|
|
|
WAISLAMU Jijini Dar es Salaam wamemtaka Kamanda Gewe amkamate Bw. Daniel Zakaria kwa kosa la kughushi hati za nyumba na kutaka kuzipora. Wito huo umetolewa kufuatia ushahidi mpya uliopatikana kuelezea jinsi Bw. Daniel alivyokuwa amefanya jaribio la kupora nyumba za Hajat Aziza Bint Omar toka akiwa hai. Ushahidi huo unaonyesha kwamba mwaka 1986 Bw. Daniel alighushi hati za nyumba na kuandika jina lake la Daniel Zakaria. Taarifa zilipelekwa kituo cha Polisi Msimbazi ambapo ilitolewa hati ya kusakwa Bw. Daniel. Hata hivyo Bw. Danile hakuonekana hadi alipofariki Hajat Aziza. (Marehemu) Hajat Aziza alipewa barua na Polisi akapewa hati mpya na jina la Daniel Zakaria likafutwa kwenye vitabu vya ofisi ya kodi ya mapato. Katika hali isiyoeleweka Bw. Daniel kupitia mahakama ya Kisutu alipewa kibali cha usimamizi wa nyumba hizo. Kufuatia shauku ya Waislamu kutaka kujua ni kwanini Bw. Daniel hajakamatwa, ANNUUR iliwasiliana na Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es Salaam Bw. Alfred Gewe. Hata hivyo, Kamanda Gewe alipoombwa
aeleze ni kwa nini Bw. Daniel hajakamatwa na hati ya polisi ya kukamatwa
mtuhumiwa humaliza uhalali wake baada ya muda gani, hakutaka kusema lolote
akidai kwamba suala hilo lishahukumiwa mahakamani.
SHEIKH Yasin Mpako wa Liwale amepongezwa na waumini kwa hatua yake ya kuwasambaratisha walevi ambao walikuwa wamevamia eneo karibu na Msikiti. Walevi hao walikuwa wakinywa pombe na kucheza ngoma jirani kabisa na Msikiti wa Mtaa wa Soko; hali iliyofanya watu wanaoswali wasisikilizane. Wakati mmoja ndani ya mwezi wa Ramadhani walevi hao wlaianza ngoma yao wakati swala ya Dhuhri ikikimiwa. Sheikh Mpako alitoa dakika 15 kwa walevi hao kusambaa lakini wakakaidi wakidai kwamba pombe ni yao na wana kibali cha serikali. Kufuatia ukaidi huo, Sheikh Yasin Mpako alichukua bendera yake na kuanza kuuzunguka uwanja huo kwa Tahlil na Takbir, waumini walifurika eneo hilo kumhami Sheikh wao jambo lililowafanya walevi watimke. Kufuatia hatua hiyo, Waislamu wa Liwale hasa waumini wa Msikiti wa Mtaa wa Sokoni wamekuwa wakimpa pongezi Sheikh Mpako kwa kuwaondolea kero ya walevi hao. |
YALIYOMO
Tahari
Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel Sheikh awasambaratisha walevi Liwale Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa Njaa hakuna, tunategemea kula silaha Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa
Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa Waislamu Msonge waomba wanusuriwe Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|