NASAHA
Na. 036 Jumatano Februari 23 - 29, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Makala ya Kimataifa 
 
 

Mtazamo wa maadui wa Uislamu juu ya Uislamu 




KUTOKANA na mbinu na harakati za makafiri kwa kukwepa ukweli uliopo juu ya dini ya kweli mbele ya Mungu ya Uislamu, wanajaribu kupaka matope utaratibu wa ustaarabu wa maisha ya binaadamu ya kila siku. Mwandishi MNESE RASHIDI anaelezea zaidi.

MATAIFA ya Magharibi yanaongoza kundi la kukandamiza Uislamu katika dunia hii tangu awali walipoteketeza watu na rasilimali kubwa ya vitabu katika maktaba nyingi za Kiislamu za mashariki ya kati na Ulaya mashariki kwa lengo la kuumaliza Uislamu. 

Tangu kipindi hicho mpaka sasa maadui wa Uislamu wamekuwa wakiendeleza juhudi mbalimbali za kuvunja dini hii. Kwa mtazamo wao makafiri hawa ni kuijazia propaganda jamii yetu kuwa Uislamu ni "ugaidi" na kama sio "ugaidi" basi ni kitu cha hatari sana na tishio kwa ustaarabu wa mataifa ya magharibi na dunia kwa ujuma, kwa mtazamo wa propaganda hizo mataifa ya magharibi na Marekani nia yao kubwa ni kutokomeza Uislamu au Waislamu duniani. 

Kutokana na harakati hizo za makafiri upo ushahidi wa wazi wa kupigwa vita dini ya Mungu "Uislam" kama tunavyoshuhudia vita vinavyoendelea huko Chechnya na ndivyo unavyofanana na vita vilivyotokea Basnia, Somalia na Kosovo. Makafiri wanaita vita hivyo (ethnic cleasing) ikiwa na tafsiri ya kuutakasa jamii au kukihirisha kukundi fulani cha watu. 

Hali ya machafuko ya kuangamiza halaiki za jamii ya Kiislamu. Pia inakumba nchi nyingi za Asia, Africa ya kati magharibi, kaskazini na kusini. Watu kuteswa kwa kupigwa virungu, kupata ulemavu wa viungo na kudhulumiwa mali zao na vitisho vikali kwa kuwa ni waumini wa Kiislamu. 

Makafiri wanatumia vyombo vya habari (magazeti, Redio na Televisheni) ambavyo vinatoa habari potofu juu ya dini ya Uislamu, habari ambazo zinaandaliwa na kuandikwa na mashirika ya mataifa mengi ya hayo ni ya nchi za Magharibi. 

Hivyo hufanya jamii kuona moja kwa moja ya kuwa Uislamu kama "ugaidi", wakati ni dini iliyo kamilika, iliyoshushwa ikiwa kamili na utamaduni wake, kinyume chake tunaambiwa na vyombo vya habari kuwa Uislamu ni "siasa kali" na wala sio Imani tena ya kumcha Muungu. 

Na kwa kweli, kadri mambo yalivyo ushahidi unaonesha kuwa baada ya ukomunisti, sasa adui nayefuata kupigwa vita na kuangamizwa ni Uislamu! 

Karne hii ya 21 ambayo imeingia mwezi mmoja (uliopita) sasa imekuwa ni karne ngumu sana kwa Waislamu wa Ulaya. Aghalabu katika historia pametokea huko mauwaji ya kikatili hivi sasa Chechnya na yaliyotokea huko Bosnia na Kosovo. Hivi ni dhambi kuzaliwa mtu Muislamu Ulaya, Marekani na sehemu nyingine duniani? 

Wakati wa vita baridi baina ya Ulaya mashariki na magharibi au wakati wa malumbano ya itikadi. Kati ya usoshalisti na ukomunisti ni watu wachache waliofahamu kuwa kumbe kulikuwepo Uislamu na Waislamu wengi huko Yogoslavia, Urusi (USSR) na China. 

Itikadi ya Ukomunisti iligandamiza Uislamu. Kuanguka kwa himaya ya Urusi (USSR) ambayo iliashiria kuporomoka kwa dola za ukomunisti Ulaya yote ya mashariki kuliondoa pazia lililofunika imani ya Kiislamu katika nchi hizo. 

Watu wengi wameshuhudia 1994 shirikisho la Urusi lilipokuwa linajaribu kuzuiwa uasiw a jimbo la Chechnya ambalo lilikuwa lilikuwa linataka kuyatenga; wapiganaji wa Chechnya walikuwa wakitukuza Mungu kwa takbir Allah Akbark!! Juu ya udhalimu unaofanyika juu ya haki yao. 

Katika vita vile vya mwaka 1994 watu wa Chechnya walishinda vita vile vile na kumlazamisha Mrusi kuingia mkataba wa kuacha mapigano. Walishinda vita vile katika mazingira magumu sana; walipigana kwa silaha duni dhidi ya vifaru na ndege za kijeshi za shirikisho la Urusi. 

Baada ya kuona mfano wa Chechnya kwamba kudai uhuru siyo lazima kubembeleza, majimbo mengine jirani ya Chechnya ambayo pia wakazi wake ni Waislamu nayo yakataka uhuru wake na nje ya shirikisho la Urusi kwa nguvu za silaha. Juhudi za hizo za ukombozi zilizuiwa kwa nguvu za kijeshi za Urusi. 

Ndipo Urusi ikaamua kuikalia Chechnya kijeshi ili kuhakikisha kuwa nchi nyingine hazifuati mfano wake. Ingawa palitokea milipuko ya mabomu mjini Moscow na baadhi ya miji mingine, wakati hakuna ushahidi kwamba vitendo hivi vya kigaidi vilitokea au chimbuko lake lilikuwa Chechnya. 

Ni dhahiri kwamba Urusi ilikuwa imepania kuisambaratisha Chechnya. Kwa sababu mbili, moja kuitakasa Urusi au kuwafuta jamii ya Waislamu wasiwepo katika ardhi yaUrusi kwa visingizio vya "ugaidi" na "siasa kali" na kuhakikisha kuwa hapatakuwepo tena majimbo yatakayotaka kujitenga ndani ya Urusi. 

Ushahidi mwingine wa maadui wa Uislamu ni pale jamii kushangazwa na kitendo cha kukaa pembeni kwa mataifa ya magharibi ikiwemo (USA) Marekani na kutochukuwa hatua zozote. Kushinikiza Urusi kuacha vita vyake hivi vya kuangamiza watu halaiki (genocide) ndani ya Chechnya. Inaonesha jinsi gani Serikali za Ulaya Magharibi na Marekani hufurahia na kukubaliana moja kwa moja kwa mapigano hayo kwa kile kinachoitwa Waislamu ni magaidi, wamalizwe! 

Ingawa Urusi ina nguvu za mabomu ya nyuklia, lakini Urusi ya leo ni kama Tanzania tu, inategemea mikopo ya IMF na Benki ya Dunia, taasisi zilizo katika himaya ya nchi za Magharibi. 

Matukio kama haya hayana tofauti kama yale yaliyotokea katika nchi yetu ya kadhia ya Mwembechai, malalamiko ya Waislamu juu ya haki zao za msingi kama elimu, nafas za uongozi na pia kujiunga na taasisi ya OIC ambao alikabidhiwa Mheshimiwa Rais katika siku ya Baraza la Idd, Diamond Jubilee Januari 19, 1999 na kujibu tofauti na mtazamo wa watu wengi kwa kupuuza mambo muhimu yanayoiathiri jamii moja anayoiongoza na kunadi kuwa ni kiongozi anayejali maslahi na haki za Watanzania. 

Kwa hiyo basi, inashangaza sana kwamba mataifa haya yamefumbia macho dhuluma ya kuuawa kikatili kwa watu wasio na hatia wa Chechnya na kwengineko duniani. Mauaji haya yanatisha kwa kiasi kikubwa na yanafanya watu wajiulize, hivi ndivyo baadhi ya binadamu wanashangilia kuona milenia mpya huku watu wengine wanapigwa risasi na mabomu? Kama mambo haya yalianza karne ya 20, karne ya 21 je itakuweje? 

Kwa mtazamo wa watu wenye busara wanahoji kuwa kinachochochewa kuongezeka ni ustarabu au ushenzi katika jamii zetu za wanaadamu, zaidi pale inapotokea kukandamizwa kwa jamii fulani; kutopatiwa haki kama watu huru, kuwanyanyasa na kuwatesa kwa misingi ya udini na ubinafsi. 

Sasa kinachopandwa katika Uislamu ni mbegu za chuki juu ya madhalimu wa haki zao za msingi, lazima ifahamike ya kuwa haki ya watu ipo na itapatikana angalau itachelewa; cha msingi ndugu Waislamu ni kutafakari mambo muhimu ya dini yetu na kuongeza dua za maombi kwa Allah juu ya maadui zetu. 

Juu

YALIYOMO
 

Tahariri:
Katiba ya Zanzibar ni ya Wazanzibari

‘CUF tumejiandaa kuchukua serikali'

Suala la Mwembechai lazua mtafaruku

Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar: CCM Z'bar ina nafasi ya ushindi

MPASHO NASAHA
Ulimbukeni wa siku ya Valentino

Habari za ndani
NCCR-Mageuzi wamkataa Msimamizi wa Uchaguzi

Ushauri Nasaha
Nafasi ya familia katika makuzi ya mtoto

MAKALA
CCM imepindua nini?

WAZO  LA  WIKI
Vitisho vya kikachero visihamishiwe mashuleni

Makala ya Kimataifa
Mtazamo wa maadui wa Uislamu juu ya Uislamu

Kalamu ya Mwandishi
Katiba irekebishwe, lakini kwa maslahi ya wananchi

MAKALA
MAREKEBISHO YA 13 YA KATIBA YA  JAMHURI YA MUUNGANO -2
Vita dhidi ya demokra

HABARI ZA KIMATAIFA

  • Clinton kusaidia  amani Burundi
  • Nigeria yaazimia kuwa taifa la Kiislamu
  • n.k

  • Riwaya 
    Ndoto ya mafanikio - 2

    LISHE
    Madhara ya mafuta mwilini

    Barua/Maoni

    MASHAIRI

    MICHEZO

  • Makoye, Mapunda wateta Dar 
  • Tino, Katolila, Omar 'wautwaa' ukocha 
  • Tuna mashaka na Shungu - Yanga

  •  

     

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com


    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita