AN-NUUR 
Na.185 Shawwal 1419, Januari 29 - Februari 4 , 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa
 

MSIKITI wa Mwinyimkuu upo katika Jijini la Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni kata ya Mzimuni Magomeni Mapipa katika mtaa wa Mwinyimkuu kitabu No. 38. 

Kuna idadi ya nyumba zisizopungua mia tano na nne (504) zilizogawanyika katika mitaa ipatayo ishirini (20) yenye kukaliwa na familia zipatazo elfu moja mia nne na mbili (1,402) zenye jumla ya wakazi wasiopungua watu elfu sita mia nne na sabini na moja (6,471) kwa hesabu iliofanywa kati ya mwezi wa tisa na kumi na moja (9-11), 1998. 

Katika hesabu hiyo, idadi ya watu wazima wanaume ni elfu mbili mia moja na themanini na tisa (2,189), ambayo ni wastani wa asilimia thelathini na nne (34%). Wanawake elfu mbili mia moja na kumi na sita (2,116) ambao wanafanya wastani wa asilimia thelathini na tatu (33%). 

Kwa upande wa watoto, wapo elfu mbili mia moja na sitini na sita (2,166) ambao wanafanya wastani wa asilimia thelathini na nne (34%) ikiwa takriban sawa kiasilimia kati ya watoto wa kiume na wale wa kike, lakinI kwa kihesabu wanaume ni elfu moja na sabini na sita (1,076) na wa kike wapo elfu moja na tisini (1,090). 

Katika utaratibu huu uliofanywa na Msikiti wa Mwinyimkuu ulisajili jumla ya wajane mia moja na hamsini na sita (156) ambao sawa na asilimia mbili (2%) ya watu wote au asilimia nne ya watu wazima. Pia iliwaratibu watoto mayatima mia mbili na hamsini na saba (257) ambao sawa na asilimia nne (4%) ya wakazi wote au asilimia kumi na mbili (12%) ya watoto. 

Jamii yote hiyo iliyotajwa hapo juu inauhitaji na kutumia Msikiti wa Mwinyimkuu katika shughuli zao mbalimbali za kijamii za kila siku, mfano mazishi, ibada za kila siku n.k. 

Ambapo pia umekuwa ni kiungo muhimu kwa jamii nzima ya eneo hilo kutokana na kuwepo karibuni na sehemu inayotumika kuzikia (makaburi) ya eneo hilo. 

Kutokana na wakati wetu wa sasa tulionao, na tunapokwenda ambapo mambo yote hususan mipango inayohuSu miradi ya kimaendeleo, inahitajia takwimu katika upembuzi wake kabla kufikia hatua ya kufanyika uamuzi wa jambo lolote linalohitajia, mfano fedha katika hatua zake za awali au nguvu kazi, hivyo basi ilibidi kwanza ijulikane idadi ya watu wanaoishi katika eneo letu ambalo tutaweza kuwatumia katika kufikia hayo malengo yetu ya kunyanyua na kukuza maendeleo na hali ya jamii ya Kiislamu inayotuzunguka kwa manufaa yetu ya hivi sasa na kuweka misingi imara kwa vizazi vijavyo. 



Njaa hakuna, tunategemea kula silaha 

KWANZA namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia. Nchi yetu ya Tanzania imekuwa ikidumu katika amani miaka mingi, tangu tupate uhuru mwaka 1961. Hakuna Mtanzania yeyote aliyewahi kufundisha watu wengine walete vita miongoni mwetu Watanzania pamoja na kwamba haki kwa waumini haipo, lakini hakuna vita vyovyote vilivyotokea hata kwa wale wanaodhulumiwa hawakuwa na uamuzi wowote wala mawazo ya kupigana hayakuwakaribia. 

Sasa katika upole huu wa Watanzania na uelewano wao wote huu walionao hata kabila moja hupendana na lingine na hata kushirikiana katika njia kuu za uchumi wa nchi yetu, na hapa tunaona hata kualikana katika sherehe za watu binafsi na zile za serikali, makabila yote huwa pamoja. Je, ni vipi serikali yetu ya watu wapole namna hii na wastarabu namna hii ione wamestahili kurahisishiwa kupata silaha. 

Badala ya kuwaletea ngano, mahindi kwa gharama yoyote ili wale chakula washibe ili waweze kudumisha amani sawa sawa. Hizi bunduki, tunaiomba serikali iwatangazie Watanzania kazi yake kwamba ni za kuleta amani au maafa kwa Watanzania au kuna agenda fulani ya baadhi ya watu au kundi fulani lipate kununua wa ajili ya kunyanyasa watu fulani. 

Maana maghala ya silaha yapo jeshini yametulia kwa kudumisha amani nchini, je huko madukani hata jambazi atanununua kwa kuwa wana mitaji mikubwa kutokana na silaha chache wanazoporea mali za watu? 

Ni mambo gani haya ya kuchezea maisha ya watu, serikali ifikirie upya suala hili kwani ni hatari mno. Je, wale waumini wa Msikiti wa Mwembechai wangekuwa wanazo bunduki ingetokea nini kati yao na polisi? Serikali imefikia hatua mbaya sana na uamuzi huu umekujaje, serikali imeona nini kutuagizia silaha? 

Hivi mambo ya Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Congo (Zaire), Congo Brazaville, Somalia, Siera Leone, Algeria, Uganda, Afrika Kusini, Kossovo, Ireland ya Kaskazini hamuoni watu wanavyo malizana kwa silaha na hata zingine tumezikamata hapa kwetu Tanzaina? 

Tukawalaumu Wanajeshi na watu binafsi wa Rwanda na Burundi, sasa vipi sisi tusiagize mahindi kumshibisha Mtanzania? Wanatanzania tunashindwa kuwaandikisha watoto wetu shule na madawati hatuna, je silaha tutaweza kununua? 

Serikali iwatangazie Watanzania ina agenda gani kuhusu bunduki hizo zinazotegemewa kununuliwa kama njugu. Hata hivyo, fedha hatuna sisi wadogo labda wabunge na mawaziri wao mishahara yao na marupurupu yao yanawaruhusu kuzinunua ili hata getini kwao watakapotuona wazitumie kutulenga ili tusiwasumbue. 

Vipi serikali imepitisha suala hili bila ya kutuuliza au ni mbunge gani ametumwa na watu wa jimbo lake kwamba pametokea wanyama katika kijiji au wilaya na kuomba silaha? Serikali ituambie bunduki ni za nini kwa watu waliona sifa ya amani. 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Kama hakuna haki watu watachukua sheria mkononi 

Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa 

Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 

Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa 

Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel 

Sheikh awasambaratisha walevi Liwale 

Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha 

Mjue Usama bin Ladin -2 

Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa 

Njaa hakuna, tunategemea kula silaha 

Parole kwa mbinde! 

Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil 

Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha 

Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR 

I.P.C yatakiwa kujitangaza 

Kutoka magazeti ya zamani 

Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa 
Na Muhibu Said 

Waislamu wachoma moto nguruwe 

Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa 

Waislamu Msonge waomba wanusuriwe 

Sayansi na Teknolojia 
[PELEKA FAX NCHI ZA NG’AMBO BURE! – (2)] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na Lishe 
[Mwongozo wa mlo wa kila siku] 
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita