|
|
| Fatwa
Masheikh kususia mazishi
Ndugu Mhariri NAPENDA kuchukua fursa hii katika gazeti lako ili niweze kumsaidia ndugu yangu Muislamu ambaye alitoa maoni yake kuhusu habari iliyoandikwa katika gazeti hili toleo nambari 181 iliyokuwa na kichwa cha habari "Maiti ya Muislamu yasusiwa". Ndugu huyu aliomba Masheikh watoe Fatwa kuhusu kususia mazishi. Katika barua yake ambayo imechapishwa katika gazeti hili toleo nambari 183 iliyokuwa na kichwa cha habari "kususia mazishi Masheikh tupeni Fatwa". Naomba nimsaidie kwa kurejea aya ifuatayo katika Qur’an (9:84) "Wala usimswalie kamwe mmoja wao yeyote yule akifa wala usisimame kaburini kwake (kumuombea dua). Hakika hao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakafa na hali ni wenye kuvunja amri za (Mwenyezi Mungu)". Habari zilizotolewa kwenye gazeti hili ni kwamba maiti ya Muislamu huyo ilisusiwa kwa kuwa alikuwa tarkuswalat. Kwa hiyo moja kwa moja inaonyesha kuwa alikuwa anakwenda kinyume na maamrisho ya Allah (s.w.) na mwenendo (mafundisho) ya Mtume (s.a.w.). Maana yake ni kwamba hakuwa anatekeleza lengo la kuumbwa kwake ambalo ni kumuabudu Allah (s.w.). Kutokana na aya hiyo hapo juu namuomba ndugu yangu atoe shaka na hofu kwa kitendo cha Masheikh kususia mazishi ya Waislamu ambao wanakwenda kinyume na maamrisho ya Allah (s.w.) na mwenendo wa Mtume (s.a.w.). Insha-Allah. Sharifa Yusuf,
Ndugu Mhariri KWA mara yangu ya kwanza napenda kuwapongeza Waislamu wa Makole kata ya kwa Fungo tarafa ya Mbwembwera wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga wakiongozwa na Sheikh Yahya Mohammed Kiduo. Kwa kuwa na msimamo wa kweli mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.) na hivyo ndivyo Waislamu wa ulimwengu tunatakiwa tufuate. Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.) pia ni kauli ya Mtume Muhammad (s.a.w.). Nawaoma Masheikh wote na Waislamu tufuate amri zote za Mwenyezi Mungu (s.w.) na Mtume wake. Cha kushangaza amri hii inafumbiwa macho nawaomba Masheikh watukumbushe Waislamu wote kupitia ANNUUR pia kupitia katika radio kuhusu msimamo huu wa kutozika wala kuswalia maiti ya namna hiyo kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume (s.a.w.). Tunawaomba waweke wazi jambo hilo ili lifuatwe na wacha Mungu wote Insha-Allah. Pia namuomba Sheikh ambaye alikuwa akitufunza Dawa za miti ajitahidi kutoa mafunzo kila makala ili tupate faida. Ninamuomba arudie somo la dawa ya Mkomamanga na aendelee na miti mingine pamoja na dawa zote. Mfano Zamda n.k. naomba anuani yake ili tuweze kumtumia barua. Mola wetu twakuomba tuzidishie elimu na utuzidishie ufahamu. Awadh Salim,
Ndugu Mhariri ALHAMDULILLAH tumemaliza Ramadhani yetu katika kuisherehekea hatuna budi kupongeza wale wote waliofanya maandalizi ya Baraza la Idd ambayo imetufanya kusisimkwa na kujengwa hisia mpya za kuingia mwaka mpya wa Kiislamu. Hivyo basi, Waislamu popote tulipo tafadhali tuingie katika harakati za kudai ukombozi. Tudai mashule ya msingi yote yaliyotaifishwa ili tuweze kuendeleza kizazi kipya kwa misingi ya dini kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu. Kama Wakristo wameweza kurudishiwa shule zao za misheni kwa nini sisi kuwepo kigugumizi cha kurudishiwa? Tunatoa pongezi kwa IPC kutuandalia muhtasari wa kufundishia na hivyo kutuwezesha kuujua Uislamu wetu vilivyo dhidi ya makafiri. Wakati huo tuwe katika maandalizi ya kufanya kumbukumbu za mashujaa wetu waliokufa shahidi Mwembechai. Mswadiku,
|
YALIYOMO
Tahari
Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe - Manyema Maoni yetu
DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA Uislamu na Mazingira katika
Umoja wa Mataifa
Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika
Internet
Rais Mkapa atekeleze hadi yake
kwa hadhari
Mashirika ya Dini yaelekeze
misaada vijijini
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma Ni serikali ipi anayoiwakilisha
Sumaye
Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|