NASAHA
Na. 034 Jumatano Februari 9 - 15, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI ZA KIMATAIFA 



Wachechnya wapania kuidhibiti upya Grozny

Barcelona, Hispania

KIONGOZI wa Chechnya Aslan Maskhadov amesisitiza dhmaria yao ya kuukamata upya mji wa Grozny kutoka katika majeshi ya Russia. Bwana Maskhadov aliyasema hayo katika mahojiano yaliyochapoishwa na gazeti moja la kila siku la Hispania liitwalo Vanguardia.

"Kwa sasa tumeuachia mji. Tutauchukua tena katika siku za baadae", amesema Maskhadov na kuongeza kwamba vita vya msituni ndiyo hatua itakayofuata. 

Bw. Maskhadov alikanusha habari za kuwepo kwa majeruhi wengi miongoni waasi waliogawanyika na kusema kwamba majeshi ya Chechnya walitoka nje ya mji kwa mpangilio madhubuti kupitia njia iliyokuwa imetayarishwa. 

"Kikosi kikubwa cha askari 2,000 kilitoka bila ya kupata hasara. Kundi lingine la watu 300 au 400 liligonga mgodi wa madini na kupata hasara kadhaa. Lakini vikosi vyetu vingi vilifanikiwa kutoka nje ya mji bila ugumu wowote na viko mahali pa salama hadi sasa", alisema Bw. Maskhadov. 

"Tumeamua kuhamia katika vita vya msituni. Tutakamata maeneo yetu katika bonde la mto Argun", aliongeza. 



Wanaoacha umalaya wagawiwa fedha Zamfara

JIMBO la Zamfara nchini Nigeria ambalo Januari 27 mwaka huu lilitangaza kuanzisha sheria ya Kiislamu jimboni humo ili kukomesha watu kufanya maovu kinyume na jamii iliyostaarabika sasa limeanzisha kampeni ya kuhimiza ndoa kwa kuwagawia fedha taslimu malaya wote wanaokubali kuacha biashara yao ya ukahaba ili wafunge ndoa kihalali.

Jimbo hilo linatoa Naira 25,000 (ambazo ni sawa na dola 250 za Marekani) kwa kila mwanamke anayefanya biashara ya ukahaba aliyeamua kuacha umalaya kwa ridhaa yake mwenyewe ili afunge ndoa. 

Mpaka sasa wanawake 27 wameishapokea fedha hizo zilizokuwa zikitolewa na mke wa Gavana wa jimbo hilo Bi. Kavina Ahmad Sani. 

Dola hiyo ya Kiislamu pia itatoa msaada wa kifedha kwa wanandoa wapya wa baadaye. "Kw wimbi la sharia linaloendelea katika jimbo hili, shughuli zetu zote zitalazimika kuandama na mafundisho ya Qur'an", alisema Bibi Ahmad. 

Jimbo hilo pia limedhamiria kuondoa tatizo la watoto ombaomba wa mitaani na vijana wazururaji kwa kuwajengea vituo maalum vya kuwashughulikia mahitaji yao. 

Licha ya serikali kutoa uhakikisho kwamba sheria ya Kiislamu jimboni humo haitawagusa watu wasio Waislamu, bado Wakristo jimboni humo hawajaridhika. Baadhi ya watu wasio Waislamu wamekimbia jimboni humo ili kuepuka kuvunja sheria hiyo ya Kiislamu. 

Rais wa Nigeria, Jenerali Obasanjo ambaye ni Mkristo amepinga azimio hilo la Gavana Sani na kuhoji uhalali wa sheria ya Kiislamu. Hata hivyo, Rais Obasanjo hakumtaka Gavana Sani kuondoa sheria hiyo. 

Rais Obasanjo alisema mwezi Novemba mwaka jana kwamba aliamini sheria hiyo isingeweza kutekelezwa Zamfara na kwamba jaribio hilo lingeshindwa. Hata hivyo, majimbo mengine manne ya kaskazini - Kano, Niger, Sokoto na Yobe yameshaanzisha sheria ya Kiislamu pamoja na majimbo mengine ya kusini pia. 

Nigeria ina watu wanaokaribia kufikia milioni 120 asilimia 50 ikiwa ni Waislamu na Zamfara ni moa ya majimbo 36 ya Nigeria sasa inaongozwa na sheria ya Kiislamu kwa masuala yote ya kidini. 



Wiranto akanusha kuhusika na mateso ya watu wa Timor 

ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi ya Indonesia Jenerali Wiranto amesema kuwa hatokubali lawama zozote juu yake kama mtu binafsi au kuwajibika kwa lolote kwa kisheria juu ya makosa yaliyotendwa na askari wa Indonesia huko Timor Mashariki.

Jenerali Wiranto aliliambia gazeti la Straits Times la Singapore kuwa anajivunia rekodi yake na hatojiuzulu Uwaziri kwa vile hiyo inaweza kuonekana kama ni kukubali makosa. 

Wiki iliyopita Rais AbdulRahman Wahid alitoa mwito kuwa Wiranto ajiuzulu baada ya taarifa ya serikali kumlaumu Jenerali huyo kwa unyama uliofanyika Timor Mashariki. 

Tume ya haki za binadamu ya Indonesia ilipendekeza kuwa Wiranto na maafisa wengine watano wa ngazi za juu jeshini washitakiwe kwa kuhusika kwao na fujo zilizotokea baada ya kuwa na maoni juu ya uhuru wa Timor Mashariki ambako watu 250 walikufa. 

Taarifa ya Tume teule ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa vurugu za Timor Mashariki imewalaumu maafisa wa juu wa jeshi la Indonesia kwa kutoa amri ya kuishambulia Timor Mashariki. 



Hizbollah kulipiza kisasi kwa Israel

MAELFU ya Waisrail wanajiandaa na mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa wapiganajio wa Hizbollah walioko Lebanon baada ya jeshi la Israil kushambulia vituo vya nguvu za umeme huko Lebanon Jumatatu usiku.

Kiasi cha watu kama 17 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo ambayo ni makubwa kuliko yote ndani ya kipindi cha miezi saba. 

Ripota wa BBC, Hilary Anderson amesema hii inaweza kuwa sababu ya kusitishwa kwa mpango wa amani kati ya Israel na Syria. Mgogoro huu unaonekana kuendelea hasa baada ya Hizbollah kuahidi kulipiza kisasi mapema iwezekanavyo na Waziri wa serikali ya Israel kudai kuwa kuanzia sasa hawatozingatia tena makubaliano ya 1998 yanayotaka raia wasishambuliwe. 

Wayahudi wengi wanaoishi mpakani na Lebanon walipitisha usiku mzima kwenye vizuizi vya kuwakinga na mashambulizi ya anga ya Hizbollah. Wameshauriwa na jeshi kubakia katika mahandaki hadi watakapotangaziwa vinginevyo. Wayahudi wengine walikimbia kwa magari muda mfupi kabla ya majeshi ya Israel kuanza kushambulia Lebanon. 

Mkazi mmoja wa mji wa Kiryat Shmona ulioko mpakani na Israel alieleza kuwa wengi wa wakazi wa mji huo wameondoka. Tumekuwa tukiishi katika hali hii ya mashambulizi kwa miaka 33 sasa. 

Pamoja na vitisho vya kamanda wa Israel Meja Jenerali Giora Eiland, kuwa shambulizi lolote la Hizbollah litajibiwa kwa nguvu zaidi, masaa machache tu baada ya uvamizi huo wa usiku Hizbollah walitoa taarifa kuwa hawatatishiwa na kuongeza kuwa "tunayo haki ya kujibu kwa wakati tukaouona ni muafaka, ambao inaweza kuw ani mapema, taarifa ya kikundi cha Hizbollah ilisema. 

Majeshi ya Wayahudi katika ardhi inayokaliwa na Israel yataendelea kuwa ni shabaha ya mabomu ya Mujahidina", taarifa iliongeza. 

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Barak ameahidi kuondoa majeshi yake katika ardhi ya Lebanon mwezi Julai. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri:
Mkataba wa Muungano wa 1964 usifanywe siri

Serikali inakwamisha barabara ya Kibiti-Lindi -CUF

Waislamu kuadhimisha mauaji ya Mwembechai J’pili

Wazanzibar sasa wataka kuuona Mkataba wa Muungano

Wanawake wa Kiislamu watakiwa kupinga unyanyasaji wa kijinsia

Rufaa za chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji

Makala 
Hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Zanzibar, Hassan Mussa Takrima  katika maadhimisho ya miaka 23 ya CCM 

MAKALA
Uhuru na ukombozi

MAKALA
Suala la Dk. Salmin kubadili katiba:
Wasomi wafichua siri ya Muungano

Kalamu ya Mwandishi
Wazanzibari unganeni 

Makala
UPINZANI  OCTOBA 2000 - 2

USHAURI NASAHA
Matitizo ya ajira, Nini kifanyike?

MAKALA
Mgogoro wa kisera ndani ya CCM usigeuzwe kuwa ni wa kitaifa

HABARI ZA KIMATAIFA 

  • Wachechnya wapania kuidhibiti upya Grozny
  • Wanaoacha umalaya wagawiwa fedha Zamfara
  • n.k

  • Riwaya
    Ndoto ya ajabu

    LISHE 
    Umuhimu wa mafuta mwilini

    Barua/Maoni

    MASHAIRI

    MICHEZO

  • Ligi Kuu sasa kuchezwa kwa makundi
  • Simba kuipa Prisons mazoezi leo 

  • Michuano ya soka Mataifa ya Afrika
     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com


    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita