|
|
|
Miaka ya nyuma mpaka kufikia mwishoni mwa miaka ya sitini, baadhi ya makabila hapa nchini yalijijengea utamaduni wa kutoa mafunzo ya kitabia kwa vijana waliofikia balegh, chini ya hapo kidogo au zaidi kiumri. Mafunzo hayo yaliyoendeshwa porini kwa masiku kadhaa, yalifahamika kama Jando au Jandoni kwa upande wa wavulana na unyago kwa mabinti (wana wari). Jandoni, wavulana walitahiriwa na kupewa mafunzo mbali mbali ya tabia na ukakamavu katika kipindi chote cha mauguzo.haya yalifanyika katika utaratibu maalum uliowekwa na wahenga wa kabila. vijana walilelewa hivyo kwa kipindi chote, lengo likiwa kudumisha mila na desturi za kabila, athari ya mafunzo hayo ilionekana katika maisha ya vijana. Wale ambao hawakupata fursa ya kupita "kambi" hizo walijulikana. Ndio tukajasikia maonyo na makaripio dhidi ya tabia mbovu kwamba wahusika hawakwenda jandoni kwa maana hawakupata mafunzo maalum au hawakupita katika tanuri la tabia, yaani si waungwana. Kwani Muungwana ni yule anayejiepusha na kila lenye kuudhi wengine. Hujitahidi kutenda yafaayo kisha watu wakamsifu kwayo. Yule mwenye tabia ya kujisifusifu si muungwana. Yule mwenye kiburi si muungwana. Mwenye kauli za kuudhi si muungwana, asiye na huruma kwa wengine si muungwana. Mwenye majivuno si muungwana, na kadhalika. Hayo ni mambo ya zamani jandoni, kama yapo mazuri yaliwanufaisha baadhi ya watu na kinyume. Katika toleo lililopita la gazeti hili ukurasa wa mbele nilisoma habari iliyohusu ziara ya Alhaji Ali Hasaan Mwinyi mkoa wa Mwanza. Kwa mujibu wa ripoti hiyo Wananchi wa mkoa huo, wenyeji kwa wageni walimlaki kwa shangwe na hoi hoi Rais huyo mstaafu wa awamu ya pili. Swali lililokuja mara tu baada ya kusoma habari hiyo ni kwa nini imekuwa ni kawaida kwa Rais huyo mstaafu kushangiliwa kila anapopita. Hapana shaka kuna mengi mazuri aliyoyafanya wakati wa kipindi chake cha uongozi kwa hiyo kutokana na hayo wananchi hushindwa kujizuia kila wamuonapo. Na huenda pia mashangilizi haya huwa na ujumbe wa namna fulani unaofikishwa na wananchi hao kwa watawala waliopo ambao inasemekana hawajafanya lolote tangu washike madaraka. Ndipo nikakumbuka kuwa Mzee Mwinyi anastahili hayo kwa sababu ni muungwana yeye aliyewalisha na kuwavika vizuri Watanzania baada ya kuwakuta hoi, fii na taabani chini ya kinyamkera cha "ujamaa na kujitegemea" cha awamu iliyomtangulia. Ni muungwana yeye aliyewatoa ngomeni Watanzania chini ya zidumu fikra sahihi za mtu fulani. Ni muungwana huyu aliyefungua demokrasia ya upashanaji wa habari ambayo awali ilitungikwa kitanzini chini ya jinamizi la Glanost! Ni muungwana yeye aliyesimamia kikamilifu mageuzi ya kisiasa yanayoonekana kupingwa na wahafidhina wenye kujali maslahi yao zaidi. Nchi chini ya uongozi wa Muungwana huyu na washauri wake wa karibu iling’ara kinyume na kabla yake halikadhalika baada yake. Kwa uungwana wa kwetu mgeni wa aina hii hustahili heshima ya pekee na tunakawaida ya kumkaribisha kwa "bhabhooooo" katika mji wetu uliojaa mapagala (vidunda) ya tangu uhuru! |
YALIYOMO
Tahariri
Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|