|
Mashairi
Miaka 37 ya uhuru, lakini mhh!
Naanza kwa kumtaja, Mola aliye Karima,
Duniani amejaa, kwa zake nyingi rehema,
Sifa hii haikuja, bali kwa zake hekima,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Hodi hodi gazetini, Mhariri nimekujua,
Maswali yamenihini, majibu sijayajua,
Sikizeni kwa makini, malenga mtayajua,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Neno lanishangaza, siku nyingi nimewaza,
Bali leo nauliza, kitu hiki chanikwaza,
Mabangoni wamejaza, uhuru kuutangaza,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Muda mwingi umetimu, leo inaadhimishwa,
Tatu saba imetimu, ukoloni kuhamishwa,
Imekatika misimu, wananchi tumechoshwa,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Zimekithiri nchini, kero zimetapakaa,
Ofisini na shuleni, huduma za kubagua,
Uhuru huu ni nini, leo washeherekea,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Wananchi wateseka, hujuma zimeenea,
Nzasa wanasikitika, ukimbizi wahofia,
Bagamoyo na Tandika, matunda wayazuia,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Watu wengi wateseka, huduma zilivyo duni,
Viongozi waneemeka, hawatekelezi ilani,
Kodi nayo waitaka, matunda hatuyaoni,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Islamu tunalia, uonevu umezidi,
Chuki anaangamia, Salehe kama shahidi,
Sote tunashuhudia, imetoweka ahadi,
Uhudu wa Tanzania, maana siitambui!
Uhuru huu wa nani, ndugu nisaidieni,
Ni wa Anna ama Johni, jibu nibainishia,
Nimechunguza makini, uhuru huo sioni,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Kadi tama kituoni, wenzangu nawaachia,
Jibu nisaidieni, bado nasisitizia,
Nami niwe shereheni, uhuru nikitambua,
Uhuru wa Tanzania, maana siitambui!
Fatma H. Mkombozi,
Jangwani High School,
Dar es Salaam.
Mola wasitiri
Rabi Mola wasitiri, viumbe walofariki,
Waondolee shubiri, hiyo siku ya hilaki,
Uwaepushie shari, na adhabu za makuki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Maombi yetu Ghafuri, twaomba uyaafiki,
Vifo vimetuathiri, hiki baada ya hiki,
Nyoyo zimetahayari, huzuni kutamalaki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Vimetutia dosari, hali hatuzimiliki,
Idadi naikariri, watatu walohiliki,
Mwanavita ya Bakari, mauti kumdiriki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Wa pili yake nambari, alefuata twariki,
Abdallah mashuhuri, mwadini ndie atiki,
wa tatu namuhubiri, alepambana na dhiki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Mamepuju jamadari, maradhi yalimsaki,
Hali ikawa dhahiri, mwili kuwa kititiki,
Juhudi za daktari, nduli kaziona feki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Wote hawa majasiri, mwadini alishiriki,
Kawazaa kwa uzuri, malezi yalibariki,
Idadi naisitiri, kuibaini si haki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Kigombe yao bandari, kwengine hawahusiki,
Walidumu kwa fahari, bila kuwa mamluki,
Kizazi kilishamiri, kufikia halaiki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Mwazema fukolaari, Kigombe hawashikiki,
Kwa wingi na uhodari, na mali kutowadhiki,
Mola kawajaza mori, kutafuta hawachoki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Dua ni kwake Jabari, tumuombe mwenye haki,
Awaepushe na shari, humo ndani ya handaki,
Uwape sitighifari, pepo isiwadhihaki,
Harufu zitamalaki, bustani za kaburi.
Ally Mwazema Saidi (Nyenga),
P.O. Box 2112,
Tanga.
Upinzani dhidi ya
|
YALIYOMO
Tahari
Kama hakuna haki watu watachukua sheria mkononi
Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu:
Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa
Afariki baada ya kutokwa damu nyingi:
Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000
Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa
Kamanda Gewe atakiwa amkamate
Daniel
Sheikh awasambaratisha walevi
Liwale
Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango,
madirisha
Mjue Usama bin Ladin -2
Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya
sensa
Njaa hakuna, tunategemea kula
silaha
Parole kwa mbinde!
Mabaraza yawatetee Waislamu
- Sheikh Bafadhil
Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa
inatisha
Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza
magazeti ya ANNUUR
I.P.C yatakiwa kujitangaza
Kutoka magazeti ya zamani
Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa
Na Muhibu Said
Waislamu wachoma moto nguruwe
Tume ya kubadili Katiba Kenya:
Waislamu kuwakilishwa
Waislamu Msonge waomba wanusuriwe
Sayansi na Teknolojia
[PELEKA FAX NCHI ZA NG’AMBO BURE! – (2)]
Masomo ya Kiislam
Barua za Wasomaji
Mashairi
Chakula na Lishe
[Mwongozo wa mlo wa kila siku]
|