AN-NUUR 
Na.187 Shawwal 1419, Februari 5 - 11 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Ni hatari kuwaambia wananchi wasichague chakula 
 
Na Mujahid Mwinyimvua
 

KATIKA kile kinachoonekana na kuwa juhudi ya kukabiliana na baa la njaa nchini Tanzania (1998/99), kiongozi mmoja wa ngazi ya juu serikalini, hivi karibuni amewataka wananchi wa Tanzania kula vyakula bila ya kuchagua. Yaani kwa vile kuna njaa, chochote kitakachopatikana lazima watu wale! 

Wito huo wa kisiasa una hatari na ni kinyume kabisa na kanuni za chakula na lishe. Makala hii imekusudiwa kuweka wazi hatari hiyo na hatimaye kuishauri serikali. 

Kwanza ni vyema ikakumbukwa kuwa tunapokula vyakula, lengo kuu siyo kujaza matumbo kama watu wengi wanavyofikiria. Lengo kubwa katika kula ni chakula hicho kiweze kuupa mwili virutubisho vyote vinavyohitajika kwa ujenzi wa afya bora. Sawia na lengo hilo, chakula pia kisiwe na kiwango kikubwa cha madawa (chemicals) ambayo yanadhuru afya ya mlaji. 

Takriban vyakula vyote vina kiwango fulani cha madawa yanayoweza kuudhuru mwili. 

Kwa mfano, kinywaji cha kahawa kina madawa karibu mia nane (800) yanayopatikana katika mmea wenyewe wa kahawa. Katika madawa hayo, kati ya madawa 21 yaliyofanyiwa utafiti, 16 yanaweza kusababisha ugonjwa wa saratani (kansa) kwa anayekunywa kinywaji hicho. 

Juisi ya machungwa nayo pamoja na faida ya kutupatia vitamini C, ina dawa inayoitwa ‘D-limonene’ ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa saratani. 

Vile vile, juisi ya Epo (Apple) ina madawa karibu 125. Madawa matano kati ya hayo yamefanyiwa majaribio na kuonyesha kwamba madawa matatu (kati ya hayo matano) yanaweza kusababisha saratani. 

Mifano ya vyakula vyenye madawa yanayoweza kuwadhuru viumbe hai iko mingi, lakini itoshe kwa kumalizia mfano huu wa chakula cha muhogo (michungu na ile mitamu) ina dawa ijulikanayo kama Sayanaidi (Cyanide). Sayanaidi ni sumu ambayo inaweza kusababisha hata kifo. 

Zaidi ya hayo, vyakula pia vinatofautiana kiasi cha virutubisho. Pia vyakula vingine vina vitu ambavyo vinazuia mwili kuvipata virutubisho vilivyomo katika chakula (kilicho tumboni). 

Tukizingatia, dondoo za hapo juu ni wazi kuwa swala la kuwahamasisha wananchi waache kuchagua vyakula siyo tu ni kinyume cha kanuni ya chakula na lishe, bali pia ni kinyume na ubinadamu. 

Hali inakuwa mbaya zaidi tunapoitazama Tanzania. Karibu kila mwaka kuna upungufu wa chakula. Mvua zikiwa nyingi mafuriko, jua likiwa kali ukame. Hali zote hizo zinachangia upungufu wa chakula. Kwa hali hiyo, kila mwaka wananchi watawajibika kutokuchagua vyakula, kama wito wa viongozi wa serikali ya Tanzania utatekelezwa na wananchi. Je, hali yao ya afya itakuwaje? 

Ninamalizia makala hii kwa kuishauri serikali kuwa wakati umefika sasa yenyewe binafsi iwekeze katika sekta ya kilimo na pia iweke mazingira mazuri kwa wawekezaji binafsi. Nina imani kuwa kama serikali itawahamasisha wawekezaji kama ilivyofanya kwenye bia (pombe) na sigara, nchi yetu itaepuka baa la njaa la kila mwaka. 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Mauaji ya Mwembechai; Mh. Rais apewe kanda

Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri

Hijab ivaliwe shuleni

Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais

Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe  -   Manyema

Maoni yetu
Kauli ya Waziri Mkuu Bungeni: Tumsikilize nani?

DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA

Mjue Usama bin Ladin -3

Uislamu na Mazingira katika Umoja wa Mataifa
Na Dk.  Wahid

Barua ya wazi kwa Rais Mkapa

Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika Internet
Na. Zituzzaman Hoque

Kutoka magazeti ya zamzni

Rais Mkapa atekeleze hadi yake kwa hadhari
J.R. Msuya, Moshi

Mashirika ya Dini yaelekeze misaada vijijini
Na KAWELE  SAIDI 

Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma

Ni serikali ipi anayoiwakilisha Sumaye
Na Abu Salim

Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni

Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Na SALUM ALI 

Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro

Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel

Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina

Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti

Sayansi na Teknolojia 
[Jifunze ‘Kubana’ Majalada] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Chakula na Lishe 
[Ni hatari kuwaambia wananchi wasichague chakula] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita