|
|
Akizungumza Bungeni Februari 2, 1999 Mbunge wa Kigamboni Mh. Kitwana Kondo alisema kwamba kwa mwaka 1998 watoto Waislamu waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoa wa Dar es Salaam walikuwa asilimia sabini na moja (71%) wakati Wakristo walikuwa 29% ya watahiniwa wote. Hata hivyo, akasema kwamba waliokuja kuchaguliwa kwenda sekondari Waislamu walikuwa asilimia ishirini na moja (21%) wakati Wakristo waliochaguliwa walikuwa asilimia sabini na tisa (79%). Kutokana na kielelezo hicho, Mh. Kitwana Kondo alihoji: "ama Waislamu ni wajinga, ama akili zao hazifanyi kazi " ama mtu akiwa Muislamu basi wewe huna kitu au kuna kitu". Kwa hiyo, akaitaka serikali itoe maelezo. Katika utangulizi wake, akiielezea nukta hii Mh. Kitwana Kondo alikariri ahadi ya Mh. Rais ya kuyashughulikia matatizo ya kielimu ya Waislamu ambapo pia alishauri wafadhili wajenge shule zaidi badala ya Misikiti, lakini akamtaka Waziri wa Elimu atoe ufafanuzi juu ya jambo hili. Kwamba je, watoto wa Kiislamu kutochaguliwa kwenda kidato cha kwanza ni kwamba Waislamu kwa asili yao wanazaliwa wajinga au zipo juhudi za kuwakandamiza. Wakati huo huo, Mh. Kitwana Kondo ameliambia Bunge kwamba yapo mambo ambayo yanapangwa na serikali ambayo yanaweza kuleta mfarakano katika jamii yetu, jambo ambalo Mh. Rais amelikemea. Akitoa vielelezo alitaja suala la siku ya Ijumaa ambapo katika baadhi ya maofisi na mashule ratiba za kazi hazizingatii haki ya Waislamu kwenda kuswali. Ameiomba serikali itoe agizo kwamba shughuli zote za kazi na masomo zisimame saa sita na kama ni kuendelea ziendelee baada ya saa nane. Mfano mwingine aliotoa Mh. Kondo ni tabia ya serikali kuchelewesha usajili wa taasisi za Kiislamu bila sababu zozote za msingi. Alieleza kwamba taasisi moja ya Kiislamu ijulikanayo kama Baraza la Maimamu toka iombe kusajiliwa ni miaka mitatu bado haijasajiliwa. Aidha, alisema kwamba wakati mwingine Waislamu hudaiwa walete kibali cha Bakwata wanapoomba kusajiliwa, akahoji je, hiyo ni sheria ya serikali au matakwa tu ya wakubwa. Suala lingine aliloligusia kama kielelezo cha Waislamu kutokutendewa haki na hivyo kuhatarisha amani ya nchi, ni tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali na hasa katika taasisi za elimu kuwazuia mabinti Waislamu kuvaa hijab. Amesema hiyo ni amri ya Qur’an (33:30-31)na ni lazima iheshimiwe. Akizungumzia suala la mitihani ya kidato cha nne kufanyika mwezi wa Ramadhani, Mh. Kitwana Kondo alisema kwamba hiyo ni moja ya chehe za kuleta mfarakano. Hata hivyo akasema kwamba baada ya manung’uniko Waziri wa Elimu alitoa maelezo ambayo yaliwaridhisha Waislamu. Hata hivyo, akashangazwa na kuhoji dhamira ya wale wakubwa waliosema kwa jeuri na takabari kwamba watoto wa Kiislamu wakitaka kufanya mtihani wafanye na wasipotaka basi. Hakufafanua ni mkubwa gani huyo. Mh. Kitwana Kondo alisisitiza kwamba hao wasiojali hisia za Waislamu na wanaotoa kauli hizo za jeuri ndio wasio itakia kheri nchi yetu. Ila kwa upande wake na wengine wanaokuja na kusema hadharani ndio waitakiao mema nchi. Aliwaomba viongozi wa serikali na hasa Mawaziri kumsaidia Mh. Rais Mkapa kutekeleza dhamira na ahadi yake ya kuyashughulikia malalamiko ya Waislamu. Mh. Kitwana Kondo alipata fursa ya kuyasema yote hayo katika kipindi
cha kujadili hotuba ya Mh. Rais Mkapa aliyoitoa Bungeni mwaka jana.
|
YALIYOMO
Tahari
Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe - Manyema Maoni yetu
DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA Uislamu na Mazingira katika
Umoja wa Mataifa
Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika
Internet
Rais Mkapa atekeleze hadi yake
kwa hadhari
Mashirika ya Dini yaelekeze
misaada vijijini
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma Ni serikali ipi anayoiwakilisha
Sumaye
Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|