NASAHA
Na. 042 Jumatano Aprili 5 - 11, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Mbukuzi anguruma Chuo Kikuu: 
Wasomi mnatakiwa kukomesha dhuluma 

Na Mwandishi Wetu

VIJANA wasomi wa Kiislamu nchini wametakiwa kujitokeza na kusimama imara kukomesha dhuluma iliyoelezwa imeshamiri katika jamii na hivyo kuhatarisha mustakabali wa taifa hili.

Wito huo umetolewa na Amir wa Shura ya Maimamu nchini Sheikh Juma Mbukuzi , alipozungumza na wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumapili iliyopita. 

"Nyie vijana wa chuo kikuu lazima muwe wacha-Mungu ili (muweze) kuupiga kumbo udhalimu katika dunia ..." alisema Sheikh Mbukuzi alipoongea na wanafunzi hao katika msikiti wa Chuo Kikuu hicho. 

Aliwambia wasomi hao kuwa dhuluma katika jamii ni lazima iondolewe kwa gharama yoyote na kwamba "wanaodhulumu wasiungwe mkono". 

Amir huyo wa Shura ya Maimamu aliwaambia wanafunzi hao kwamba kwa mujibu wa dini yao ya Kiislamu kuubadilisha utawala usio na uadilifu ni suala la wajibu. 

"Kuubadilisha utawala ulio dhalimu ni wajibu katika dini yetu ya Kiislamu ... Hadith nyingi za Mtume (s.a.w.) zinafundisha kuondoa dhuluma kwa gharama yoyote" alisema Sheikh Mbukuzi. 

Akionesha haja ya kuleta mabadiliko nchini, Amir Mbukuzi alisema jamii ya Watanzania imegubikwa na madhila mengi ikiwemo hali mbaya ya uchumi na ukiukwaji wa haki za raia. 

"... na anayechafua mazangira tunamjua, hivyo Oktoba dhalimu aondolewe ..." alisema Amir huyo na kisha akaonya kwamba iwapo mabadiliko hayataletwa basi hali hiyo mbaya itazidi. 

Hata hivyo Amir huyo wa Shura ya maimamu alilitia moyo kundi hilo la wasomi kuwa dhuluma huwa haidumu. 

"Hakuna dhuluma inayodumu", alisema Amir Mbukuzi 

Mwezi Oktoba mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa madiwani, Rais na wabunge ambao ni wa pili katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika mwaka 1995 ambapo mgombea wa CCM, Bw. Benjamin William Mkapa, alishinda kiti cha urais. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Mnaodhulumiwa lindeni kura zenu

Mbukuzi anguruma Chuo Kikuu:
Wasomi mnatakiwa kukomesha dhuluma

Kuelekea uchaguzi mkuu 2000:
CUF yaiteka Dar

Maalim Seif afunguliwa mashitaka

‘Tume ya Keenja’ haikufanya ilichoagizwa - Wananchi

MPASHO NASAHA
WE THIO LAFKIYANGU TEENA!

Ushauri Nasaha
Namna ya kumfanya mtoto wako aweze kuzungumza

MAKALA
Kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani

WAZO  LA  WIKI
Ajenda mpachiko

MAKALA
Kuporomoka kwa maadili  katika jamii yetu; Sababu na utatuzi wake

Kalamu ya Mwandishi
Ulaya yaiambia Afrika iboreshe demokrasia kabla ya kufutiwa madeni yake

Makala
Wasifu wa marehemu Sheikh Said Sabiq

MAKALA
Uchaguzi Mkuu Mwaka 2000 (5):
Wananchi mjiandae kulinda kura

HABARI ZA KIMATAIFA

Riwaya
Kisasi cha mauti -2

Lishe
Ni kwa jinsi gani wanawake wanapata utapiamlo

MASHAIRI

MICHEZO

  • Kajumulo atishia kuwanyang’anya Kibadeni Simba
  • Kipukuswa kufuata nyayo za ‘Mgosi’ Hazali
  • Hazali sio Yanga ni Simba ‘kindakindaki’

  • Madadi azionya timu za Ligi Kuu
     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita