|
Na. 034 Jumatano Februari 9 - 15, 2000 |
|
|
|
|
|
KATIKA KUONGEZA USHINDANI
Mabadiliko hayo yametangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Aden Rage jana katika ukumbi wa jengo la FAT alipokuwa akiongea na wanahabari Jijini, mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kumalizika. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kilikuwa na kibarua cha kuhakiki majina ya wachezaji waliosajiliwa na timu 20 zitakazoshiriki ligi kuu mwaka huu. Aidha, Rage ameahidi kutangaza rasmi leo majina ya wachezaji na vilabu watakavyochezea katika ligi kuu ikiwa ni pamoja na hitimisho la kinyang'anyiro cha wachezaji Steven Mapunda na Ephaim Makoye wanodhaniwa kusaini Simba na Yanga. Katika ligi hiyo ya makundi ambayo itaanza Machi 4, mwaka huu, Rage amesema itazishirikisha timu ishirini ambazo zimegawanywa katika makundi manne ya timu tano tano kwa kuzingatia mikoa zinakotoka. Kundi A imeelezwa litazishirikisha klabu zinazotoka kanda ya kaskazini na kati ambazo ni AFC, Coastal Union, Mji Mpwapwa, CDA na Mtibwa ambao ni mabingwa watetezi. Wakati kundi B litakuwa na klabu za kanda ya ziwa ambazo ni Singida United, Kagera, Milambo, Pamba na Toto Africa. Simba watoto wa Msimbazi wamepangwa na timu za kanda ya nyanda za juu katika kundi C lenye timu za Lipuli, Majimaji, Prisons na Tukuyu Stars huku wakimuacha hasimu wao mkubwa katika soka Yanga kanda ya Mashariki inayounda kundi D lenye timu za Bandari, Kajumulo, Kariakoo na Reli. Kwa mujibu wa Rage timu tano kutoka kila kundi zitacheza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na timu moja ya mwisho toka kila kundi itashuka daraja na kuziacha mbili za kwanza katika kila kundi zitakazofanya jula ya timu nane ambazo zitacheza ligi ya kilele yaani Safari Lager Super Premier League katika hatua ya pili. "Katika hatua hii, ligi Kuu pia itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, washindi watatu wa kwanza ndiyo watakaowakilisha Tanzania Bara katika Ligi ya Muungano na timu tatu za visiwani", amesema. Akifafanua zaidi Rage amesema mshindi wa kwanza katika Safari Lager Super 8 Premier League ndiyo ataiwakilisha Tanzania Bara katika bingwa ya Afrika Mashariki na Kati. Aidha, Rage ametaja faida za mfumo huu mpya wa ligi kuwa ni kuifanya ligi iwe fupi zaidi na kushirikisha timu nyingi pia kuongeza msisimko wa kushindana na hivyo kuinua hamu ya watazamaji na kuongeza pato. Hali kadhalika, kupunguza gharama za vilabu vinavyoshiriki na kuongeza
vivutio toka kwa wafadhili, zawadi na maslahi ya timu.
KLABU ya soka ya Simba ya Jijini leo inajitupa katika uwanja wa Taifa Jijini kucheza mechi ya kirafiki n atimu ya Prisons ya Mbeya. Prisons ambao ni mabingwa wa soka Tanzania wanatarajiwa kutumia mechi hiyo kufanya tathmini y amwisho juu ya uwezo wao kisoka kabla ya kupambana na timu ya Feroviaro ya Msumbiji. Feroviaro watakuwa wageni wa Prisons katika mchuano wa marudiano utakaofanyika Jumamosi au Jumapili wiki hii, uwanja wa Taifa kugombea kombe la Klabu Bingwa Afrika. Katika mchezo wa awali uliofanyika mjini Maputo, Prisons ilifungwa bao 1-0. Prisons imefanikiwa kupata fursa ya kucheza na Simba leo baada ya jitihada zake za muda mrefu kugonga ukuta kwa Simba na Yanga kwa kile kilichodaiwa kutofuata utaratibu. Akiongea na gazeti hili jana jijini kocha mkuu wa Simba, Nzoyisaba Tauzany aliahidi kupanga kikosi cha kwanza dimbani ili kuipa mazoezi ya kutosha Prisons. Naye Katibu Mkuu wa FAT, Ismail Aden Rage pamoja na kuthibitisha kuwepo kwa mechi hiyo pia ametja viingilio katika mchezo wa leo kuwa ni shilingi mia tano kwa mzunguko, jukwaa la kijani na jukwaa kuu.
Michuano ya soka Mataifa ya
Afrika:
TIMU ya Taifa ya Afrika Kusini kesho inatarajiwa kuing'oa timu ngumu ya Nigeria (Super Eagle) katika michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika katika mchezo wa nusu fainali utakaofanyika mjini Lagos, Nigeria. Matumaini hayo yametolewa na wapenzi wengi wa soka mjini Dar es Salaam wanaofuatilia michuano hiyo, walioongea na mwandishi wa habari hivi kwa nyakati tofauti, kwa madai kuwa Nigeria imeonesha 'ubovu' mkubwa katika safu yake ya ulinzi huku Bafana Bafana wakiwa na washambuliaji wenye uchu mkubwa wa kufunga. "Bafana Bafana inayo washambuliaji wenye kasi na wasiokata tamaa kama vile akina Siyabonga Nomvete, Helman Mkhalele, Dumisa Ngobe, Fortune na mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi Shaun Bartlet", amesema Derick Dominic mkazi wa Tandale Jijini. "Vile vile 'ukuta' wa Bafana Bafana ni mzito kupitika kirahisi ambao uongozwa na wachezaji mahiri, Lucas Ladebe, Piere Issa na Mark Fish ambayo wameonesha kiwango kikubwa cha uchezaji katika michuano hiyo', amesema. Hata hivyo, shabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Omar, ameonesha wasiwasi wake kwa kutokuwepo kwa kiungo mahiri wa Bafana Bafana, Eric Tinkler ambaye alioneshwa kadi mbili za njano katika pambano la robo fainali na Ghana na hivyo kutoka uwanjani na kumfanya akose pambano hilo la nusu fainali. Timu nyingine zitakazocheza katika nusu fainali hizo ni Cameroun itakayomenyana na Tunisia. Cameroun imefikia hatua hiyo baada ya kuitoa Algeria na Tunisia iliweza kuking'oa kigogo Misri ambacho kilikuwa ndio bingwa mtetezi. |
YALIYOMO
Tahariri:
Serikali inakwamisha barabara ya Kibiti-Lindi -CUF Waislamu kuadhimisha mauaji ya Mwembechai J’pili Wazanzibar sasa wataka kuuona Mkataba wa Muungano Wanawake wa Kiislamu watakiwa kupinga unyanyasaji wa kijinsia Rufaa za chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji MAKALA
MAKALA
Kalamu
ya Mwandishi
Makala
USHAURI
NASAHA
MAKALA
LISHE
Michuano ya soka Mataifa ya Afrika |
|
|
|
|