AN-NUUR 
Na.187 Shawwal 1419, Februari 5 - 11 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mjue Usama bin Ladin -3
 

Katika sehemu ya pili, wiki iliyopita, tulichapisha mahojiano ya Bw. Usaama bin Ladin yaliyochapishwa katika gazeti la Nida’ul Islam, Toleo la 15, Oktoba - Novemba 1996 (http://www.islam.org.au). Katika mahojiano hayo, Bin Ladin aliishutmu vikali serikali ya Saud Arabia kwa kung’ang’ania madaraka, kuwabana wanazuoni waadilifu na pia wananchi kwa ujumla. Aidha mwanaharakati huyu alizichambua siasa za Saudia kuhusiana na ulimwengu wa Kiislamu. 

Leo, alhamdulillah, tunaendelea na sehemu ya tatu ya mahojiano hayo ambapo Bw. Usama anaubainisha ubabe wa Marekani dhidi ya Waislamu na, kisha, anatoa wito kwa Waislamu ulimwenguni kote kuukumbuka wajibu wao wa kidini unaowataka kuunganisha nguvu zao kumkabili dhalimu huyu, Marekani.  

Mwisho wa mahojiano tumetoa mambo matano ambayo tumeyapata (yatokanayo) katika mahojiano haya na tunadhani ni vizuri Waislamu tukayatia katika nyoyo zetu. 

Sasa endelea ... 

[Unafikiri] ni nini wajibu wa Waislamu ulimwenguni kote kuhusiana na hizi kampeni za kimataifa kuupiga vita Uislamu? 

Jambo ambalo halina shaka katika hizi kampeni za pamoja kati ya Wayahudi na Wakristo dhidi ya Waislamu ulimengini kote, kampeni ambazo mfano wake haujawahi kupatikana, ni kwamba lazima Waislamu kukusanya nguvu zote ili kumshinda adui kijeshi, kiuchumi, kiitikadi na pia katika nyanja zingine zote. 

Ni muhimu kwa [Waislamu ulimwenguni kote] kuwa ni wenye subira na kushirikaina katika mambo mema na ucha-Mungu na [pia] kuongeza kuujua zaidi ukweli kuwa kilicho muhimu zaidi baada ya sisi kuamini ni kumg’oa adui ambaye anaivuruga dini na ulimwengu kwa ujumla. 

Ni muhimu kuepuka kugombana wenyewe kwa wenyewe katika mambo yasiyo ya msingi ili tuunganishe juhudi zetu tupate kuung’oa ukafiri uliokithiri. 

Ni lazima wayaweke maneno haya ya Allah, Aliye Mtukufu, katika vitendo: "hakika huu umma wako ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wako, hivyo niabudu Mimi", na wala wasiwe kama wale ambao Allah amewelezea kwa maneno Yake haya: "hakika wale walioigawanya dini yao na kuwa vikundi vikundi, wewe si katika wao". 

Ipo haja ya kujitolea na wala sio kuzozana katika mambo madogo madogo, na [wala] Muislamu asiyabeze matendo mema [ ya mwenzie] kwa namna yoyote ile. Mtume (s.a.w.) alisema: "Yeyote anayemwamini Allah na Siku ya Mwisho basi aseme maneno mazuri au akae kimya". Pia wazingatie maneno ya Mtume (s.a.w.), "wafahamisheni [wenzenu] wala msiyaharibu [mema waliyoyafanya] wafanyieni wepesi wala msiwafanyie ugumu". 

Tunamuomba Allah kuujalia umma huu uongofu, kuwainua daraja watu wenye kumtii Yeye[s.w.t.] na kuwadhalilisha wale wote wenye kumuasi, na atupe utawala ambamo wema unaarishwa na uovu unazuiliwa. Ee Mola mpe Rehma Zako Muhammad, [ambaye ni] mja Wako na Mjumbe Wako, na familia yake, na masahaba zake na uwape amani .... Shukurani zote zinamstahiki Allah, Mola wa ulimwengu. 

Yatokanayo 

1. Tawala nyingi zipo madarakani si kwa maslahi ya wananchi, bali kwa maslahi ya watawala. 

2. Utakapokuta katika nchi fulani ambapo utawala wake si kwa mujibu wa sheria za Allah lakini utawala huo ukawa na mahusiano mazuri na viongozi wa kidini, basi uwezekano ni kuwa viongozi hao wa kidini hawatendi kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu. 

3. Katika jamii ni muhmu liwepo kundi, hususani la wanazuoni, japo wachache,ambalo litakuwa likifanya tathmini ya mwenendo wa serikali na mamlaka za kidini zilizoidhinishwa na serikali. Kundi hili litazikosoa mamlaka hizo mbili na kisha kuonesha Njia Sahihi ingawa litapata misukosuko ndani na nje ya nchi hiyo. 

4. Adui anayetukabili Waislamu amepania kwelikweli. Kumshinda adui huyu tunahitaji juhudi za pamoja na kufuata Qur’an na Sunnah. Leo hii hapa Tanzania Waislamu tumegawanyika makundi makundi; mbaya zaidi ni kuwa Waislamu wa kundi moja wanakuwa ni vipenzi zaidi wa makafiri kundi la Waislamu wenzi wao! 

5. Mwenyezi Mungu aliyetuamrisha kufunga saumu ya Ramadhani ndiye huyo huyo ametuarisha kupigana kwa ajili Yake kuondoa dhuluma na pia kulipiza kisasi. Yote haya yamo ndani ya Qur’an na hatuna budi kutii ikiwa sisi ni wenye kuamini. 

Allah ndiye Mjuzi zaidi 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Mauaji ya Mwembechai; Mh. Rais apewe kanda

Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri

Hijab ivaliwe shuleni

Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais

Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe  -   Manyema

Maoni yetu
Kauli ya Waziri Mkuu Bungeni: Tumsikilize nani?

DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA

Mjue Usama bin Ladin -3

Uislamu na Mazingira katika Umoja wa Mataifa
Na Dk.  Wahid

Barua ya wazi kwa Rais Mkapa

Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika Internet
Na. Zituzzaman Hoque

Kutoka magazeti ya zamzni

Rais Mkapa atekeleze hadi yake kwa hadhari
J.R. Msuya, Moshi

Mashirika ya Dini yaelekeze misaada vijijini
Na KAWELE  SAIDI 

Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma

Ni serikali ipi anayoiwakilisha Sumaye
Na Abu Salim

Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni

Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Na SALUM ALI 

Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro

Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel

Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina

Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti

Sayansi na Teknolojia 
[Jifunze ‘Kubana’ Majalada] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Chakula na Lishe 
[Ni hatari kuwaambia wananchi wasichague chakula] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita