|
Mashairi
Lipumba usilale
Lipulipu usilale, CCM bado tele,
Vijijini wengi tele, fanya hima twende kule,
Nikote si peke Hale, mambo bwana Lipu kule,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Usiamini mayowe, ukahisi mwambawewe,
Kura Bwana si mayowe, kura ni tiki upewe,
CUF bado utambuwe, kina mama wambiwe,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Kura ziko vijijini, kura haziko mijini,
Mijini bwana rahani, kupiga hawatamani,
Mijini ushabikini, si watu wakuamini,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Utangaze matawini, wote wawe safarini,
Wote kwenda vijijini, wakafanye kampeni,
Sivyo Lipu hutawini, amini hiloamini,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Nenda nawe vijijini, watuwawe na imani,
Wakujue waamini, wajue wasema nini,
Sivyo baba naamini, hutashinda abadani,
CCM namba wani, vijijini masikani.
CCM namba wani,huko kote mashambani,
Wapinzani ndio nini, watavuruga amani!,
Kwanza CUF cha udini, wanasema vijijini!,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Wamechoka naamini, watu wote vijijini,
Tatizo kukuamini, ukifuzu tutawini,
Lipumba baba amini, mambo iko vijijini,
CCM namba wani, vijijinimasikani.
Tangaza wajemjini, watu wako vijijini,
Sema bendera shikeni, rudi sasa vijijini,
Matawi kafungueni, HAKI SAWA tangazeni,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Baba niko ukingoni, Lipu yangu yashikeni,
CUF mimi idamuni, ikishindwa nitabuni,
Kwani mwingine sioni, na hofu uchumi duni,
CCM namba wani, vijijini masikani.
Beti kumi kaditama, zanitosha mie mwana,
Fatuma Magimbi mama, msalimu sanasana,
Azidi mama kusema, Bunge azidilibana,
CCM namba wani, vijijini masikani.
AlmasiH. Shemdoe,
(Tunda la Matumaini), Dar es Saaam.
Nendeni salama mahujaji
Utukuke rabikwanza, ombi waende salama,
Wacha waende jifunza, yaHijauliosema,
Kishawajekutufunza,yakotuyatende vyema,
Ndugu nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Nenda nendenisalama, kule Makkha naMadina,
Nendeni na kusimama, Arafa na huko Mina,
Kafanyeni yote mema, mfanyieni Rababa,
Ndugu nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Nguzo ya TANO kanena, Rabi kasema bayana,
Nguzo hii bora sana, bora kuwasiliana,
Hali zetu kujuana, amani kutakiana,
Ndugu nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Hija nuru ya upendo, Rasuli kasema sana,
Hija hujenga upendo, moo moomoo sana,
Kuipata ni uhondo, jambo la hahati sana,
Ndugu nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Hija ni kama kitovu, kwa mwsaka yalokubana,
Hija kufuta maovu, kwa mwaka yalokabana’
Hatutaraji uovu, hapa mkirudi tena,
Ndugu nendeni salama, Mahujajiwetu wema.
Mtaona mengisana, kufuta potofu dhama,
Kwanza kutobaguana, japorangi nyingi sana,
Piakushirikiana, mbora hapo Rabana,
Ndugu nenden salama, Mahujaji wetu wema.
Tena mtaulizana, yalonenwa mwaka jana,
Hivi kweli yamefana yote mloambizana,
Mapya mtaagizana, diniisikwame tena,
Nenda nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Mafunzo nimengisana,iliuchaji kufana,
Udugu wa damusana, usawa nakujuana,
Utiifu kwa Rabana, na upweke kwake tena,
Nenda nendeni salama, Mahujajiwetuwema.
Dua mkaombe sana, kwa yote yanotubana,
Kamuombeni Rabana, hali yetu duni sana,
Ibada mashaka sana, kihali dhaifu sana,
Nenda nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Hapa mwisho sasa ona, ona kalamu yagoma,
Jamani kwaheri sana, Mahujaji hija njema,
Nendeni kushikamana, nenda Makhalifa wema,
Nenda nendeni salama, Mahujaji wetu wema.
Almasi H. Shemdoe.
(Tunda laMatumaini)
Kidogo, Dar es Salaam.
Haki ama propaganda!
Hodi tena Mhariri,naingia gazetini,
Ingawa s mashuhuri, kuingia mitamboni,
Naja nalangu shairi, usilitupe kapuni,
Hakihizi haki gani, TAMWA mnazozidai.
TAMWA wamebeba bango, kinamama hima hima,
Wachemsha watu bongo, kidete wamesimama,
Wanadai kwa usongo, kutetea kinamama,
Kinamama tambueni, si haki balini hila.
Ha! Eti wadai haki, usawa upatikane,
Nyumbani hakukukaliki, mambo yawatengamane,
Mama tena hashikiki, haki itambulikane,
Wanawake tambueni, si haki bali ni hila.
Haiingi akilini, pindi unapofikiri,
Zamu kwa zamu jikoni, wanadai kwa fahari,
Ikiwa madarakani, mwanamke ni mahiri,
Hizi tena sio haki, bali ni propaganda.
Mimba zibebwe kwa zamu, hiki tena si “kiroja”!,
Kina mama mfahamu, zisizo mashiko hoja,
Wataka kuwahujumu, mje kukosa faraja,
Hizi tenasio haki, bali ni propaganda.
Usawa uwepo kote, ofisini nashuleni,
Haki ipiganiwe pote, mavazi pia makini,
Mila tena zisifwatwe, TAMWA wawashaurini,
Haki hizi hakigani, TAMWA mnazozidai.
Suruali ivalike, hata ofisini pia,
Nchini ifahamike, mwanamke mtetea,
Na mama ajumwike, urais kugombea,
Hee sikiroja hiki, haki zinazodaiwa!.
Kurudi kuwe ni sawa, kati yababa na mama,
Pasiwepo kuchelewa, wameiweka azama,
Uke wenza wahofiwa, kuwanyonya kinamama,
Wanawake tambueni, si haki ila ni hila.
Mama atoe talaka, machungu yakimfika,
Mirathi iwe hakika, sawa kwa kugawika,
Fukutolimweashika, agenda mbovusimika,
Wanawake tambeuni, sihaki bali ni hila.
Matokeo ni fedheha, hakuna usaidizi,
Kadhia zimeenea, kila kona machukizi,
Na kubakwa kumepea, hakuna cha ufumbuzi,
Hila na propaganda, wanawakewaumia.
Witirini ninakoma, hoja nazikaribisha,
Kusema yalo murua, ukweli kuuonyesha,
Naomba nyote tambua, TAMWA sasaimechosha,
Hila na propaganda, wanawake waumia.
Bi-Fatma,
Dar es Salaam.
Chombo hiki chombo gani kinayumba baharini?
Mhariri gazetini, nimekuja kwa huzuni,
Niweke hata pembeni, kwenye kurasa za ndani,
Ili ninene tungoni, swaliniwaulizeni,
Chombo hiki chombo gani kinayumba baharini.
Chombo kimetoka mbali, ndugu nawatarifuni,
Nahodha kimebadili, mara tatusikieni,
Watatu ameshafeli akizamisha majini,
Chombo hiki chombo gani kinayumba baharini.
Si meli wala si boti Malenga msihariri,
Hakijajengwa kwa bati mbaowala misumari,
Msipoteza wakati kwa undani kufikiri,
Chombo hiki chombo gani kinayumba baharini.
Nahodha ameamua, chombo chetu kukitweza,
Abiriaataua, namalikuzipoteza
Kosale anatambua chombolinalohemeza,
Chombo hikichombogani kinayumba baharini.
Chombo hichochombogani, mabingwa kitegueni,
Kinazama bahari kijukuunimondani,
Kinazamishwa nanini, sitakikuwambieni,
Chombo hiki chombo gani kinayumba baharini.
Nahodha huyu ni nani Rasakiupo makini,
Chombo ameanza linikuongoza baharini,
Achiduka kaa chinichombo hikikubaini,
Chombo hiki chombogani kinayumbabaharini?
Wino umeniishiana luku ipo mwishoni,
Mezani ninakimbiaswalinawaachieni,
Chombo nakishuhudia msonde nimashakani,
Chombo hiki chombo gani, kinayumba baharini
Y. Kijukuu,
Safarini Mkulanga
Nifanyeje Walimwengu (Jibu)
Hodi hodi Muhariri, naja kwako gazetini,
Angalia natafsiri, manenoye kwa makini,
Bichwa sugu nakariri, mshahirilikizoni,
Vuta subira kijana, maishasiyakimbie.
Fanya kazi kwa bidii, isije ukawa mwizi,
Kujinyonga siyo dili, kamulize hata inzi,
Chooni anajadili, hata naosisimizi,
Maisha si yakimbie, jitahidiutashinda.
Kuwa kucha unalia, wajuasababu zake?
Shambani ulikimbia, ukaingilia mateke,
Na wifi akakimbia, akakuacha mpweke,
Usiogope maisha, jipemoyo utashinda.
Bichwa sugu kaka yanguusije konda mwanetu,
Usiutake uzungu, ukawa kama kamtu,
Usizugwe namahangu, ukawavuliautu,
Kama wayashindwa wewe, naniayaweze hayo?
Kujinyonga si kifani, mbona wawatangazia?
Hata kama mpagani, Munguanakutambua,
Hata ukawa chumbani, motoni utaingia,
Hilolinge kuwa dili, watuwangeliendea.
Kifo kipo nakwambiawala usikimbilie,
Waulize Namibia, iliwakuimbilie,
Kaburinitaingia, wala usikimbilie,
Ingoje siku yako mbona una wasiwasi.
Elfu mbili humalizi, elfutatuhuingii,
Hata hawa sisimizi, wakuuisiakimwili,
Pika hata maandazi, mchukuehuyo wifi,
Kama huna mtajjii, sema watutukugee.
Msamala Muslim,
Asha Juma,
S.L.P. 985, Songea,
Safarini South Afrika.
Nyota naomba mchango No 1
Mimi Nyota Jemedari, inayong’ara kusini,
Nataka nunua gari,yenye pambolathamani,
Hii gari niJohari, ni pepo ya duniani,
Nyota naomba mchango, nipate nunua gari.
Nipate nunua gari, nirande nayo mijini,
Nawaomba mabepari, pamoja na masikini,
Ni mchango wa hiyari, Nyota nisaidieni,
Nyota naomba mchango, nipate nunua gari.
Nyota nanunua gari, initoe mashakani,
Gari zao matajiri, kupanda sizitamani,
Wanazo nyingi jeuri, na matusi midomoni,
Nyota naomba mchango, nipate nunua gari.
Ni gari ya kifahari, siyo siri nabaini,
Yenye kubwa matairi, nimeagiza Japani,
Watakoma mabepari, kuninyanyasa njiani,
Nyota naomba mchango, nipate nunua gari.
Japo Nyota ni fakiri, sina kitu mfukoni,
Kuikosa hii gari, sikubali abadani,
Ili nitoe kiburi, kwa walo nazo jirani,
Nyota naomba mchango, nipate nunua gari.
Tamati hili shairi, nimefika kituoni,
Michango ninasubiri, toka kote duniani,
Hata kama ni hariri, nitapokea jamani,
Nyota naomba mchang, nipate nunua gari.
Muhammed Mbiku
(Nyota ya Kusini).

|
YALIYOMO
Tahariri:
Katiba
ya Zanzibar ni ya Wazanzibari
‘CUF
tumejiandaa kuchukua serikali'
Suala
la Mwembechai lazua mtafaruku
Mabadiliko
ya katiba ya Zanzibar: CCM Z'bar ina nafasi ya ushindi
MPASHO
NASAHA
Ulimbukeni
wa siku ya Valentino
Habari
za ndani
NCCR-Mageuzi
wamkataa Msimamizi wa Uchaguzi
Ushauri
Nasaha
Nafasi
ya familia katika makuzi ya mtoto
MAKALA
CCM
imepindua nini?
WAZO
LA WIKI
Vitisho
vya kikachero visihamishiwe mashuleni
Makala
ya Kimataifa
Mtazamo
wa maadui wa Uislamu juu ya Uislamu
Kalamu
ya Mwandishi
Katiba
irekebishwe, lakini kwa maslahi ya wananchi
MAKALA
MAREKEBISHO
YA 13 YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO -2
Vita
dhidi ya demokra
HABARI
ZA KIMATAIFA
Clinton
kusaidia amani Burundi
Nigeria
yaazimia kuwa taifa la Kiislamu
n.k
Riwaya
Ndoto
ya mafanikio - 2
LISHE
Madhara
ya mafuta mwilini
Barua/Maoni
MASHAIRI
MICHEZO
Makoye,
Mapunda wateta Dar
Tino,
Katolila, Omar 'wautwaa' ukocha
Tuna mashaka
na Shungu - Yanga
|