AN-NUUR 
Na.185 Shawwal 1419, Januari 29 - Februari 4 , 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Afariki baada ya kutokwa damu nyingi

Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 
 

BIBI Consolata Makene (Hamida) alifariki dunia Januari 16, 1999 mnamo saa 1.00 jioni baada ya kujifungua katika Hospitali ya Mount Meru ya mjini Arusha kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uzembe wa Daktari na wauguzi wa zamu. 

Kwa mujibu wa barua ya mume wa marehemu Bw. Abubakar Ally aliyoiandikia Wizara ya Afya, marehemu alianza kuumwa uchungu asubuhi siku hiyo na baada ya kufikishwa Hospitali ya Levolosi, Daktari aligundua hakukua na mapigo ya moyo ya mtoto hivyo alihamishiwa Hospitali ya Mount Meru kwa uangalizi zaidi. 

Alifika Hospitalini hapo saa 4.30 asubuhi. Baada ya Daktari kumpima, jibu lilikuwa ni lile lile kuwa mapigo ya 

mtoto yalikuwa hayasikiki na tayari ilikuwa ni ishara ya hali ya hatari. 

Tofauti na matarajio ya wengi, marehemu Consolata alidaiwa shilingi 4,000 na kwa vile hazikuwa karibu, alitekelezwa hadi alipojifungua katika kitanda alicholalia mnamo saa 9.00 mchana mtoto asiye riziki. 

Kama vile haitoshi, aliendelea kutokwa na damu nyingi ya uzazi hadi saa 12 jioni wakati wauguzi walipozindukana na kuanza kutafuta mishipa ya kuchomekeza sindano lakini wapi ni tayari walishachelewa. 

Mume wa marehemu Bw. Abubakar anaeleza kuwa alipoingia wodini alimkuta mkewe akiwa amelowa damu mwili mzima na kuelezwa kwamba wauguzi walimwambia shauri yake kwa kuwa hajatoa chochote na hajalipia gharama ya shilingi 4,000. 

Bw. Abubakar anadai kuwa kuona hivyo alimfuata nesi ili kujua matatizo ya mkewe na msaada gani unahitajika. Hata hivyo anadai kwamba aliambulia kufokewa. 

Hata hivyo, anasema kwamba baadae nesi huyo aliagiza maji na sindano na kuanza kumtoboa toboa mgonjwa akijaribu kumwekea maji. Lakini alikuwa amechelewa kwani mishipa ilikuwa haipatikani. 

"Alimtoboa toboa mpaka nikaona mke wangu sasa kageuza macho tayari anaingiliwa na mauti nilishindwa kuvumilia nililia na kutoka nje", alieleza kwa masikitiko Bw. Abubakar. 

Baada ya mazishi yaliofanyika Januari 18, mwaka huu siku ya Jumatatu Bw. Abubakar alimwarifu Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Ole King’ori kuhusiana na tukio hilo, lakini Dk. Ole alimwambia arudi Januari 21, mwaka huu. 

Na aliporudi akifuatana na dada wa marehemu Bibi Meristella Bonzo na jamaa zake wawili Daktari alikiri kufanyika uzembe na akaahidi kutoa ripoti kamili baada ya siku 28 baada ya muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo kurudi toka likizo. 

Miaka minne iliyopita, ulifanyika uzembe wa aina hiyo na mama mmoja kupoteza maisha japo mtoto alinusurika, lakini Daktari aliyekuwa zamu pamoja na wauguzi waliwajibika. 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Kama hakuna haki watu watachukua sheria mkononi 

Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa 

Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 

Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa 

Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel 

Sheikh awasambaratisha walevi Liwale 

Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha 

Mjue Usama bin Ladin -2 

Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa 

Njaa hakuna, tunategemea kula silaha 

Parole kwa mbinde! 

Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil 

Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha 

Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR 

I.P.C yatakiwa kujitangaza 

Kutoka magazeti ya zamani 

Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa 
Na Muhibu Said 

Waislamu wachoma moto nguruwe 

Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa 

Waislamu Msonge waomba wanusuriwe 

Sayansi na Teknolojia 
[PELEKA FAX NCHI ZA NG’AMBO BURE! – (2)] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na Lishe 
[Mwongozo wa mlo wa kila siku] 
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita