|
|
| TAHARIRI
S.L.P. 55105, SIMU 181365, DSM Hatutaki Hekaya za Abunuwasi WIKI ijayo Waislamu nchini watasherehekea uzawa wa Mtume (s.a.w.) ambapo yatasomwa Maulid na kufuatiwa na Baraza la Maulid. Sherehe hizi zina umuhimu wake, kwa sababu ni siku aliyozaliwa Mtume wa mwisho aliyekuja kuhuisha ujumbe wa dini ya Baba yetu Adamu, Ibrahimu, Mussa, Issa (a.s) n.k. Hata hivyo, sherehe hizo zitakuwa na manufaa zaidi endapo mtizamo na mwelekeo wa sherehe zenyewe utakuwa wa kuzingatia ujumbe aliokuja nao Mtume (s.a.w.) hasa kwa kuzingatia wakati na matukio na masuala (issues) tunayokwenda nayo. Kwa hakika itakuwa ni kupoteza muda na fedha bure endapo katika sherehe hizo hatutachota katika hazina aliyotuachia Mtume (s.a.w.) tujikwamue kutokana na matatizo yanayotukabili hivi leo. Wapo watu wanasema kwamba walionewa, kupuuzwa na kunyonwa kwa sababu ya unyonge wao. Kwahiyo, ili kujikomboa ni lazima kwanza waondokane na unyonge huo. Muislamu kabla hata hajaumbwa ameambiwa kwamba yeye anakuja kuwa Khalifa. Msimamizi wa dunia kwa niaba ya Allah. Na ili alitekeleze jukumu hilo, vitu vyote vikadhalilishwa kwake. Avitumie kwa manufaa yake. Aidha, dini yake Uislamu ikapewa hadhi kuwa juu ya dini zote, japo watachukia wenye dini zao nyingine. "Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake (Nabii Muhammad) kwa uongofu na kwa dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa makafiri watachukia". (61:9) Kwahiyo, kwa asili yake Muislamu si mnyonge wala Mwenyezi Mungu hajampa sifa ya unyonge. Kule kuikubali Tawheed na cheo cha Ukhalifa ndio ukombozi wenyewe. Maulid hii itukumbushe kwamba, Mtume (s.a.w) hakuwa dhalili mbele ya maadui wa Allah. Hakupiga magoti mbele ya maadui wa Uislamu kuomba kibali cha kuhubiri Tawheed wala haikuwezakana kumzuia kwa mabavu kuifanya kazi hiyo. Maulid hii itukumbushe kwamba, Mtume (s.a.w) hakukubali kudhulumiwa wala kuonewa halikadhalika hakukubali wengine wadhulumiwe au waonewe. Uislamu ni dini ya amani, uadilifu na maelewano. Ni dini iliyoweka msingi madhubuti wa kuishi pamoja watu wa dini, makabila na mataifa mbalimbali (Co-existence) katika hali ya kukubali kutokubaliana. Hatutegemei Masheikh wetu watuletee ngonjera, visa vya Abunu wasi, kasema mshairi, ipo hekaya moja, visa vya wanawake, Israiliyat n.k. Huu ni wakati wenye matukio na masuala (issues) maalum na muhimu kwa Waislamu na mustakbali wao katika nchi hii ya Tanzania. Tunataka Maulid hii itukumbushe Mfalme Najash aliwafanya nini Waislamu wale waliosema "Yesu si Mungu" mbele yake. Tunataka Maulid hii itukumbushe Shaheed Hamza aliwafanya nini wale waliowapiga na kuwaua Waislamu wasio na hatia wala silaha. Tunataka Maulid hii itueleze Mtume (s.a.w) aliwachukulia hatua gani wale waliovunja makubaliano ya kuishi pamoja katika hali ya kuheshimiana na kuchunga haki za wengine. Maulid hii itueleze Mtume aliwachukulia hatua gani wale walioua japo Muislamu mmoja tu bila ya hatia. Maulid hii itueleze wale waliomdhalilsha mwanamke wa Kiislamu walichukuliwa hatua gani. Kwenye Uislamu hakuna ukasisi wala uaskofu kama taasisi ya kutiiwa bila kuhojiwa. Asiyejishughulisha na masuala ya Waislamu hupuuzwa tu bila kujali jina, cheo na nasaba yake, Waislamu wakaendelea na mambo yao ili mradi wana Qur’an yao na mafundisho ya Mtume (s.a.w). Na Maulid hii itawachuja wengi. Waislamu tayari tuwamoja, Mungu wetu mmoja na Kibla kimoja. Wote tukienda Msikitini tunaswali pamoja, kisomo kile kile na rakaa zilezile. Kuwepo kwa Jumuiya na Taasisi nyingi sio alama ya kukosa umoja au ugomvi. Ni vituo vya kazi, lengo letu likiwa moja. Tusingependa kusikia katika Maulid hii zile kampeni za maadui wa Uislamu kwamba eti hatuna umoja, hatuna uongozi, tusigombane, tutumie hekma n.k. Hizi ni kauli za maadui wa Uislamu kutupoteza maboya tuache kuwaangalia walioua pale Mwembechai na kumlemaza Chuki Athumani, tudhani tatizo ni sisi wenyewe. Tatizo ni madhalimu sio umoja wa Waislamu. Tayari umoja tunao, wala hatuzozani. Suala hapa ni dhulma iondoke sio kuwafanya Waislamu wote wawe chini ya Mufti au Kadhi mmoja! Tungependa turejee nasaha zetu kwa Waislamu na hasa Masheikh watakaopewa fursa kusema chochote katika hafla za Maulid zinazoanza rasmi wiki ijayo kwamba tuzitumie vizuri fursa hizo kuyaeleza yale yenye manufaa na Waislamu kulingana na wakati na matukio munasibu. Tutegemee vile vile kwamba katika Maulid hii, Waislamu watapumua. Hawatatiwa majeraha tena kwa kukejeliwa, kukashifiwa, baada ya kuuliwa, kufungwa, kusababishiwa vilema vya maisha na mama zao kudhalilishwa. |
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|