|
|
| TAHARIRI
Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Dk. Omar, serikali
ipi tukae nayo?
ALIPOKUWA anatembelea Jiji la Dar es Salaam na kukutana na watendaji wa Serikali za Mitaa, Waziri Mh. Kingunge Ngombale Mwiru aliripotiwa na vyombo vya habari akiwakosoa viongozi wanaoigombanisha Serikali na wananchi. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mh. Kingunge alisema kwamba wapo baadhi ya viongozi/watendaji ambao hutumia madaraka yao vibaya bila kuwajali wananchi na kutokana na utendaji wao huo mbaya, hupelekea wananchi kujenga hisia kwamba serikali yao inawaonea, haiwajali na inawanyanyasa. Mantiki ya maelezo haya ya Mh. Kingunge ni kujenga hoja kwamba serikali yenyewe haina tatizo na wananchi wake na kwamba matendo ya baadhi ya viongozi yasifanye kwamba ndio msimamo wa serikali. Au tuseme isidhaniwe kwamba kiongozi anapowatendea vibaya wananchi kaagizwa na serikali. Wananchi wanaitegemea serikali na serikali inawategemea wananchi. Aidha, ili nchi ijitegemee; idumu katika amani na utulivu na kuwa na mazingira mazuri ya kupiga hatua katika maendeleo; ni lazima pawe na mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi. Serikali iwaheshimu, iwajali, iwatendee haki na isimamie mambo yao wananchi kwa uadilifu. Kwa upande mwingine wananchi nao waiheshimu na kuitii serikali kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Kila sehemu inapotekeleza wajibu wake ndipo maelewano yanapokuweko. Serikali yoyote iliyo makini na ambayo haina agenda ya siri (kinyume na yale yatamkwayo hadharani) dhidi ya baadhi ya raia wake itakuwa macho kuhakikisha kwamba watendaji wake hawaichonganishi na wananchi. Na pale ambapo kiongozi ama kwa makusudi, kwa uzembe na hata kwa bahati mbaya; utendaji wake utajenga taswira ya wananchi kuhisi wanaonewa, kunyanyaswa na kudhulumiwa na serikali, basi hatua za haraka na za wazi huchukuliwa dhidi ya kiongozi huyo. Ili serikali kujikosha na kufuta hisia hizo hatua zinazochukuliwa huwa za wazi na wala sio kimya kimya. Sikwambii kufumba macho na kupiga kimya. Iwapo itatokea baadhi ya watendaji wa serikali kuwahujumu wananchi na wananchi hao wakailalamikia serikali na isichukue hatua yoyote. Je, hili nalo alaumiwe nani? Hata kama haikuwa agizo la serikali, wananchi watalazimika kuamini kwamba wanayotendewa ama ni maagizo ya serikali au inafurahia wao kuhujumiwa. Wapo wananchi hapa wameuliwa na wengine kunyanyaswa na kudhalilishwa. Wananchi wanachodai ni kwamba Katiba na sheria za nchi na hata zile za kimataifa zitumike kulihukumia jambo hili. Serikali haitaki na badala yake inawalinda wahusika. Mh. Kingunge pamoja na heshima zote, je, tuamini kwamba yule aliyetoa amri "piga yule", "mwongeze" na yule aliyetekeleza hawakutumwa na serikali bali wamefanya vile ili kumchonganisha Mh. Rais pamoja na serikali yake na wananchi! Nini hukumu ya mtu anayeleta fitna kubwa kama hii kati ya serikali na wananchi. Labda katika mfano huu huu Mh. Makamu wa Rais Dk. Omar Ali Juma majuzi naye kawahimiza Waislamu wakutane na serikali kutatua matatizo yaliyopo kuliko kuisema serikali pembeni. Lakini hayo mazingira yenyewe si yawepo? Kwa mtu kama Padri Lwambano ambaye akisema "Yesu anatukanwa" serikali yote hugwaya, Mkuu wa Mkoa akaenda mbio na vyombo vya usalama vikaingia kazini sio kuchunguza ukweli wa madai ya Lwambano, lakini kuwatia adabu wanaodaiwa kutukana! Kwa mtu kama Paroko Lwambano ambapo chama cha CCM chini ya Mwenyekiti wake wa Taifa kadhalika Bunge la Jamhuri; vilipongeza kazi iliyofanywa na polisi kufuatia kauli yake bila ya kuhoji kwanza usahihi na ukweli wa madai yake Paroko huyu hahitaji kuhimizwa kwamba akiwa na tatizo asilalamike pembeni bali aione serikali. Lakini vipi yule aliyepigwa risasi katika harakati za polisi kuyafanyia kazi madai ya Paroko; kwanza akaachwa bila ya matibabu akapooza, pili akafungwa pingu kitandani hadi mwili ukakaribia kuoza kwa madonda, tatu akasingiziwa na Waziri wa serikali Bungeni kwamba yote hayo yamemkuta kwa sababu ya kuwa na makaratasi ya uchochezi, nne Bunge lisitake kujua ni makaratasi ya uchochezi gani huo unaohalalisha mtu kupigwa risasi bila hata ya kufikishwa mahakamani. Je, mazingira haya ambayo serikali ishajijengea ni ya kukaribisha kweli mazungumzo kati ya serikali na Waislamu! Lipi hapa la kuwafanya Waislamu waone kwamba haya yote yanafanywa ili kuwachonganisha na serikali na wala sio serikali yenyewe inayowaonea na kuwadhulumu! Itakuwa ni kuifanyia kejeli na kuivunjia heshima sera ya Rais wetu Mh. Mkapa ya Uadilifu, Ukweli na Uwazi kama lawama zitaelekezwa kwa baadhi |
YALIYOMO
Tahariri Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|