasa upo katika harakati ya kusoma historia hivyo matukio yanayotokea sasa hivi yanakupita huko ulikokatika maktaba yako ya kuufundishia historia. Hii itakufanya kila siku ubaki ukiuliza maswali katika magazeti maana watu wakiona na kufanyia kazi wewe uko kwenye historia zilizopita zamani. Kwa sasa hivi inaonyesha dhahiri, upo katika harakati za kujifunza jinsi serikali ya Wamuya Pili ilivyoendeshwa. Kitu kinacho kufanya endelee kuchelewa yanayofanywa na serikali ya awamu ya tatu (awamu ya Mkapa). Hata hivyoinakuwia vigumu kufanyia uchunguzi hoja zilizotolewa na mwandishi wa awali na kujua malengo yake matokeo yake unalazimisha maswali ambayo si kazi ya mwandishi kuyatolea suluhisho bali hivyo ni kazi ya vyombo husika ambayo mwandishi amevitaja katika maelezo yakeyote. Leo naomba uache historia japo kidogo ili twende pamoja katika mambo ambayo bado haya hitaji kumbukumbu za zamani ili uone mwenyewe serikali ya Awamu ya Tatu inavyofanya huenda ikakupa hata urahisi wakati wa kurejea historia yako. Hekaheka zilizotokea hivikaribuni katikavikundi vya dini mbili hizi pinzani yaani Uislamu na Ukristo; hali hii iliibuka baada Wakristo kugawa biblia kwa Waislamu ili waisome kwa lengo la kuelewa biblia na ikiwezekana Waislamu wavutike na KURITADI. Baada ya kukisomakitabu hicho wakaona Wakristo wanaenda kinyume na maandishi yaliyomo ndani ya kitabu hicho,kwa mfano kumuita Isa mwana wa Manamu ni Mungu wakati ni kinyume na mafundisho ya kitabu hicho.Maswali yakaanza kutoka katika vikundi vya khidima Daawat Islamiya Al-Maldi kwa upande wa Waislamu. Biblia ni jibu wakasema watatetea hoja na wakanza kufanya hivyo. Mafanikio yavikundi vyote hivyo yalionekana katika hashara mbali mbali. Serikali ya Awamu yaTatu ilifanya juhudi ya kuvikemea vikundi hivi kuwa vina chochea vurugu ndani ya pande hizi mbili za waumini. Katika sakata hilo wahadhiri wa vikundi hivyo mashuhuriwalitiwa katika mikono ya dola kwa kosa la kile walichokiita mihadharaya kashfa. Ustaadh Shaabani Magezi alikuwa wa kwanza kukamatwa. Kwa kosa la kukashifu dini za watu wengine ndani ya serikali inayojiita haina dini lakini inajua kashfa yadini; kwa hilo hilo na wakatihuo huo Muhadhiri wa Biblia ni Jibu Simba Ulanga alikamatwa natuhuma kama za Magezi na wote kufikishwa ikavyombo vya dola. Matokeo yake ambayo nafikiri wewe na kundi lako bado haujayapata kutoka na misks miysno yulioessvhs mkiysguys hidyotis. Drtiksli yryu imrgsnys ksms igusysbyo: Ustaadh Shaaban Magezi (Mwislamu) ameshikiliwa na polisi hadi hivi sasa na anaambiwa hana haki ya kupata dhamana kutokana na kwa lake hilo wakati huo huo SimbaUlanga wa Biblia ni Jibu aliyekuwa akishikiliwa kwa kosa hilo hilo yeye amepewa dhamana zamani sana bila masharti na kesi yake haijasikika kutajwa hata siku moja. Kwa mtizamo huo wee Kasupa unataka uwaeleze nini Waislamu juu ya dhuluma dhidi yao. Kuwa serikali haiwafanyi kama tambara la kufutia nyayo? Kwa mtizamo huo lazima Waislamu wadai hakizao. |
Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|