AN-NUUR 
Na.187 Shawwal 1419, Februari 5 - 11 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Zanzibar ni nchi au mkoa?.
 

ZANZIBAR imeundwa kwa visiwa viwili ambavyo ni Unguja na Pemba. Nchi ya Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili tofauti ambazo ni Tanganyika na Zanzibar, ambapo Zanzi bar ina mikoa mitano na Tanganyika ina mikoa ishirini, kwa pamoja inafanya Tanzania kuwa na jumla ya mikoa ishirini na tano. Salum Ali wa Zanzibar anaelezea zaidi. 

Dhana ya kujiuliza endapo Zanzibar ni nchi au mkoa ndani ya Tanganyika inakuja baada ya kufuatilia mambo kadhaa ya msingi ya kiutendaji katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Uwezo wa Zanzibar kama nchi unaelekea kuondoka kabisa baada ya kubanwa kiuchumi na serikali ya Muungano. Sisi kama Wazanzibari tunapaswa kujiuliza huu Muungano wetu ni muungano gani wa kiuchumi kati ya "The Free Trade Area" au "The Customs Union" au "The Common Market" au "The Economic Union? Mifano hii ya miungano ya kiuchumi haina ubaguzi wakati baina ya nchi husika na "terms" zake za mikataba zipo wazi kwa pande zote mbili na inafaidisha pande zote husika bila pande moja kuona na kuhisi inabaguliwa. 

Inawezekana kabisa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ni muungano wa pumbazo la kisiasa la kuharibu na kunyonya upande mmoja ambao ni Zanzibar. Maana Zanzibar haina tofauti sana na mikao ya Pwani, Tabora, Mtwara, Lindi, Kigoma na Tanga n.k. Kwa sababu mikoa hii huishi Waislamu wengi angalau kama Zanzibar. 

Wazanzibari hatuna budi kuhisi hivyo kwa jinsi tunavyotendewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar ni nchi yenye asilimia 99% ya Waislamu kati ya wananchi wote wa Zanzibar. Cha kushangaza serikali ya Jamhuri ya Muungano imeizuia Zanzibar kujiunga na umoja wa nchi za Kiislamu (OIC) kwa sababu zisizoeleweka. Kinyume chake Wakristo wa Tanzania hupata misaada mbalimbali kutoka kwenye nchi za Kikristo kwa manufaa ya Wakristo. Kwa mfano sasa hivi vyuo vikuu vingi vimejengwa vya Kikristo kwa misaada kutoka nje, Je, Waislamu sisi hatma yetu nini baadaye? Hali hii inaonyesha upendeleo wa kidini ndio ulio tawala katika serikali ya Jamhuri ya Muungano. 

Zanzibar inashindwa kutetea nguvu za umeme wa kutumia taka kutoka Malaysia ambao ilitarajiwa kuwekeza hapa Zanzibar. Hii ni kutokana na serikali ya Jamhuri ya Muungano kutounga mkono na shinikizo toka nje. Zanzibar tunategemea umeme kutoka bara, hii ni kutufanya tuwe tegemezi katika nyanja muhimu ili tutawaliwe kisiasa na kiuchumi na ndivyo ilivyo. Sababu mojawapo ya kuzuia uwekezaji ule wa umeme wa taka ni kwmba eti TANESCO itakosa mapato kutoka Zanzibar. 

Hii ni sababu dhaifu sana na ni ya kidini kwa sababu zipo Missions za Kikristo kama vile Peramiho - Songea, Nambele - Songea n.k. zina umeme wa kutumia maji kwa ajili ya matumizi yao binafsi na vijiji vya jirani mbona serikali ya Jamhuri ya Muungano haisemi kama TANESCO itakosa mapato kwa Missions hizo kuwa na umeme wao? Huko kukosa mapato kupo Zanzibar tu? Kama siyo udini ni nini? Tuelezwe. 

Zanzibar tunataka kuanzisha kampuni ya simu (ZANTEL) ambayo itatoa huduma Zanzibar bado nayo tunatiliwa ngumu eti TTCL itakosa mapato. TTCL itakosa mapato kwa Zanzibar tu kuanzisha kampuni yake ya simu? Mbona kuanzishwa kwa TRITEL na MOBITEL haiwi kukosesha mapato TTCL ila Zantel itakosesha mapato. Hii inaonyesha jinsi gani Zanzibar inavyokabwa katika kujiendeleza. Suala lolote linaloonekana ni mali na manufaa kwa Zanzibar halikubaliki, kwa nini? 

Hii ni jitihada ile ile ya kudhoofisha kiuchumi maeneo yenye Waislamu wengi Tanzania kama vile Mtwara, Lindi, Kigoma, Pwani na Tanga n.k. 

Kama kweli Tanzania ni muungano wa nchi mbili zenye Marais yaani Zanzibar na Tanganyika, mbona mgawanyo wa taasisi na vyuo vya elimu haupo sawa? Tanzania bara kwa mfano kuna vyuo vya biashara kama vile College of Business Education (CBE), DSA, Vyuo vya Ufundi, SIDO n.k. ambavyo vimetapakaa karibu mikoa yote ya bara na hakuna hata kimoja Zanzibar. Sisi kama Watanzania Wazanzibari tuelewe vipi, ikiwa tuna haki ya kupatiwa na sisi ujenzi wa vyuo hivyo Zanzibar? 

Sasa hivi tuna msuguano mwingine wa Zanzibar kuwa "Free Port" bado tunatiliwa ngumu na serikali ya Jamhuri eti serikali itakosa mapato, mapato gani hayo? Kama kweli Muungano wetu ni wa kheri kwanini tuvutane au tuwekeane ngumu kwa kuona wivu kuwa Zanzibar itanufaika. 

Mlioliona kwa serikali ya Jamhuri kukosa mapato ni kwa Zanzibar kuwa "Free Port" tu? Vipi ndege za Kikristo zinaingia na kutoka Tanzania kwenye viwanja vyao bila kupekuliwa hamuoni kama serikali inakosa mapato? Mali inayoingizwa au kutolewa kwenye "Air Strips" za Wakristo kusiko na polisi wala Afisa "Custom" kwa ndege za Kikristo mnazijua? Ila Zanzibar tu kuwa "Free Port" huu ni udini ulio dhahiri. 

Ili kujinasua na hali hii serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wazanzibari wote kwa ujumla bila kujali tofauti za kisiasa tushikamane ili tuweze kujitegemea katika njia zote kuu za uchumi na ulinzi. La sivyo, tukubali Zanzibari kuwa mkoa na siyo nchi yenye Rais. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Mauaji ya Mwembechai; Mh. Rais apewe kanda

Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri

Hijab ivaliwe shuleni

Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais

Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe  -   Manyema

Maoni yetu
Kauli ya Waziri Mkuu Bungeni: Tumsikilize nani?

DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA

Mjue Usama bin Ladin -3

Uislamu na Mazingira katika Umoja wa Mataifa
Na Dk.  Wahid

Barua ya wazi kwa Rais Mkapa

Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika Internet
Na. Zituzzaman Hoque

Kutoka magazeti ya zamzni

Rais Mkapa atekeleze hadi yake kwa hadhari
J.R. Msuya, Moshi

Mashirika ya Dini yaelekeze misaada vijijini
Na KAWELE  SAIDI 

Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma

Ni serikali ipi anayoiwakilisha Sumaye
Na Abu Salim

Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni

Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Na SALUM ALI 

Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro

Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel

Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina

Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti

Sayansi na Teknolojia 
[Jifunze ‘Kubana’ Majalada] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Chakula na Lishe 
[Ni hatari kuwaambia wananchi wasichague chakula] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita