AN-NUUR 
Na.187 Shawwal 1419, Februari 5 - 11 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Dondoo za KISAIKOLOJIA:
 
PEDOPHILIA
 

KATIKA mfululizo wetu wa kuyaangalia maradhi ya kisaikolojia, leo tuyaangalie maradhi yaitwayo Pedophilia . Maradhi haya ni ya mtu mzima (hususan aliyepea kiumri, yaani mtu wa makamo au mzee) kupenda mahusiano ya kijinsia na watoto wadogo, hususan wale ambao hawajafikia balegh. Tafsiri hii ni ya kawaida iliyozoeleka lakini kwa undani zaidi, Pedophilia ni maradhi aliyonayo mtu yeyote ambaye ni balegh, anayependelea mahusiano na mtu wa jinsia nyingine ambaye hajafikia balegh. 

Wagonjwa wa maradhi haya mara nyingi wanakuwa wanaume, ingawaje wapo wanawake ambao hujihusisha na kuwaghilibu watoto katika masuala ya maasi ya zinaa. 

Katika jamii yetu, maradhi haya yameenea kwani ni mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia au kusikia na kusoma habari kwamba mtoto mdogo, na wakati mwingine hata mtoto mchanga amenajisiwa. 

Nini chimbuko la maradhi haya au tuseme maovu haya? 

Jamii yetu hivi sasa imekumbwa na wimbi la wale wanaodhani mwanadamu yupo hapa duniani ili ale vizuri zaidi, anywe kwa israf, alale pazuri na avae vizuri zaidi. Ufupi wa maneno apate kustarehe. 

Dhana hii huendana na dhana nyingine ya kukimbia majukumu. Ndio maana leo watu wanahamasishwa wasizae maana wakiwa na watoto watabeba jukumu la kulea na hiyo kupunguza starehe zao. 

Dhana hizi zikishajengwa na kustawi katika fikra za watu, mambo makubwa mawili ni matokeo ya lazima. Kwanza ubinafsi na hali ya kutowajali wengine hustawi. 

Kwa hiyo hakuna atakayejali njaa ya mwingine wala janga jingine katika maisha. Na tunashuhudia leo katika jamii yetu wagonjwa wanavyotekelekezwa katika mahospitali kwa vile hawana fedha. Wenye madaraka serikalini wanavyotumia kodi za wananchi, wanatembelea magari ya fahari , kula na kusaza wakati wenyewe wananchi hawana madawa wala maji safi ya kunywa. 

Jambo la pili ni kiu isiyokatika wala isiyo na mipaka ya kutosheleza matamanio ya nafsi (kustarehe). Kila mtu hujiundia namnayake ya kustarehe. 

Wengine wataendekeza ngono ya jinsia moja, wengine watataka waparamie hata wanyama na wengine wataona starehe yao ipo katika kuwabaka watoto wadogo. 

Kwa mtu mzima kupenda kuwa na mahusiano ya kingono na watoto wadogo (Pedophilia) ni matokeo ya dhana nzima ya maisha inayopandikiza hisia kwamba lengo la maisha ni kustarehe. 

Watu wanahamanika leo kutaka kudhibiti wabakaji wa watoto wadogo na matatizo mengine kama matumizi ya madawa ya kulevya. Kosa halianzuii hapo. Hayo ni matokeo ya falsafa inayoongoza maisha katika jamii. 

Uislamu hautazami tatizo la ubakaji na tabia ya watu wazima kupenda mahusiano ya kingono na watoto wadogo kama tatizo au maradhi yenye kujitegemea. Wala si maradhi yanayoweza kuhusishwa na elimu nafsi bali ni matokeo ya lazima ya mifumo mibovu ya maisha. 

Dawa ya maradhi hayo ni kurejea kwenye mfumo sahihi wa maisha. Mfumo usio mtizama mwanadamu kama mnyama aliyeko hapa kwa ajili ya kustarehe, bali Khalifa wa Allah (s.w.) kwa ajili ya kumwabudu Muumba wake. 

Mtu aliyelelewa katika jamii ya Makhalifa wa Allah (s.w.) kula kwake, kunywa kwake na mengine yote atakayoyafanya yatatizama lengo kuu, sio kustarehe. 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Mauaji ya Mwembechai; Mh. Rais apewe kanda

Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri

Hijab ivaliwe shuleni

Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais

Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe  -   Manyema

Maoni yetu
Kauli ya Waziri Mkuu Bungeni: Tumsikilize nani?

DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA

Mjue Usama bin Ladin -3

Uislamu na Mazingira katika Umoja wa Mataifa
Na Dk.  Wahid

Barua ya wazi kwa Rais Mkapa

Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika Internet
Na. Zituzzaman Hoque

Kutoka magazeti ya zamzni

Rais Mkapa atekeleze hadi yake kwa hadhari
J.R. Msuya, Moshi

Mashirika ya Dini yaelekeze misaada vijijini
Na KAWELE  SAIDI 

Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma

Ni serikali ipi anayoiwakilisha Sumaye
Na Abu Salim

Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni

Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Na SALUM ALI 

Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro

Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel

Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina

Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti

Sayansi na Teknolojia 
[Jifunze ‘Kubana’ Majalada] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Chakula na Lishe 
[Ni hatari kuwaambia wananchi wasichague chakula] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita