AN-NUUR 
Na.182 Ramadhan 1419, Januari 1 - 7, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Matokeo ya Darasa la Saba yacheleweshwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi
  • Wananchi wahoji je, nchi hii ina dini moja tu?
WANANCHI mbalimbali wamewasiliana na gazeti hili wakieleza kushangazwa na kauli ya Wizara ya Elimu na Utamaduni kwamba matokeo ya mitihani ya darasa la saba yamechelewa kutolewa ili kuwapa fursa watoto wa Kikristo kusherehekea vizuri sikukuu ya Krismasi. 

Wamesema taarifa hiyo iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari imewaacha wananchi hao wakijiuliza maswali mengi kuliko majibu. 

Katikati ya wiki hii msemaji wa Wizara ya Elimu wakati akielezea  

moja ya sababu za kuahirishwa kutolewa matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu mbele ya waandishi wa habari, alisema kama matokeo hayo yangetolewa kabla ya Krismasi watoto wa Wakristo ambao hawakuchaguliwa wasingesherehekea sikukuu ya Krismasi kwa furaha. 

Bw. Abeid Juma akiongea na gazeti hili alisema kwamba kauli hii inawakilisha dhana iliyojengeka miongoni mwa watendaji wa serikali kamba wanafunzi wote ni Wakristo tena basi wakusherehekea Krismasi. 

Kufuatia mawasiliano na wananchi waliotaka ufafanuzi wa maelezo ya Wizara, AN-NUUR iliwasiliana na Wizara ya Elimu kutaka kujua ukweli wa madai haya. Baada ya kumkosa Mh. Waziri na Katibu wake Mkuu, Msemaji mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake alikiri kwamba Katibu Mkuu wa Wizara alitoa sababu hiyo lakini akadai kuwa hiyo haikuwa sababu pekee. Hata hivyo hakutoa ufafanuzi zaidi. 

Kilichowafurahisha wananchi walioongea na gazeti hili ni kuona jinsi Wizara ilivyo makini na inavyojali na kuthamini hisia za kidini za wanafunzi katika utendaji wake. 

Hata hivyo, wamehoji je, nchi hii ina dini moja tu. 

Taarifa hizi za kucheleweshwa kutolewa matokeo ya darasa la saba ili kuwawezesha watoto Wakristo kusherehekea vizuri Krismasi zimekuja wiki moja tu baada ya gazeti hili kuripoti kuwa wanafunzi Waislamu watalazimika kufanya mitihani ya kidato cha nne ndani ya Ramadhani na pengine kuikosa Id el Fitr. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma

Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha

Matokeo ya Darasa la Saba yacheleweshwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi: Wananchi wahoji je, nchi hii ina dini moja tu?

Njaa yaikumba Kilwa

Dondoo za Saikolojia
Na. Abu Halima Sachangwa

Kona ya Wacha Mungu
Mavuno yangu yasiwe...

Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana huyoo!
Na Sompo wa Kahambwe

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897)

Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Imetayarishwa na Africa Muslims Agency

Marekani ni mtetezi au adui wa haki?: Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Na Abu Salim

Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Na Habiba Swedi, Arusha

Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an

Ijue  Madrasa Hudaa Arusha

Wazazi waaswa kutoshabikia maovu

Mzee maarufu afariki Moro

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? (jibu) 
Na Ally Said

Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani?

Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Na Habiba Swedi

Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar

Baada ya kuvunjiwa nyumba, kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Na Q. Mtaita

Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile

Sayansi na Teknolojia 
[Kuunganisha Kompyuta kwa Kutumia Modem

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Saumu na lishe ya mama anayenyonyesha] 
 


Baraza ya Wasomaji
(Kwa mjadala na maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu)

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita