|
|
|
SUALA la uchaguzi wa chakula (mlo) - nile hiki au kile ni kongwe katika historia ya mwanadamu. Hata hivyo, uchaguzi huo kwa miaka mingi ya nyuma haukujengwa kwa misingi ya hoja za kina za kitaalamu. Katika zama zetu hizi, kutokana na mandeleo ya sayansi na teknolojia yake tunafanya uchaguzi wa vyakula kutokana na utafiti uliofanywa juu ya vyakula mbalimbali. Kwa utafiti huo, tunajua kwa kina kwanini chakula fulani kinatupa afya bora zaidi kuliko chakula kingine. Pia tunajua kwanini chakula fulani kinaua mtu akikila. Licha ya maendeleo hayo makubwa katika taaluma, bado kuna watu hasa katika nchi zetu za ulimwengu wa tatu kama Tanzania, ambao uchaguzi wa vyakula vyao vya kila siku unategemea ladha ya vyakula, hivyo mazoea ya kila kabila au mazoea ya sehemu wanakoishi. Wanasayansi hasa wa chakula na lishe wametengeneza mwongozo wa mlo wa kila siku (A daily Food Guide) ili kuwasaidia watu mbalimbali katika suala la watu wale nini ili kujenga afya bora. Makala yetu ya wiki hii inazungumzia dhana hiyo ya mwongozo wa mlo ili iwe ni sehemu ya juhudi ya kuondoa tatizo lililoko katika jamii mbalimbali ya kuchagua vyakula kwa hoja sizizo kuwa za kisayansi. Vyakula hugawanywa katika mafungu mbalimbali (mfano, manne, matano, saba n.k.) kutegemea na aina ya mwongozo wa mlo. Mwongozo wa mlo katika makala hii ni ule ambao unaviweka vyakula katika mafungu manne. Kundi la kwanza ni maziwa na vyakula vinavyotengenezwa kutokana na maziwa. Kwa mfano, maziwa ya maji, maziwa ya mgando (mtindi), maziwa ya unga, cheese, Ice Cream za maziwa, n.k. Kundi hili la vyakula linatupa virutubisho ambavyo huuwezesha mwili kukua, kujikarabati (repair), kuimarisha mifupa na meno. Pia huwezesha misuli (muscles) na mishipa ya fahamu kufanya kazi vizuri na vile vile huwezesha mwili kuweza kupata nguvu na joto. Zaidi ya hayo, maziwa hutoa virutubisho ambavyo huwezesha damu kuganda (kutokana) kama mtu atakuwa amejikata. Kwa faida hizi ni wazi kuwa maziwa ni kundi muhimu la vyakula. Kwa hiyo, kundi hili lazima liwe moja ya vyakula vyetu japo mara mbili kwa wiki kama tutashindwa kila siku kunywa maziwa au kula chakula chenye maziwa. Kundi la pili ni nyama na vyakula vinavyotokana na wanyama. Kwa mfano nyama, samaki, kuku, mayai, n.k. Pia vyakula vinavyotokana na mimea kama vile maharage, karanga, kunde, choroko n.k. navyo huwekwa katika kundi la nyama. Vyakula katika kundi hili la pili huitwa vyakula vinavyojenga mwili. Vile vile vyakula hivyo hutoa nguvu na joto mwilini, na zinavitamini ambayo husaidia kulinda mwili usipate maradhi mbalimbali. Tukizingatia faida za hapo juu, ni muhimu kila mtu ajitahidi kula vyakula hivyo japo mara tatu kwa wiki kama haiwezekani kila siku. Kundi la tatu ni vyakula vya matunda na mboga za majani. Mboga za majani na matunda hutoa virutubisho ambavyo husaidia kulinda mwili, kuwezesha mwili kufanya kazi vizuri. Pia mboga za majani na matunda husaidia tumbo kuweza kusaga chakula vizuri. Kwa hiyo, kila mtu ajitahidi kula matunda na mboga za majani kila siku. Kundi la nne ni vyakula vya nafaka, mfano wa vyakula hivyo ni kama vile
ngano, mchele, mahindi n.k. Vyakula hivyo huupa mwili nguvu na joto. Kila
binadamu mwili wake unahitaji nguvu na joto vinginevyo hakutakuwa na uhai.
Kwa hiyo, kila mtu ajitahidi kula vyakula vya nafaka milo mitatu au zaidi
kila siku. Hata hivyo, watu wanene hawatakiwi kula kiasi kikubwa cha vyakula
hivyo (vya nafaka).
|
YALIYOMO
Tahari
Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel Sheikh awasambaratisha walevi Liwale Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa Njaa hakuna, tunategemea kula silaha Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa
Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa Waislamu Msonge waomba wanusuriwe Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|