|
|
|
Upinzani dhidi ya Serikali ya Kiislamu wakati wa Khalifa wa Pili Umar Bin Khatab Mfalme wa Persia alikimbilia Hulwan ambako alijiandaa tena kukutana na Waislamu. Jeshi la adui liliongozwa na Kharzad ndugu wa Rustam ambae ndie aliyekuwa mkuu wa majeshi. Na Hashim na Qaqas waliongoza jeshi la Waumini. Vita hivi vilivyopiganiwa Jahula na kujulikana kwa jina la vita vya Jahula, viliwapa ushindi Waislamu na Wapeshia wakakimbilia kaskazini. Waislamu walisonga mbele na kuteka Qaka Hulwan, Nihawand, Hamdan, Azerbaijan na Armenia. Vita ndani ya Persia vilikwisha mwaka 21 A.H. na Himaya yote ya Persia ikawa chini ya Dola ya Kiislamu. Wapeshia walilazimika kuingia katika mkataba wa amani na Waislamu lakini ukadumu kwa miezi michache na Waajemi wakauvunja mwaka 638 A.D. Hii ikapelekea vita kubwa kupiganwa mwaka 642 huko Nihawand na Wapeshia wakashindwa kabisa. Upinzani wa Wapeshia uliishia hapa. Upinzani kutoka kwa Warumi Sababu za uchokozi wa Warumi dhidi ya dola ya Kiislamu zimeshaelezwa hivyo katika Ukhalifa wa umar kilichotokea ni maendelezo ya uhasama uliokwisha anaza wakati wa mtume (s.a.w.). Habari za ushindi wa Waislamu katika vita vya Ajnadayn dhidi ya Warumi mpakani mwa Syria na Dola ya Kiislamu zilimkuta Abubakr akiwa katika kitanda cha mauti. baada ya ushindi huu Khalid aliteka miji ya Damascus, Ardan na hims na kuiunganisha na Dola ya Kiislamu. Kutekwa kwa miji hii, kulimkasirisha sana hericlius na akaandaa jeshi kubwa ili kuwafukuza Waislamu kutoka Syria. Waislamu walikusanyika Yarmuk - mpaka wakati huu kamanda wa majeshi ya Kiislamu alikuwa Khalid bin Walid. Lakini baadae alipata barua kutoka kwa Khalifa umar kuwa asiendelee kuwa mkuu wa majeshi ya Kiislamu. Khalid hakuvunjika moyo aliendelea kupigana kwa juhudi kubwa. Jeshi la Warumi lashindwa Vita vya Yarmuk Kukusanyika kwa Waislamu Yarmuk kulimaanisha waachie sehemu walizoziteka awali kwa kuwa waliziacha na walirudisha Jizya kwa watu wanaohusika kwa vile hawakuweza kuwalinda tena. Hatimae majeshi ya mfalme wa Urumi Heraclius yakiwa na wapiganjai 240,000, 72 yaliwasili Yarmuk na mapigano makali yenye hasara kubwa upande wa adui yaliendelea. Askari wa Mwenyezi Mungu wanakadiriwa kufikia 30,000.73 Theodorus kamanda wa jeshi la Warumi aliuawa na jeshi lake likakimbia kwa khofu. Karibu Warumi laki moja waliuawa na Waislamu elfu tatu waliuawa. Vita vya Yarmuk vilivyopiganwa Rajabu 15 A.H. sawa na 636 A.D. viliwafikisha Warumi njia panda. syria iliwatoka moja kwa moja kutokana na kushindwa kwao na kuwa mikononi mwa Waislamu. Mfalme heraclius alikimbilia constantinople kutoka Antioch. Mkataba wa Jerusalem Baada ya kushinda katika vita vya Yarmuk makamanda wa Waislamu Amr bin al-As, Abu Ubaidah na Khalid bin Walid waliamua kukamilisha ushindi wao kwa kuizingira Jerusalem mji mtakatifu. Bishop wa Jerusalem na watu wake kwa kuzingatia kushindwa kwa Warumi katika vita kadhaa waliamua kutopigana na Waislamu bali kuiacha Jerusalem iwe chini ya Dola ya Kiislamu kwa sharti kuwa mkataba utiwe sahihi na Khalifa mwenyewe na yeye ndie akabidhiwe mji. Ujumbe ulimfikia Khalifa Umar Faruq ambae baada ya kushauriana na shura yake mji wa Madina akauacha chini ya uangalizi wa Ali Ibn Khatab naye akaenda Jerusalem. Umar alienda yeye binafsi na mfanyakazi mmoja tu walichukua ngamia mmoja ambae kila mmoja limpanda kwa zamu. Umar alipokuwa anaingia Jerusalem ilikuwa zamu ya mtumishi wake kwa kuwa ilikuwa haki ya mtumishi wa Khalifa wa Dola kubwa ile ya Kiislamu hakufanya udhalimu wa kutaka kuchukua nafasi ya mfanyakazi wake, ingawa yule mtumishi alikuwa tayari kumpisha. Lakini kwa upande mwingine nae mtumishi alifahamu haki zake, kwa kutambua haki yake hakujisikia vibaya kupanda ngamia wakati muajiri wake, kiongozi mkuu wa dola anatembea kwa miguu. Jambo lingine la msingi hapa ni kuwa Khalifa hakuchukua msururu wa watu kumsindikiza. Vile vile Khalifa hakujifaharisha kwa mavazi, lakini alivaa nguo za halali yake ambazo zilikuwa na viraka. Huu ndio uongozi katika Uislamu. Kiongozi si bwana lakini ni mtumishi wa watu. kwa mwenendo huo huo, usio na mikogo Khalifa aliwashangaa na kuwakasirikia makamanda wake, waliokwenda kumpokea wakiwemo abu ubaidah, Khalid na wengine wakiwa katika mavazi ya gharama waliyoyavaa na akawaambia. Njia pekee ya kufaulu ni kufuata mwenendo wa Mtume (s.a.w.). Makamanda hawa walimpokea Khalifa wao mahali paitwapo Jabiya, mahali ambapo mkataba uliandaliwa. Mkataba huu unaojulikana kwa jina la Mkataba wa Jerusalemu unasema hivi: Hii ni hifadhi ambayo mtumishi wa Allah, Umar Kamanda wa waumini amewapatia watu wa Ailiya. hifadhi hii ni ya maisha na mali, makanisa na misalaba, wagonjwa na wazima na kwa wafuasi wao wote. Makanisa yao hayatatumika kwa makazi wala hayatavunjwa, wala hayataharibiwa wala viwanja vinavyoyazunguka, wala misalaba yao, wala mali za makanisa hayo hazitaguswa. Wakazi wa Ailiya hawatalazimishwa katika maswala ya Dini, wala hakuna mtu atakaepata usumbufu wowote kwa ajili ya Dini. Wayahudi hawataishi Ailiya.Watu wa Ailiya watalipa Jizya kama wakazi wa miji mingine na kuwaondoa Warumi. Uhai na mali ya Warumi wanaohama itakuwa salama mpaka atapofika sehemu ya usalama, lakini Mrumi ataamua kuishi Ailiya atakuwa salama na atalipa Jizya. Kama mkazi wa Ailiya anataka kuhama na Warumi na kuchukua mali zao, wao wenyewe, makanisa yao na misalaba yao mali zao na wao watakuwa salama mpaka watapofika mahali pa usalama. Kila kilichoandikwa hapa ni ahadi ya Allah na jukumu la Mtume wake, makhalifa na waumini ilimradi wahusika wanalipwa Jizya.74 Mkataba wa Jurusalem vile vile uliwapa haki sawa Dhimmis na Waislamu. Kama Muislamu ataamua Dhimmis kosa hili litalipwa kwa uhai wake. Mali ya Dhimmis pia ilikuwa salama. Ardhi katika miji iliyotekwa ilibaki kwa wenyewe wa asili na Waislamu walizuiwa kuinunua. Kutoka Jabiya Umar aliendelea hadi Jerusalem na milango ya mji ikafunguliwa na Waislamu wakaingia Jerusalemu - mwaka wa 16 A.H. 635 A.C. Lakini wanahistoria wengine wanadai kuwa mkataba huu ulisainiwa mwaka wa 17 A.H. Umar aliukagua mji wa Jerusalem. Muda wa swala ulipofika Bishop aliwaruhusu
waswali kanisani, lakini Umar aliogopa kuswali humo kusije kuwa hoja ya
kuchukua kanisa hilo, hivyo aliswalia nje kwenye ngazi. Hata hapo aliacha
maandishi yanayokataza kuchukua sehemu hiyo.
|
YALIYOMO
Tahariri Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|