|
|
| Waislamu
wachoma moto nguruwe
MAELFU ya Waislamu mwanzoni mwa wiki hii walivamia shamba la Mkristo mmoja na kuwaua nguruwe wote. Tukio hilo la aina yake lilitokea katika viunga vya jiji la Jarkata nchini Indonesia hivi karibuni. Taarifa za vyombo vya habari zimeeleza kwamba kundi la Waislamu lilivamia shamba la ufugaji nguruwe la PT Kember baada ya viongozi wao kulalamika kuhusu uvundo. Gazeti la Observer la Indonesia limesema kwamba baada ya maafisa wa polisi na serikali kukataa kuingilia, kundi hilo la Waislamu lilichukua hatua. Katika tukio hilo, Waislamu waliwaua nguruwe wote na kuchoma moto nyumba kadhaa za shamba hilo. Indonesia ina watu wapatao milioni mia mbili na mbili (202) ambapo Waislamu ni asilimia 90 sawa na watu milioni mia moja thamanini na mbili (182). SUPKEM yaagiza majina
WAISLAMU wa Kenya watawakilishwa katika Tume ya kubadili Katiba ambayo imeanza kufanya kazi Januari 25, 1999. Sheria ya kubadili Katiba ya mwaka 1997 inataka Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya (SUPKEM) na Baraza la Shuura Muslim Consultative Council (MCC) kuteua Muislamu mmoja kuwa Kamishna katika Tume ya kubadili Katiba. Taarifa iliyotolewa na SUPKEM/MCC na kutangazwa na magazeti ya Kenya ya Januari 27, 1999 imewataka Waislamu kupitia jumuiya na taasisi zao kutoa mapendekezo ya watu wanaoona wanafaa kuchukua nafasi hiyo. Pamoja na sifa nyingine muhimu za weledi wa sheria na katiba, anatakiwa mtu ambaye ana rekodi ya kuwa karibu na Waislamu na kujishughulisha na masuala yao. Nafasi hii imetolewa kwa kuzingatia kuwa Waislamu wana sheria zao na taratibu zao ambazo ni lazima zilindwe ndani ya Katiba. Na hilo haliwezi kufanyika bila ya kuwepo mtu mweledi wa sheria za Kiislamu. WAISLAMU wa kijiji cha Msonge kilichopo tarafa ya Mvuha wamejiona wapo sawa na watu wasiokuwa Waislamu (Wakristo) kutokana na kutopata mafundisho ya dini yao na kuamua kuishi maisha yasiyokuwa ya Kiislamu. Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea kijijini hapo wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani alishuhudia Msikiti uliopo kijijini hapo ambao una uwezo wa kuswaliwa na zaidi ya waumini 20 (ishirini) kwa wakati mmoja, ukiswaliwa na waumini wasiozidi wawili kila swala ya jamaa. "Hali ya Uislamu ni mbaya mdogo wangu, kama unavyoona mwenyewe tunaswali watu wawili mwezi huu wa Ramadhani, sasa miezi mingine unafikiri hali inakuwaje?" Alisema Imamu wa Msikiti walioupa jina la Masjid Nuru Sheikh Jafar Maulidi. Kijiji cha Msonge ambacho kipo kilomita 23 kutoka makao makuu ya tarafa hiyo Mvuha kimegawanyika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza kuna eneo wanaloishi Wakristo na sehemu ya pili wanaishi Waislamu na Wakristo wachache. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umeonyesha kuwa kutokana na watu wa eneo hilo kuishi katika makundi mawili yenye imani tofauti bila kuwepo watu wa kutangaza na kuufundisha Uislamu kuwa ndio dini ya haki, imesababisha Waislamu wengi kuhisi kama Uislamu na Ukristo ni sawa tu. "Litakapofika kundi lenye kuutangaza Uislamu kama la kina Mazinge au Magezi litatusaidia sana hapa Msonge kwani vijana wetu wengine wanashiriki hata kuimba kwaya Kanisani", alisema Katibu wa Masjid Nuru Bw. Selemani Makila. Naye bibi kizee mmoja aliyekuwa anaswali Msikitini hapo peke yake alipoongea na mwandishi wa habari hizi nje ya Msikiti huo alisema: "Sasa hivi hali huku vijijini ni mbaya mjukuu wangu, Imamu wetu peke yake hana uwezo wa kuwavuta Waislamu waujue Uislamu wao na waingie Msikitini". Imamu wa Msikiti huo Sheikh Jafar Maulidi na Katibu wake Bw. Selemani Makila walipoulizwa wana mikakati gani ya kuunusuru Uislamu kijijini hapo walisema huku wakinyooshea kidole kiwanja kilichopo chini ya Mwembe. "Hapa ndio madrasa yetu kwa ajili ya watoto na inakufa wakati wa mvua kama unavyoona ipo chini ya Mwembe", walisema kwa pamoja viongozi hao. Hata hivyo wamewaomba Waislamu, taasisi za dini ya Kiislamu, watu binafsi waende kuwasaidia katika kuunusu Uislamu katika kijiji chao cha Msonge. |
YALIYOMO
Tahari
Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel Sheikh awasambaratisha walevi Liwale Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa Njaa hakuna, tunategemea kula silaha Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa
Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa Waislamu Msonge waomba wanusuriwe Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|