AN-NUUR 
Na.182 Ramadhan 1419, Januari 1 - 7, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897)

"KATIKA giza nene lililotanda na kufunika ummah wa Kiislamu ilitoka sauti katika nchi ya Afghanistan inaita njoo katika kheri. Sauti hiyo ilisikika kila upande, hakika sauti hiyo ilikuwa ni Jamaldin Afghan muasisi wa ummah huu kuelekea katika maendeleo mapya ya siku mpya". 

Haya ni maneno toka kwa mwanaharakati mkubwa wa Tunisia Malik bin Nabiy akimuelezea Jamaldin Afghan katika urathi na utamaduni wa dola yetu kuu ya Kiislamu ambayo kwa upande wa Asia ilianzia China Magharibi, India, Jamhuri za Urusi, Turmanistan, Harzabajan, Tajikistan, Kirikistan, Daghastan, Chechnya. 

Upande wa Afrika Magharibi na Kaskazini na upande wa Ulaya ni Uturuki, Yugoslavia, Ugiriki, Markodonia, Albania na kuishia Spain. Dola hii kubwa ya Kiislamu ilikuwa chini ya Khalifa mmoja bila kutambua mpaka wala ubaguzi wa rangi, ummah huu wa Kiislamu ulihitaji mwanamapinduzi na mwanafikra wa Kiislamu katika utamaduni, siasa, uchumi na maendeleo kwa ujumla. Mwanamapinduzi huyo hakuwa mwingine bali ni Jamaldin Afghan aliyezaliwa mwaka 1838 na kufa mwaka 1897. 

Sheikh Imam Muhammad Abduh ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kutegemewa wa Jamaldin Afghan ameandika makala haya walipokuwa wote Ufaransa mwaka 1883 - 1885, Sheikh Muhammad Abduh Mmisri ndiye Sheikh aliyemfundisha Hassan el-Banna muasisi wa Ikhwan (Muslim Brothehood). 

Kwa ujumla Maulana Sayyid Jamaldin Afghan alizaliwa katika kijiji cha Kandri kilichopo pembezoni mwa mji wa Kabul, Afghanistan, alikulia katika mtaa wa As’ad Abad, ametokana na familia za Maulamaa wa Afghanistan walioshi katika zama za utawala wa Dust Muhammad Khan 1826 - 1862.  

Alianza kusoma nyumbani kwa baba yake na alipofikia miaka kumi alikuwa tayari amekwishahifadhi Qur’an yote kichwani na kujifunza misingi ya lugha ya Kiarabu. Katika mwaka 1848 alijiunga na chuo cha Karziwin amabcho baba yake alikuwa akifundisha, alikaa miaka miwili kisha yeye na baba yake wakahamia Tehran mwishoni mwa mwaka 1849. 

Mwaka huo huo wakasafiri na baba yake kuelekea Irak katika mji wa Najaf ambako waliishi miaka minne akisoma na kujifunza elimu ya Hadith, falsafa, Mantik, Usul pamoja na elimu ya upasuaji. Kutokana na kipaji chake, kulizuka fitna kwa wanafunzi wenzake waliokuwa na khiyana kwa nini yeye awazidi katika kila fani jambo lililopelekea kutaka kuuawa mwaka 1854. 

Mwishoni ikambidi aukimbie mji wa Najaf na kuelekea Bombay nchini India na kuishi kwa miezi michache Bombay kisha alielekea mji wa Karkit ambapo alijifunza elimu nyingine zaidi, katika mwaka 1857 akaelekea Makkah kwa ajili ya ibada ya Hijja. 

Akarejea Afghanistan ambako ni kitovu cha harakati zake kwa mara ya kwanza akaingia kwenye mapambano na wakoloni wa Kiingereza akishirikiana na rafiki yake Amir Muhammad Aghdham Khan dhidi ya mpinzani wao kibaraka wa Uingereza Dust Muhammad Khan mwaka 1862 wakaweza kumshinda na yeye (Jamaldin) akapewa cheo cha Uwaziri Mkuu. 

Mwaka 1868 Shir Ally Khan akisaidiwa na wakoloni wa Kiingereza aliuteka mji wa Kabul. Rafiki yake Muhammad Aghdham alitorokea nje ya nchi na yeye kuwekwa kizuizini nyumbani kwake. Mwaka huo huo mamlaka ya Kiingereza ulimuamishia India. Akiwa nchini India alikutana na Maulamaa na Masheikh mbalimbali na kuanzisha harakati dhidi ya Uingereza na vibaraka wake, baada ya wakoloni wa Kiingereza kuhojiwa maslahi yao wakamteka usiku nyumbani kwake walimkuta akiswali sala ya Tahajud wakamfunga kitambaa usoni na kumsafirisha hadi Misri ambapo alikaa kwa muda. 

Katika muda mchache alipokuwa Misri aliweza kukutana na Masheikh na wanafunzi wa Al-Azhar na kuwapa nasaha mbalimbali dhidi ya maadui wa Uislamu, kutokana na hayo alipendwa sana baada ya hapo akaondoka kuelekea Istambul Uturuki akapokelewa na Sultan Abdul Aziz Muhammad, kiongozi wa Dollat Uthmaniya (Othman Empire) huko alipata fursa ya kujifunza lugha ya Kituruki kwa miezi sita aliweza kuijua vizuri lugha hiyo, baada ya hapo akachaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu la elimu na yeye mwenyewe akawa anafundisha katika Misikiti na vyuo mbalimbali . 

Akaanza kutoa hutuba za mwamko kuhamasisha Waislamu akaweza kuunda kundi kubwa la wanaharakati toka vyuoni, serikalini pamoja na Masheikh kutokana na mwamko huo ummah ukamtaka Sultan Abdul Aziz Muhammad kufanya mabadiliko katika uongozi wake ili kuweka mfumo mzuri wa Dola ya Kiislamu. 

Ikazuka fujo iliyopelekea yeye kufukuzwa, ikamlazimu aondoke na kuelekea India kupitia Misri Machi 23, 1871 aliwasiri Cairo kwa mara ya pili ili kuelekea India. Misri alikutana na Riadh Basha ambaye alimuomba abaki kutokana na elimu na fikra zake ambazo zilihitajika Misri na kuahidiwa kulipwa mshahara wa Paundi kumi kila mwezi pamoja na nyumba ya kuishi bure. Kutokana na kuombwa sana ikambidi abaki, habari zilipoenea wanafunzi wa vyuo vikuu na Maulamaa wakawa wanamiminika nyumbani kwake.  

Muhammad Abduh anaelezea kumwambia mwalimu wa somo la mantiki na falsafa katika chuo cha Al-Azhar Sheikh Hassan Tuliliy kwamba amepata khabari za kuwasili kwa Ulamaa mkubwa toka Afghanistan anaishi katika mtaa Khan Haliliy, tukaondoka pamoja pamoja kwenda kumsalimia nyumbani kwake tukamkuta anakula na akatukaribisha, tukamwambia ahsante. 

Tulipokaa kwa muda akaanza kutuuliza falsafa za aya kadhaa, tulipokuwa tukizitolea maelezo akatukosoa na kutupa tafsiri sahihi na falsafa za aya hizo baada ya siku kadhaa kupita akafungua darsa nyumbani kwake na kuita Masheikh na Maulamaa toka chuo cha Al-Azhar ili kuwapa nasaha mbalimbali kuanzia mwaka 1871 mpaka mwaka 1879 alikuwa akitoa mihadhara mbalimbali ya mwamko wa Kiislamu na kuwatahadharisha Waislamu na fikra za Kimagharibi na kupinga ukoloni na unyonyaji. 

Ikapelekea kuanzishwa kwa chama cha siri cha ukombozi wa nchi mbiu yake kuu ilikuwa Misri ni ya Waislamu, hatutaki kuongozwa na siasa za nje zisizokuwa za Kiislamu. Chama hicho kilikuwa na wanachama toka vyuo, maulamaa, Masheikh, wafanyakazi wa serikali pamoja na wakulima alifanya mpango wa kuanzisha gazeti na kiwanda kidogo cha uchapaji na kuandika makala mbalimbali yeye mwenyeweakiandika makala na tahariri nzito za kusisimua kwa kutumia jina la bandia "Mudhirbin Wadhaa". 

Kiini cha makala hizo ilikuwa ni kuwachochea na kuwataka Waislamu kuungana pamoja kupambana na mabeberu waliokuwa wa kitaifa na wa kimataifa wanaoenea kwa kasi katika nchi za Waislamu. Akaanzisha gazeti jingine lililokuwa likiitwa "Tijarat (biashara) lililokuwa na malengo ya kutaka nchi za Kiislamu zisikubali uchumi wake kushikwa na watu wa Magharibi (wakoloni). 

Waliokuwa walikisimamia gazeti hilo ni wanafunzi wake Muhammad Abduh na Ibrahim Liqan gazeti hilo lilichapisha makala moja iliyopelekea Waziri Mkuu wa Uingereza kutoa tamko rasmi kupinga makala hiyo iliyokuwa inahatarisha maslahi ya Uingereza kwenye nchi za Kiislamu. 

Alianzisha gazeti lingine aliloliita "Mur’atu Shark" yaani (kioo cha masharik). Gazeti hilo lilikuwa na makala nyingi za kutaka nchi za Kiislamu kutogawa mipaka kwani mipaka ni sira za Kimagharibi. 

Sheikh Jamaldin Afghan alikusanya tabaka za watu tofauti katika jamii masikini, wazee, vijana na kina mama na kuwapa fikra sahihi na maongozo ya kujikomboa kwa misingi ya Uislamu. Chama cha ukombozi cha Misri ambacho kiliongozwa na Ahmad Arab, Muhammad Sammy Burudi na Abdul Salam Waslahi na Muhammad Abdul ambao wote ni wanafunzi wake walikuwa cheche za mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya wakoloni na kutaka Misri iongozwe kwa misingi ya Uislamu. 

Harakati hizi zilipelekea wakati wa mwezi wa Ramadhani tarehe 6, 1879 akiwa na wanafunzi wake Abuturab wakirejea nyumbani toka kwenye muhadhara wakakamatwa na polisi na kuwekwa rumande na siku iliyofuatia yeye pekee (Jamaldin) akasafirishwa kwa gari lililozibwa pande zote mpaka Canal Suez kupelekwa India bila umma wa Waislamu kutambua. 

Kwa mara nyingine nchini India akaanzisha harakati dhidi ya Mahindu ambao walikuwa wakisaidiwa na wakoloni kuwakandamiza Waislamu. Baada ya harakati kushamiri mjini Bombay, serikali ya kikoloni ya Kiingereza ilimuhamisha tena na kumpeleka mji wa Karkata ambako alizuiliwa kwa miaka kadhaa mpaka 1883 aliachiwa huru na akaondoka na kuelekea Ufaransa.  

Alipofika Ufaransa akaanzisha chama cha siri kilichoitwa Jamiatul-Urwal-Uthaq, chama cha Kiislamu kilichopinga ukoloni kwenye nchi za Kiislamu, akawa Mwenyekiti wa chama hicho na akaanzisha Jarida. 

Itaendelea toleo lijalo 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma

Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha

Matokeo ya Darasa la Saba yacheleweshwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi: Wananchi wahoji je, nchi hii ina dini moja tu?

Njaa yaikumba Kilwa

Dondoo za Saikolojia
Na. Abu Halima Sachangwa

Kona ya Wacha Mungu
Mavuno yangu yasiwe...

Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana huyoo!
Na Sompo wa Kahambwe

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897)

Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Imetayarishwa na Africa Muslims Agency

Marekani ni mtetezi au adui wa haki?: Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Na Abu Salim

Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Na Habiba Swedi, Arusha

Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an

Ijue  Madrasa Hudaa Arusha

Wazazi waaswa kutoshabikia maovu

Mzee maarufu afariki Moro

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? (jibu) 
Na Ally Said

Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani?

Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Na Habiba Swedi

Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar

Baada ya kuvunjiwa nyumba, kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Na Q. Mtaita

Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile

Sayansi na Teknolojia 
[Kuunganisha Kompyuta kwa Kutumia Modem

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Saumu na lishe ya mama anayenyonyesha] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita