|
|
|
Kuna mbinu kadhaa za kutumia kuweza kukamilisha kazi inayotakiwa na muulizaji wa hilo suali hapo juu, lakini mbinu tutakayoizungumza leo ni kutumia programu moja ya kubana mafaili (file compression software) ambayo naipenda sana, na ambayo kwa bahati mbaya si watu wengi wanaoifahamu. Programu hiyo inaitwa WinRAR. WinRAR ni programu ambayo inafanyakazi sawa kabisa na programu maarufu za kubana mafaili kama vile PKZIP, WinZIP, n.k. WinRAR ni kati ya zile programu zinazoitwa shareware, yaani programu ambazo unaruhusiwa kuzitumia kwa muda kama wa mwezi mmoja hivi na kama unazipenda unalipa pesa kidogo kuweza kuendelea kuzitumia. Unaruhusiwa kutumia programu wa WinRAR kwa siku 40 na zikimalizika unatakiwa kulipa kama dola 35 za kimarekani kuweza kuendelea kuitumia programu hiyo. Kama hukulipa, hata hivyo, utaweza kuendelea kuitumia lakini utakuwa umevunja masharti ya leseni uliyopewa. WinRAR inapatikana kwenye anuani ifuatayo ya web: http://www.creabel.com/softronic Sasa, kwa ufupi tuangalie ni namna gani utakavyoweza kuitumia WinRAR kunakili kutoka kwenye kompyuta moja, faili ambalo ni kubwa sana lisiloweza kuenea kwenye disketi moja, ili uweze kulipeleka kwenye kompyuta nyingine. Njia hiyo hiyo utaweza kuitumia kunakili jalada (directory) ambalo ndani yake yamo mafaili kadhaa ambayo kwa pamoja hayawezi kuenea kwenye disketi moja. Tutajifunza jinsi ya kutumia WinRAR kuweza kubana mafaili, na kuweza kuyakatakata vipande vidogo vidogo vya kuweza kuenea kwenye disketi. Ukishaweza kuiingiza (install) WinRAR kwenye kompyuta yako, fuata hatua zifuatazo ambazo ni sahihi ikiwa utatumia version 2.06 ya WinRAR. Ianzishe WinRAR kama kawaida, na itumie sehemu ya kuangalia majalada mpaka ikuoneshe jalada (au faili) unalotaka kulinakili. Tutatumia mfano wa jalada lenye jina download kama linavyoonekana kwenye Picha 1. ![]() Bonyeza mouse juu ya jalada unalotaka kulinakili. Kama unataka kunakili mafaili zaidi ya moja, unaweza kuyachagua kwa kuyabonyezea mouse wakati umeshikilia kifungo cha Ctrl. Bonyeza sehemu ya Commands na uchague Add files to archive. Kitatokezea kidirisha kama kinavyoonekana kwenye Picha 2 na hapo utachagua mambo mbali mbali kama inavyoonekana kwenye Picha 2. Unaweza kubadilisha jina la archive (yaani jina la faili litakalotengenezwa ambalo ndani yake mtakuwa na mafaili tunayoyataka kuyabana), kwa mfano, badala ya a:download.exe unaweza kuandika a:myfile.exe, lakini ni muhimu liishie na .exe. Hii ni kwa sababu, tumeweka tiki kwenye sehemu ya SFX archive, kwa vile tunakusudia kutengeneza aina ya faili linaloitwa "self-extracting archive" lenye sifa ya kuweza kujifungua lenyewe na yenye extension hiyo yanaweza kuanzishika. ![]() Kwa maneno mengine, baada ya kutumia WinRAR kuingiza mafaili kadhaa kwenye faili moja la archive, hutahitaji tena WinRAR kuweza kuyapata mafaili yako yalio ndani ya faili hilo la archive – lenyewe litajua namna ya kuyatoa mafaili yaliyoingizwa ndani yake, na ndio maana likajuilikana kama self-extracting archive. Kwenye sehemu ya Volume size unaweza kuchagua ukubwa wa disketi zako. Kwa mfano, kwa disketi za kawaida za ukubwa wa 1.44 MB, basi utachagua 1457500. Kama una disketi zenye nafasi tafauti, au kama hujui nafasi iliyo kwenye disketi zako, basi unaweza kuchagua Autodetect. Ingiza disketi tupu kwenye sehemu yake ambayo kwa vile jina la faili tuliliandika limeanza na a: disketi yako itatarajiwa kuwa kwenye drive A. Ukibonyeza OK mambo mawili yatatendeka: kwanza mafaili yote yaliyo kwenye jalada lenye jina download yatabanzwa, yaani yatakuwa compressed ili kuyafanya yawe madogo zaidi ya yalivyo kikawaida. Yanawezwa kupungua mpaka kufikia kama robo tu ya ukubwa wake halisi! Na pili, faili la archive lenye jina download.exe litaanza kunakiliwa kwenye disketi iliyo kwenye drive A. Kama diskette moja haitoshi kunakili kila kitu, utaelekezwa uingize disketi nyingine ambayo itaingizwa faili lenye jina download.r00, na kwenye disketi ya tatu kutaingizwa faili lenye jina download.r01, na kuendelea hivyo hivyo mpaka mafaili yote yamemalizika kunakiliwa. Chukua disketi zako zote na ukifika kwenye kompyuta ya pili, ingiza kwanza kwenye drive A, ile disketi yenye faili download.exe. Bonyeza Start -> Run na uandike a:download.exe kwenye kidirisha kitakachojitokeza. Bonyeza OK na ufuate maagizo utakayopewa ya kuingiza disketi zote kwa mpango maalum. Ukikamilisha hatua hizo utakuwa tayari umeweza kunakili mafaili kutoka kwenye kompyuta moja kwenda kwenye kompyuta nyengine kwa kutumia disketi japokuwa baadhi ya mafaili hayo ni makubwa sana kiasi kwamba hayawezi kuenea kwenye disketi moja. Kwa kutumia WinRAR na kwa utaratibu tulioueleza hapo juu, utaweza kirahisi sana kunakili jalada (directory) zima na majala mengine (subdirectories) yaliyo chini yake pamoja na mafaili yote yaliyo kwenye majalada hayo. Utakapoyaweka kwenye kompyuta ya pili, majalada yote yatawekwa kama yalivyokuwa kwenye kompyuta ya kwanza pamoja na mafaili yake. Binafsi, naitumia sana WinRAR kwa kuweka hifadhi ya dharura (backup) ya baadhi ya mafaili na majalada muhimu yaliyo kwenye kompyuta yangu. Bila shaka tumejadili mambo machache tu, ingawa muhimu, yanayohusiana na WinRAR. Ukitaka kujifunza mambo mengine zaidi ya hayo, angalia Help iliyo kwenye WinRAR. Kazi tuliyoifanya hapo juu pia inaweza kufanywa na programu kama ya WinZIP na nyengine nyingi kama hizo. |
YALIYOMO
Tahari
Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe - Manyema Maoni yetu
DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA Uislamu na Mazingira katika
Umoja wa Mataifa
Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika
Internet
Rais Mkapa atekeleze hadi yake
kwa hadhari
Mashirika ya Dini yaelekeze
misaada vijijini
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma Ni serikali ipi anayoiwakilisha
Sumaye
Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|