|
|
|
Sifa njema anazistahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad, Jamaa na Sahaba wake wote. Baada ya hayo, haya ni mafunzo mafupi kuhusu saumu; hukumu yake, mafungu ya watu katika kufunga, mambo yanayofunguza na faida nyingine. Yote hayo yameelezwa kwa ufupi. 1. Kufunga ni kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa kuacha mambo yanayofunguza tokea kuchomoza alfajiri mpaka jua kuzama. 2. Kufunga Ramadhani ni mojawapo ya nguzo kubwa tano za Uislamu kwa mujibu wa kauli ya Mtume (S.A.W.) isemayo: "Umejengwa Uislamu juu ya mambo matano: (Moja) Kukiri moyoni na kutamka mdomoni kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu tu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na (Pili) Kusimamisha sala na (Tatu) Kutoa zaka na (Nne) Kufunga Ramadhani na (Tano) Kuhiji Nyumba Tukufu (Makkah)" MGAWANYIKO WA WATU KATIKA KUFUNGA 1. Kufunga ni wajibu kwa kila Mwislamu, aliye balehe, mwenye akili timamu, mwenye kuweza kufunga na mkaazi (sio msafiri). 2. Kafiri hafungi, na sio wajibu kwake kulipa iwapo atasilimu. 3. Mtoto mdogo ambaye hajabalehe sio wajibu kwake kufunga, ila anaamrishwa kufunga kusudi apate kuzoea. 4. Mwendawazimu sio wajibu kwake kufunga wala kutoa chakula badala ya kufunga ajapokuwa ni mtu mzima. Ni mfano wa mwendawazimu mtu mwenye akili taahira asiyeweza kupambanua, na pia mtu mzee (kikongwe) asiyeweza kupambanua. 5. Mtu asiyeweza kufunga kwa sababu ya kudumu kama mtu kikongwe na mgonjwa anayeugua ugonjwa usiotarajiwa kupona atatoa chakula kwa kila siku moja kumpa masikini. 6. Mgonjwa anayeugua maradhi ya ghafla na akawa anatarajia kupona ataacha kufunga iwapo funga inamuwia uzito, na atalipa baada ya kupona. 7. Mwanamke mjamzito na anayenyonyesha iwapo itawawia uzito kufunga kwa sababu ya mimba au kunyonyesha au wakihofu kuathirika watoto wao, wataacha kufunga na watalipa saumu itakapowawia wepesi na kuondokewa na hofu. 8.Mwanamke aliye katika hedhi na anayetokwa na damu ya uzazi (nifasi) hawafungi wakiwa katika hali hizo, na watazilipa siku zilizowapita. 9. Mtu mwenye kulazimika kutofunga kwa ajili ya kuokoa kiumbe kilichohifadhiwa1 Kiumbe kilichohifadhiwa ni viumbe vyote isipokuwa: 1. Muislamu asiyesali. 2. Kafiri asiyeingia mkataba wa amani na dola ya Kiislamu. 3. Muislamu ambaye ameacha Uislamu (Murtad). 4. Mzinifu aliyeoa au kuolewa. 5. Mbwa asiyetumika kwa shughuli za ulinzi. Kiumbe kilichohifadhiwa ni viumbe vyote isipokuwa: a)Kafiri asiyeingia mkataba wa amani na dola ya Kiislamu b) Mzinifu aliyeoa au kuolewa c)Mwislamu asiyesali d) Mwislamu aliyetoka katika Uislamu"murtadi" na d)Mbwa ambaye hatumiki kwa shughuli za ulinzi au uwindaji. kisizame majini au asiteketezwe na moto atafungua ili akiokoe kiumbe aliyepatwa na maafa, na atalipa 10. Msafiri akitaka atafunga na akitaka hatafunga, na atalipa siku ambazo hakufunga (akiwa safarini), ni sawa safari iwe ya dharura kama safari ya Umra au safari ya kudumu kama wenye magari ya kukodi (kama mabasi, teksi na magari ya mizigio). Wataacha kufunga wakitaka madamu wako nje ya miji yao. MAMBO YANAYOMFUNGUZA MWENYE KUFUNGA Mwenye kufunga hatakuwa amefungua iwapo atafanya lolote kati ya mambo yanayofunguza huku akiwa amesahau au asipojua (kuwa jambo hilo linafunguza) au akiwa ametezwa nguvu. Hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka: "Ewe Mola wetu usituadhibu tukisahau au tukikosea"1 kisizame majini au asiteketezwe na moto atafungua ili akiokoe kiumbe aliyepatwa na maafa, na atalipa 10. Msafiri akitaka atafunga na akitaka hatafunga, na atalipa siku ambazo hakufunga (akiwa safarini), ni sawa safari iwe ya dharura kama safari ya Umra au safari ya kudumu kama wenye magari ya kukodi (kama mabasi, teksi na magari ya mizigio). Wataacha kufunga wakitaka madamu wako nje ya miji yao. MAMBO YANAYOMFUNGUZA MWENYE KUFUNGA Mwenye kufunga hatakuwa amefungua iwapo atafanya lolote kati ya mambo yanayofunguza huku akiwa amesahau au asipojua (kuwa jambo hilo linafunguza) au akiwa ametezwa nguvu. Hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka: "Ewe Mola wetu usituadhibu tukisahau au tukikosea"2. Na kauli yake Mwenyezi Mungu: "...isipokuwa yule aliyetezwa nguvu (aliyelazimishwa) na hali ya kuwa moyo wake umetulizana katika imani".3 Na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na hakuna kwenu dhambi katika yale mliyoyafanya kwa makosa na lakini (dhambi zipo) katika yale ambayo nyoyo zenu zimekusudia".4 Mwenye kufunga anaposahau akala au akanywa haikuharibika saumu yake, kwa sababu amesahau. Lau kama mwenye kufunga amekula au amekunywa akiamini kuwa jua limekuchwa au kwamba alfajiri haijachomoza haikuharibika saumu yake, kwa sababu huo sio utashi wake. Mambo yanayofunguza ni manane nayo ni: {1} Kuingiliana mke na mume kimwili. Tendo hili likitokea katika mchana wa Ramadhani kwa mtu ambaye ni wajibu kwake kufunga itampasa, pamoja na kulipa, kutoa kafara nzito. Kafara nzito ni kumwacha huru mtumwa. Asipopata mtumwa ni kufunga miezi miwili mfululizo. Asipoweza kufunga awape chakula masikini sitini. {2} Kujitoa manii wakati wa umacho (sio usingizini) kwa kujichezea au kwa kugusana au kwa kubusu au kwa kukumbatiana au kwa mfano wa hayo. {3} Kula au kunywa. Ni sawa kilicholiwa au kunywewa kina manufaa au kina madhara kama vile sigara. {4} Sindano zinazotumika kama chakula na ambazo hutosheka kwazo na chakula . Hii ni kwa sababu sindano hizo ni sawa na kula au kunywa. Ama sindano ambazo hazitumiki kama chakula hazifunguzi. Ni sawa mwenye kufunga alizitumia sindano hizo katika misuli au katika mishipa, na ni sawa amepata ladha ya sindano hizo katika koo lake au hakupata. {5} Sindano za kuongezea damu, kama vile mwenye kufunga ikimtokea kutokwa na damu, hivyo akadungwa sindano ya kumuongezea damu badala ya ile iliyomtoka. {6} Kutokwa na damu ya Hedhi na ya uzazi (Nifasi). {7} Kutoa damu kwa kuumika na mfano wake. Ama damu ikitoka yenyewe kama mwina (ugonjwa wa kutokwa na damu puani) au damu ikitoka kwa kung’oa jino haifunguzi, kwa sababu huko sio kuumika wala sio katika maana ya kuumika. {8} Kutapika, iwapo mwenye kufunga atakusudia. Ama akitapika bila ya kukusudia hatakuwa amefungua. FAIDA Inafaa kwa mwenye kutaka kufunga kunuia saumu huku akiwa na Janaba, halafu ataoga baada ya kuchomoza alfajiri. Mwanamke ikiwa atatoharika katika mwezi wa Ramadhani kutokana na Hedhi na Nifasi kabla ya alfajiri ni wajibu kwake kufunga hata kama hataoga ila baada ya kuchomoza alfajiri. Inafaa kwa aliyefunga kung’oa jino lake, kutibu jeraha lake (kidonda) na kuweka dawa ya matone katika macho au masikio yake. Hatakuwa amefungua kwa kufanya hayo hata kama atahisi ladha ya matone ya dawa katika koo lake. Inafaa kwa mwenye kufunga kupiga mswaki mwanzo wa mchana na mwisho wake.Hiyo ni sunna katika haki yake kama ilivyo sunna kwa wasiofunga. Inafaa kwa mfungaji kufanya mambo yanayo mpunguzia makali ya joto na kiu, kama kujipoza kwa maji (kama kuoga) na kipoza hewa (air condition). Inafaa kwa mfungaji kuweka katika mdomo wake kitu kitakacho mpunguzia shida ya kupumua kunakotokana na shinikizo la damu (BP) au mfano wake. Inafaa kwa mfungaji kuitia maji midomo yake iwapo imekauka na pia kusukutua iwapo mdomo wake umekauka lakini bila ya kufikisha maji kooni. Ni sunna kwa mfungaji: a) kuchelewesha kula daku mpaka nyuma kidogo ya alfajiri b) kufanya haraka kufungua baada ya jua kuchwa na c) kufungua kwa tende tosa. Asipopata tende tosa afungue kwa tende mbivu. Asipopata tende mbivu afungue kwa maji. Asipopata maji afungue kwa chakula chochote halali . Asipopata chakula atanuia kufungua katika moyo wake mpaka atakapopata cha kufungulia. Ni sunna kwa mfungaji kutenda ibada kwa wingi na kujiepusha na mambo yote yaliyokatazwa. Ni wajibu kwa kila mfungaji kudumu katika kutenda yaliyo wajibu na kujiepusha na mambo yaliyo haramu. Anatakiwa asali sala tano katika nyakati zake na kwa Jamaa ikiwa mfungaji ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kusali Jamaa. Aache kusema uongo, kusengenya, kughushi, kujihusisha na masuala ya biashara za riba na kila kauli au kitendo kilichoharamishwa. Amesema Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani kwamba: "Yeyote ambaye hakuacha maneno ya uzushi na kuutumia uzushi na mambo ya kijinga (kipuuzi) basi Mwenyezi Mungu hana haja kwa mtu huyo katika kuacha kwake kula na kunywa". ZAKAATUL-FITRI Zakaatul-fitri ni pishi moja ya chakula (Takriban kilo mbili na nusu =2500gm), mchele au ngano au tende au chakula kingine ambacho watu wanakula. Haitoshelezi Zakaatul-fitri kutoa pesa na nguo isipokuwa chakula tu. Zakaatul-fitri hutolewa asubuhi ya siku ya Idd kabla ya kusali sala ya Idd, na inatosha kuitoa kabla ya siku ya Idd kwa siku moja au siku mbili. Haifai kuahirisha na kuitoa Zakaatul-fitri baada ya sala ya Idd isipokuwa kwa udhuru tu. Zakaatul-fitri hutolewa kumtolea mtoto mdogo, mtu mzima, mwanamume na mwanamke katika Waislamu. SALA YA IDD HUKUMU YAKE Sala ya Idd ni sunna iliyosisitizwa. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa sala ya Idd ni wajibu kwa sababu zifuatazo: 1. Mwenyezi Mungu ameamrisha kuisali sala ya Idd. "Basi sali kwa ajili ya Mola wako na chinja (kwa ajili ya Mola wako)".5 2. Mtume (S.A.W.) daima alikuwa akisali sala ya Idd. WAKATI WAKE Wakati wake unaanza tangu kuchomoza jua na kupanda kiasi cha mkuki (kama mita 3) mpaka kabla ya jua kupinduka (kutoka usawa wa katikati ya dunia kuelekea magharibi). Kusali mapema ni bora zaidi hasa katika sala ya Idd Al- Adh’haa (Idd El- Hajj) ili kuwe na wakati wa kutosha kwa anayetaka kuchinja. MAHALI PAKE Jambo lililo bora zaidi ni kuwa sala ya Idd isaliwe katika uwanja ikiwezekana, kwa kuwa Mtume (S.A.W.) alifanya hivyo na pia Sahaba wake waongofu walifanya hivyo. HAKUNA ADHANA WALA IQAMA Imepokewa kutoka kwa Ibn-Abbaas kwamba Mtume (S.A.W.) alisali sala za Idd mbili (Idd El-Fitri na Idd El-Hajj) bila ya Adhana wala Iqama. NAMNA YAKE Sala ya Idd ni rakaa mbili. Amesema Omar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba: "Sala ya Idd ni rakaa mbili, ikiwa ni sala kamili isiyopunguzwa (yakiwa ni mafunzo yaliyotoka) juu ya ulimi wa Mtume wenu na hakika amehasirika aliyeleta uzushi". Katika rakaa ya kwanza ataleta Takbira saba ukitoa Takbira ya kuanzia sala, na katika rakaa ya pili ataleta Takbira tano. Imepokewa kutoka kwa Aisha (mke wa Mtume S.A.W.), Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) katika sala ya Idd El-Fitri na Idd El-Hajj alileta Takbira saba na tano ukitoa Takbira ya kuanzia sala ya Idd. Katika rakaa mbili hizo atasoma sura Al-Aalaa (87) na sura Al- Ghaashiyah (88) kama ilivyo katika Hadithi ya Nuuman bin Bashiir aliyoipokea Imam Muslim au atasoma sura Qaaf (50) na sura Al-Qamar (54) kama ilivyo katika hadithi ya Abi -Waaqid Al-Laythiy ambayo pia ameipokea Imam Muslim. HOTUBA Hotuba inakuwa baada ya sala. Amesema Ibn-Abbas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba: "Nilishuhudia (nilihudhuria) Idd pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.), Abu-Bakari, Omar na Othman, Mwenyezi Mungu awawiye radhi, na wote walikuwa wakisali kabla ya hotuba".6 MAMBO YALIYO SUNNA SIKU YA IDD Kuoga. Imepokewa kutoka kwa Aliy bin Abi-Twalib, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba aliulizwa kuhusu kuoga akasema kuwa: Ni siku ya Ijumaa, siku ya Arafah, siku ya Idd El-Fitri na siku ya Idd El-adh’haa" 2. Kuvaa nguo nzuri sana. Amesema Ibn Abbass kuwa: Mtume (S.A.W.) alikuwa akivaa kashida (shali) nyekundu siku ya Idd. 3. Kula siku ya Idd El-Fitri kabla ya kutoka kwenda kusali. Imepokelewa kutoka kwa Anas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, akisema kwamba: Mtume (S.A.W.) Alikuwa hatoki (kwenda kusali) siku ya Idd El-Fitri mpaka ale tende. 4. Kuchelewesha kula siku ya Idd El-Adh’haa mpaka ale katika Udh-hiyah (mnyama) wake (atakayemchinja). Hiyo ni kwa mujibu wa Hadithi ya Abu-Dharr isemayo kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) alikuwa hatoki (kwenda kusali) siku Idd El-Fitri mpaka ale na alikuwa hali siku ya Idd El-Adh’ haa mpaka achinje. 5. Kubadilisha njia. Amesema Jabir, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba: Alikuwa Mtume (S.A.W.) ifikapo siku ya Idd anabadilisha njia 7 (kwa maana kwamba anaporudi kusali hupita njia nyingine na sio ile njia aliyopita wakati wa kwenda). 6. Kuleta Takbira. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na ili mkamilishe hisabu (ya siku mlizoacha kufunga kwa udhuru) na ili mumtukuze Mwenyezi Mungu (kwa Takbira) kwa vile amekuongozeni"8 Na amesema Mwenyezi Mungu:"Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohisabika (siku tatu baada ya Idd El- Haj)" 9 WAKATI WA TAKBIRAH a) Katika Idd El-Fitri wakati wa Takbira unaanza tangu kuonekana kwa mwezi wa Mfungo Mosi au kukamilika hisabu ya siku za mwezi wa Ramadhani mpaka kuanza hotuba ya Idd. b) Katika Idd El-Adh’ haa wakati wa Takbira unaanza tangu asubuhi ya
siku ya Arafah (tarehe 9 mfungo Tatu) mpaka mwisho wa siku za Tashriiq
(tarehe 13 mfungo Tatu). Hayo yamesihi kunukuliwa kutoka kwa Aliy bin Abi-Twalib,
Ibn-Abbas na Ibn-Masoud Mwenyezi Mungu awawiye radhi wote.
|
YALIYOMO
Tahariri Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|