|
|
|
Upinzani dhidi ya Serikali
ya Kiislamu wakati wa Khalifa wa Tatu Uthman bin Affan
Pamoja na barua watu waliajiriwa kuendeleza madai dhidi ya Serikali na Khalifa. Hapo awali tulieleza kuwa wapo watu waliojiunga na ghasia za Saba kwa sababu zao binafsi. ammar bin Yasir, Muhammad bin Abi Hudhaifah na Muhammad bin abi Bakr, Muhammad bin abi Hudhaifa alilelewa tangu udogo na Uthman kwa kuwa alikuwa yatima. Alitegemea apate nafasi kubwa katika serikali alipoona hapati akaenda Misri kujiunga na wahaini. Ni hivyo hivyo kwa mtoto wa Abu bakr. Alikuwa na kesi ya kudaiwa. Khalifa Uthman alihukumu kwa haki dhidi ya Muhammad bin Abu Bakr. Muhammad akaona kaonewa akaenda Misri kujiunga na Saba. Ammar alikuwa miongoni mwa maswahaba wanne waliotumwa kusikiliza malalamiko mikoani. alipofika Misri alishawishiwa na akakubali kujiunga na wanafiki wa kundi la Sabaa. Abu Sarah Gavana wa Misri alimfahamisha Khalifa kushiriki kwa Maswahaba hawa katika ghasia za Sabaa na kushauri wachukuliwe hatua. Lakini Khalifa alikataza kuwachukulia hatua yoyote. Kufa kulizuka upinzani wa wazi wakati wafuasi wa Sabaa walipotaka kuondolewa kwa amri ya Khalifa wa pili Umar aliyezuia kuondolewa kwa Dhimmis katika Ardhi yao lakini iliyotekwa. amri hii ilipokataliwa na Khalifa upinzani ukaongezeka. Kwa mbinu zote hizi za wapinzani, wasi wasi ukaenea nchi nzima na Serikali sasa ikalazimika kuchukua hatua, ili kudhibiti hali ya nchi. Hatua ya Serikali dhidi ya waanzilishi wa fitna na farka Hatua ya kwanza ilikuwa kuwahamishia Syria viongozi 10 wa upinzani kutoka Kufa. Viongozi hawa walikuwa Malik al-Ushtur Zeib Ibn Suhan, Jundub, Urwa na Thabit Ibn Qays. 85 Wakorofi hawa walipopelekwa Syria, Amir Muawiya alizungumza nao na kusikiliza mafundisho yao lakini alipowasihi waache kupoteza watu walijifanya hawamuelewi kwa sababu hii Gavana Muawiya alimuandikia Khalifa Uthman kumuomba awarudishe walikotoka ili wasiwaharibu watu wa Syria kwa vile wanazungumza lugha ya shetani na lengo lao ni kuwagawa watu na kuunda fitna. Watu hawa walirudishwa Kufa, walipoendelea na shughuli zao walihamishiwa Hirus ambako walidhibitiwa kwa muda na gavana Abdur-Rahman mtoto wa Khalid. Hatua ya pili iliyochukuliwa na khalifa pamoja na Shura yake ni kutuma wajumbe 4 kutembelea Dola nzima na kusikiliza malalamiko ya wananchi Maswahaba waliotumwa ni Muhammad bin Muslimah, Usamah bin Zaid, ammar bin Yasir na Abdullah bin Umar.86 Wajumbe hawa ambao walirudi watatu walitoa taarifa kuwa hakukua na malalamiko. Kuwasilisha malalamiko kwenye kikao cha magavana wote Kama kawaida magavana hukutana kila mwaka. katika mwaka ule taarifa zilitolewa kuwa wenye malalamiko waende kuwasili ya malalamiko yako kwenye kikao hicho. Lakini hakuna aliyejitokeza. Si hivyo tu lakini Khalifa uthman alitimiza dai la wapinzani hawa kwa kumuweka Gavana wanaemtaka kufa. Walichokifanya wapinzani ni kuwa walikusanya kundi la watu wapatao elfu moja na kumzuia gavana wa kufa asirudi madarakani alipokwenda Madina mkutanoni walimzuia mahali paitwapo Ajara, mtumishi wake aliuliwa na yeye akarudi Madina. Khalifa akamthibitisha Abu Mussa kuwa gavana wa Kufa baada ya kutakiwa na wapinzani. Hapa Khalifa alionyesha udhaifu, watu hawa walistahili kuadhibiwa kinyume na kukubali dai lao baada ya uhaini uliowazi hatua kali wote waliohusika na uchochezi uliokuwa unaendelea chini katika kikao cha magavana Khalifa alitaka ushauri wa kuzima uasi chini. Saad alishauri wapinzani wakamatwe na kuadhibiwa. Abu Sarh alishauri wasipewe posho; Ibn Aamir alitaka wapinzani wauawe kwa kuanza kampeni mpya dhidi ya wapinzani, Muawiya pia alitaka zichukuliwe hatua kali. Kutokana na maoni haya Khalifa alijibu: Ukatili sitoruhusu, kama mapinduzi yakija sitaki kulaumiwa. Ukianza hivi mwisho wake mbaya. Ingekuwa vyema pale mapema wakati uasi haujaenea. Sasa hakuna la kufanya ila kukaa kimya na kusubiri bila kumkosea mtu yeyote. Muawiya alipokuwa anaondoka Madina alimsihi Khalifa akubali kuhama Madina lakini alikataa, na kusema hata kama ni kuokoa maisha yangu sitaondoka katika ardhi ambayo Mtume aliishi na kuzikwa. 87 Kisha muawiya akamuomba akubali kuletewa jeshi lilinde mji wa Madina. Hali kadhalika Khalifa alikataa na kusema; "Sitawaweka askari wanaokaa karibu na nyumba ya Mtume". Kwa hali hiyo Muawiya akajibu "Sioni kinachokusubiri ila umauti; Mwenyezi Mungu ndie mlinzi wangu alisema Khalifa Uthman.88 ambaye alikuwa mkongwe wa miaka 82. Babu Uthman bin Affan, alijua hatari iliyokuwa inamkabili lakini hakutaka kutumia nguvu kuwadhibu wapinzani wake kwa kuhofia kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe, alihiyari afe yeye kuliko kuzusha vita vingegharimu roho nyingi. Kufa shahidi kwa Khalifa Uthman Ni dhahiri wahaini wa Serikali waliona wakati umefika tangu pale walipoweza kumtoa Gavana wa kufa na kumuweka wanamtaka bila kuadhibiwa. Wakaibua mbinu ya kutuma watu watatu kwenda Madina kuwasilisha malalamiko yao, watatu hao walitoka Misri, Basra na Kufa. Walipofika Madina baadhi ya maswahaba walimshauri Khalifa kuwa wauwawe lakini kwa msimamo ule ule wa kutomwaga damu ya Waislamu, Khalifa alikataa na kusema nitawasikiza. Khalifa aliwasikiliza kisha akatoa hutuba ndefu ambayo ndani yake alijibu tuhuma zote. Baadhi ya sehemu ya hutuba hiyo ya kihistoria ni kama ifuatavyo: Ninalaumiwa kwa kuwapenda ndugu zangu. Sio dhambi kwa mtu kumpenda ndugu yake. lakini sijamfanyia mtu udhalimu kwa sababu ya kupenda ndugu. Sijatumia chochote kwa ajili ya ndugu zangu kutoka kwenye mfuko wa serikali... Imesemwa kuwa nimewateua vijana wadogo maafisa. nimefanya hivyo kwa kuzingatia mchango katika uislamu. hakuna anaekanusha uaminifu wao na mchango wao katika Uislamu, na Waislamu. Kuteuliwa kwa Usmaha na Mtume (s.a.w.) kuwa kamanda wa jeshi. |
YALIYOMO
Tahari
Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe - Manyema Maoni yetu
DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA Uislamu na Mazingira katika
Umoja wa Mataifa
Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika
Internet
Rais Mkapa atekeleze hadi yake
kwa hadhari
Mashirika ya Dini yaelekeze
misaada vijijini
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma Ni serikali ipi anayoiwakilisha
Sumaye
Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|