AN-NUUR 
Na.187 Shawwal 1419, Februari 5 - 11 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika Internet 
 
Na. Zituzzaman Hoque
 

Barua adimu zenye chapa (seal) ya Mtume Muhammad (s.a.w.) hivi karibuni zitaanza kuonekana, Insha’Allah, katika mtandao wa kompyuta ulimwenguni, Internet, gazeti la serikali nchini Misri, Al-Akhbar, lilitangaza. Barua hizo ambazo zilipatikana kutoka katika jumba la makumbusho la Topkapi huko Instanbul [Uturuki] zilikuwa zimetumwa kwa watawala wa Uhabeshi (Ethiopia), Persia (Iraq) na Misri. Mtume (s.a.w.) alipeleka barua nyingi kwa wafalme walioishi katika ukanda unaozunguka Peninsula ya Uarabuni akiwataka watawala hao kusilimu, alisema Mkurugenzi wa mradi huo, Hamed Abdur-Rahim. Mradi huo uliotayarishwa na Kituo cha Urithi wa Kisayansi cha Chuo Kikuu cha Cairo, umekusudiwa kuthibitisha kuwa Uislamu ulianza ukiwa ni dini imara na utaendelea kuwa imara. 

Barua hizi si tu kwamba ni vitu vya kihistoria. [bali] zilikuwa ni sehemu muhimu katika mpango wa Mtume (s.a.w) kuieneza dini. Allah (s.w.t.) alisema: 

Na tumekupeleka wewe kama mletaji wa biashara njema na muonyaji kwa watu wote. (Qur’an 34:28) 

Hii ilimaanisha kuwa Uislamu (kama mfumo wa maisha ya jamii) ndio unaostahiki kuwa kigezo kwa wanaadamu wote. Hivyo sera (siasa) za Dola ya Kiislamu kuhusiana na masuala ya nchi za nje ni kuyafanya mataifa yote yafuate amri za Allah (s.w.t.). Na kwa sababu hiyo, Mtume (s.a.w.) aliwatuma mabalozi wakiwa na barua hizi, kwenda kwa watawala wa mataifa makubwa wakati huo. Mataifa hayo ni pamoja na taifa lililokuwa kubwa katika kanda ya Uarabuni mfano Yemen, na pia mataifa makubwa ulimwenguni kwa wakati ule, Warumi na Wapersia (Wairaq). 

Kwa kweli Uislamu ulianza ukiwa imara. Sera hii ya masuala ya nchi za nje ilileta mafaniko makubwa muda wote ambao ilitekelezwa na viongozi wa Dola ya Kiislamu walioshika madaraka baada ya Mtume (s.a.w.). Watu waliingia Uislamu makundi kwa makundi. Wengi walislimu na walikubali kuishi chini ya utawala wa dola ya Kiislamu. Wengine hawakusilimu lakini waliishi katika Dola hiyo na walilindwa (ahl udh-dhimmah). Wale walioyakanusha wazi wazi maamrisho ya Allah (s.w.t.) walijikuta wakipigana vita na Waislamu, vita ambayo hatimaye iliwaacha [makafiri hao] chini ya utawala wa Dola ya Kiislamu. Kwa njia hii Uhabeshi, Persia na Misri zikawa sehemu ya dola ya Kiislamu. Mataifa hayo yaliunganishwa katika Dola ya Kiislamu mpaka ikawa hakuna dalili kuwa mataifa hayo yalikuwa tofauti. Hakika, Uislamu ulianza ukiwa imara na ulindelea kuwa imara. 

Leo hii kilichobaki kama ushahidi wa sera hiyo ya dola ya Kiislamu juu ya masuala ya nchi za nje ni hizi barua na umma huu wa Waislamu. 

Hakuna utawala wa Kiislamu. Nafasi yake imechukuliwa na serikali za ki-secular (zisizofuata maamrisho ya Allah bali matashi ya mwanadamu) kama zilivyo serikali za Misri na Iran. Matokeo yake ni kuwa hivi sasa hakuna kabisa sera hiyo ambayo Mtume wa Allah (s.a.w.) aliileta. Badala yake kumekuwepo na sera ambazo zinaufanya u-secular kuwa ndio kigezo kikuu cha mfumo wa maisha ya mwanadamu. Nchi zote leo hii ni wanachama wa Umoja wa Mataifa na kwa maana hiyo zimeitelekeza Jihad zikichelea kuwa kupanuka kwa tawala za Kiislamu kutaonekana kuwa ni kukiuka sheria za kimataifa. Badala ya [mataifa ya kiislamu] kutuma mabalozi [katika nchi zisizo za Kiislamu] ili kuwafikishia neno la Allah (s.w.t.) [wapate kusilimu] zinabaki kuwanyenyekea Clinton na wenzake na kuyafuata kwa unyenyekevu yale Clinton anayowaeleza. 

Hakika Uislamu ulianza imara na utaendelea kuwa imara. [Lakini] Ili hili liwezekane inahitajika kuwepo tena kwa utawala wa Kiislamu ili Uislamu upate kuenezwa ulimwenguini kote. Muhammad (s.a.w.) alisema, "Jihad ni jambo lenye kuendelea tangu kuteuliwa kwangu (kuwa Mtume) mpaka [mtu] wa mwisho katika umma wangu atakapombana na Dajjal". 

Khilafah Magazine 
Ramadhan, 1419 
Januari, 1999 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Mauaji ya Mwembechai; Mh. Rais apewe kanda

Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri

Hijab ivaliwe shuleni

Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais

Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe  -   Manyema

Maoni yetu
Kauli ya Waziri Mkuu Bungeni: Tumsikilize nani?

DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA

Mjue Usama bin Ladin -3

Uislamu na Mazingira katika Umoja wa Mataifa
Na Dk.  Wahid

Barua ya wazi kwa Rais Mkapa

Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika Internet
Na. Zituzzaman Hoque

Kutoka magazeti ya zamzni

Rais Mkapa atekeleze hadi yake kwa hadhari
J.R. Msuya, Moshi

Mashirika ya Dini yaelekeze misaada vijijini
Na KAWELE  SAIDI 

Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma

Ni serikali ipi anayoiwakilisha Sumaye
Na Abu Salim

Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni

Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Na SALUM ALI 

Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro

Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel

Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina

Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti

Sayansi na Teknolojia 
[Jifunze ‘Kubana’ Majalada] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Chakula na Lishe 
[Ni hatari kuwaambia wananchi wasichague chakula] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita