NASAHA
Na. 042 Jumatano Aprili 5 - 11, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Habari za Kimataifa

Maiti za Makomandoo wa Russia zapatikana 

MOSCOW -Russia ilipata hasara nyingine kijeshi wiki iliyopita katika mapambano yake na wapiganaji wa Chechnya katika Wilaya moja iliyoko milimani baada ya maiti zaidi ya 30 za makomandoo wake kupatikana kufuatia shambulizi la kustukiza walilofanyiwa. 

Na hili ni shambulio la pili kali katika kipindi cha mwezi mmoja na limezidi kudhihirisha taarifa za kwamba Russia imesambaratisha kabisa upinzani kuwa sio za kweli. 

Shambulio hili limefanywa katika kipindi ambacho Russia inachunguzwa na Umojawa Mataifa kufuatia tuhuma dhidi yake kwamba imefanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi raia wa Chechnya. Kamishna wa haki za binadmau wa Umoja wa Mataifa, Mary Robinsan alikuwepo Chechnya kwa kazi hiyo ambapo maafisa wa Russia wamemzuia kutembelea baadhi ya sehemu. Zaidi ya raia 200,000 wameikimbia Chechnya kutokana na wapigano. 

Ripoti zimewakariri maofisa wa ngazi za juu wa Russia wakisema kwamba maiti hizo zilipatikana karibu na kijiji cha Zhai-Vedeno, kusini mwa mji mkuu Grozny, ambapo msafara huo ulishambuliana wapiganaji wa Chechnya wiki iliyopita. 

Shirika la habari la Itar-Tasala Russia limesema kwamba maiti zilizopatikana zinafikia 32, likimkariri Viktor Medveditskovu, msaidiz iwa mkuu wa operesheni ya Chechnya katika Wizara Mambo ya Ndani ya Urusi. 

Operesheni yao ilikuwa ikikwamishwa na mabomu ya ardhini katika eneo hilo pamoja na hali mbaya ya hewa. 

Interfax, ikiwakariri wasemaji wa kijeshi, ilisema kuwa maiti 19 kati ya 32 tayari zilishachukuliwa kwa ajili ya utambulisho. Mtu mmoja aliyejeruhiwa pia alipatikana siku tatu baada ya kipigo hicho. 

Waziri wa Mambo ya ndani Vladmir Rushailo na Mkuu wa Majeshi Anatoly Kuashnin walikwenda hadi kwenye eneo hilo karibu na bonde Ijumaa ili kutathmini shambulio. Ripoti zilizotangulia zilisema kwamba waliokufa ni 6 na 30 hawajulikani walipo. 

Inaelezwa kuwa huenda wapiganaji wa Chechnya walitumia mbinu ya kushambulia gari la mwisho na la mwanzo na kisha kumimina makombora na mizinga katikati. 

Licha ya juhudi zake, Russia bado inapata hasara kubwa zaidi katika vita vya milimani. Makomando 20 waliuawa mwezi uliopita nje kidogo ya Grozny na kikosi kizima cha askari 84 kiliangamiza katika mapigano ya kusini. 

Hadi sasa hali ya vita milimani inawafanya Russia kushindwa kutumia vizuri ndege za vita, helikopta na makombora hivyo kulazimishwa kupigana kwa mbinu za msituni ambazo wapiganaji wa Chechnya ni wajuzi zaidi. 

Hata hivyo Vladmir Putin, Rais mpya wa Cehchnya ameapa kwamba hatajitoa Chechnya kama ilivyo kuwa katika vita kama hivyo kati ya mwaka 1994 na 96 ambapo Russia ilishindwa vibaya. 


Azim Premji wa tatu kwa utajiri duniani 

WASHINGTON - Muislamu raia wa India, Azim Hashim Premji, mwanzilishi wa kampuni ya Kompyuta ya Wipro, amekuwa tajiri mkubwa ulimwenguni katika nafasi ya tatu nyuma ya Bill Cartes wa Kampuni ya Kompyuta ya Microsoft (pauni bilioni 53.12) na Robson Walton (pauni bilioni 52.87) wa kampuni ya biashara ya Wal-Mart.

Ni ajabu kwani Waislamu wa India ambao ni asilimia 23 ya Wahindi wote na ambao hapo kabla waliongoza uchumi wa India, sasa wamewekwa katika daraja la chini kiuchumi, kisiasa, kielimu na kila njanja ya maisha. 

Utajiri wa Premji unakadiriwa kufikia pauni bilioni 35, na hivyo kufanya kuwa tajiri wa tatu ulimwenguni, kulingana na gazeti la Sunday Times katika makala ya "Richlist 2000", iliyochapishwa Jumapili iliyopita. 

Premji mwenye umri wa miaka 54, ni mhitimu wa Shahada ya Uhandisi toka Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani. Alirithi kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia baada ya kifo cha baba yake. Baba yake,ambaye alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa, ndiye mwanzilishi wa kampuni iliyoitwa 'Western Indian Vegetable Company' ambacho kilitengeneza mafuta ya kupikia. 

Mwaka 1947, M.A. Jinnah, mwanzilishi wa taifa la Pakistan, alijaribu kumshawishi baba yake Premji kuhamia Pakistan na kumwahidi nafasi ya uwaziri wa fedha lakini alikataa na kusema kwamba India ni nyumbani kwake. 

Mwaka 1977,wakati Shirika la kompyuta la IBM lilipojitoa India, Azim Premji aliibadili kampuni na kuipa jina jipya la Wipro na kuipanua zaidi hasa katika teknolojia ya kompyuta. 

Kinachompa faida zaidi ni biashara ya programu za kompyuta ambayo thamani ya hisa zake zimezidi kupanda hadi kumfikisha nafasi ya tatu katika orodha ya matajiri kabisa duniani. 

Waislamu wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni Sultan wa Brunei(mafuta, pauni bilion 18.75), nafasi ya 6 Mfalme 'Fahd wa Saudia na familia yake(pauni bilioni 17.5), nafasi ya 7 

Sheikh wa Abu Dhabi(mafuta, pauni bilioni 12.5), nafasi ya 9 Amir wa Kuwait(mafuta na mali nyingine, paundi 10.62), nafasi ya 12 Mwana Mfalme, Al-Waleed bin Talal bin Abdul Aziz al Saud (pauni billioni 9.37),na nafasi ya 15 Sheikh Makhtoum bin Reshid Al Makhtoum Falme za Kiarabu(pauni bilioni 7.5) 


Waislamu waandamana Toronto kupinga udhalimu wa Russia huko Chechnya



ZAIDI ya waandamanaji 2000 waliandamana katika mitaa yaToronto, Canada wiki iliyopita (Machi 25) ili kuikumbusha serikali yao juu ya madhila yanayowakumba raia wa Chechnya. Polisi walifunga mitaa miwi li ilikuwapa waandamanaji nafasi katika safari ya kilomita 1.5 Maandamano hayo yaliyoandaliwa na kikundi kiitwacho Toronto Chechnya task force ni makubwa zaidi tangu maandamano kama hayo yalipofanyika kuwaunga mkono wa-Bosnia mnamo miaka ya 90 ambapo washiriki walifikia 4000.

Waandamanaji walikuwa na matumaini ya kulazimisha watawala wa Canada kuikemea Russia ili iache mauaji ya raia. Kikundi cha Task force kinasema kwamba hatua yao inalingana na haki za kimsingi za binadamu. Maelfu wamesha uawa na zaidi ya 200,000 wameshakimbia makazi yao kutokana na mapigano ya hivi karibuni. Vikundi vya kutetea haki za binadamu cha Human Rights Watch, Council of Europe na Physicians for Human Right (Madaktari wanaopigania haki za binadamu) wamejaribu kutoa hadharani uhalifu wa kivita hukumu za mauaji ya hapo kwa hapo na ukiukwaji mwingine wa haki za kibinadamu unaofanywa na majeshi ya Russia. "Licha ya ripoti kutoka vikundi vinavyojitegemea vya haki za binadamu, jamii ya kimataifa ikiwemo Canada wamebaki kimya, alisema Anwaar Syed, Msemaji wa kikundi cha Task Force na Mkurugenzi mtendaji wa jumuiya ya Kiislamu kwa ajili ya haki za raia cha Canada (CMCLA). 

Polisi walifunga mitaa huku waandamanaji wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "Toronto inajali" na wakisema: "Vita vya Russia vinaua maskini, simamisheni mauaji, simamisheni chuki." Watoto walitoa mchango mkubwa katika maandamano haya wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "waokoen iwatoto wa Chechnya" na "Watoto wana haki pia. Ejaz Malik wa kikundi cha Task Force alisema kwamba kulingana na watu wanaoshuhudia huko Chechnya, maelfu ya watoto wameathiriwa na vita wakiwemo watoto 30,000 waliochwa mayatima hadi sasa." 

Wakati waandamanaji walipoingia viwanja vya Queen's Park, msemaji wa sherehe hizo Abdul Rahman Malik aliwasisitizia waandamaji kudumisha msimamo wao wa kujali hali ya Wachechnya waliopo maeneo ya vita. Naye mwandishi wa nyimbo anayejulikana kimataifa Dawud Warnshy- Ali, aliwambia umati wa maandamaji kwamba Canada ni nchi ya amani na lazima itoe kauli za kupinga uvamizi wa Chechnya. 

Kikundi cha Task Force na waandamaji waliitaka serikali kulilazimisha shirika la Fedha Duniani (IMF) kusimamisha mpango wao wa kuipa fedha Russia mpaka waache vitendo vyao vya kuishamnbulia Chechnya kijeshi. 

Kulazimisha Bara la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kuwalazimisha wa-Russia kuacha mara moja mashambulizi dhidi ya raia. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Mnaodhulumiwa lindeni kura zenu

Mbukuzi anguruma Chuo Kikuu:
Wasomi mnatakiwa kukomesha dhuluma

Kuelekea uchaguzi mkuu 2000:
CUF yaiteka Dar

Maalim Seif afunguliwa mashitaka

‘Tume ya Keenja’ haikufanya ilichoagizwa - Wananchi

MPASHO NASAHA
WE THIO LAFKIYANGU TEENA!

Ushauri Nasaha
Namna ya kumfanya mtoto wako aweze kuzungumza

MAKALA
Kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani

WAZO  LA  WIKI
Ajenda mpachiko

MAKALA
Kuporomoka kwa maadili  katika jamii yetu; Sababu na utatuzi wake

Kalamu ya Mwandishi
Ulaya yaiambia Afrika iboreshe demokrasia kabla ya kufutiwa madeni yake

Makala
Wasifu wa marehemu Sheikh Said Sabiq

MAKALA
Uchaguzi Mkuu Mwaka 2000 (5):
Wananchi mjiandae kulinda kura

HABARI ZA KIMATAIFA

Riwaya
Kisasi cha mauti -2

Lishe
Ni kwa jinsi gani wanawake wanapata utapiamlo

MASHAIRI

MICHEZO

  • Kajumulo atishia kuwanyang’anya Kibadeni Simba
  • Kipukuswa kufuata nyayo za ‘Mgosi’ Hazali
  • Hazali sio Yanga ni Simba ‘kindakindaki’

  • Madadi azionya timu za Ligi Kuu 


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita