|
Mashairi
Chuki kafukuzwa
Bismillah muhimu, kwa wingi wa ukarimu,
Asaalam aleykumu, ama baada ya salamu,
Ndugu zangu Islamu, ni letu hili jukumu,
Kufukuzwa kwake Chuki, tujaribu tafakari.
Kaletwa hospitali, matibabu akapewa,
Imefikia mahali, ikanenwa wamtowe,
Hiyo kweli ni kauli, halali atamkiwe?
Kufukuzwa kwake Chuki, tutafute muafaka.
Waislamu tukae, mawazo tukapeane,
Fikra zetu tutoe, vifua tusivibane,
Mikakati tuandae, itujenge tupambane,
Kufukuzwa kwake Chuki, tutafute muafaka.
Huo jama mtihani, katuletea Manani,
Hapa hapa duniani, ni Yeye alotupeni,
Ili atutathimini, atakaye kufu nani,
Kufukuzwa kwa Chuki, dhamira hasa ni nini?
Ndugu yetu kaka yetu, ni ndani ya yetu dini,
Mabinti nusra yetu, tena wanne jamani,
Wasiwasi ndani yetu, la kufanya hatuoni,
Kufukuzwa kwake Chuki, tunayo mengi majonzi.
Wabillah Tawfiq, mbele sitaendelea,
Natusiwe wanafiki, madhalimu kuwalea,
Kamwe nyuma hatubaki, mbele tutaendelea,
Kwa wetu mshikamano, Inshallah tutafuzu.
Aula Tinda,
S.L.P. 1573,
DAR ES SALAAM.
Mtukufu Ramadhani
Bismillahi naanza, kwa jina lake muweza,
Nilo nayo kueleza, mupate kuyasikia,
Ya muhimu kuwajuza, na ya kheri kuyajua,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Mtukufu Ramadhani, sasa kishatufikia,
Tumjue kwa makini, kuwa ni kujizuia,
Kutia kitu kinywani, na maasi yote pia,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Tufunge kwa lengo lake, ucha Mungu kufikia,
Pia umuhimu wake, tupate kuutambua,
Tuzipate radhi zake, kwa kutekeleza Twaa,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Mwezi huu Qur'an, ndio imetushukia,
Kafaradhisha Manani, kwa watu kujifungia,
Nguzo zake kwa yakini, nia na kujizuia,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Nia kila Isilamu, moyoni kukusudia,
Kujizuia muhimu, alfajiri sawia,
Hadi jioni kutimu, bila ya kuingilia,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Katika yaliyo Sunna, ni kufuturu mapema,
Na daku usiku sana, na Qur'an kusoma,
Na kuwa karibu sana, na kwa swala kusimama,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Kufanya mema muhimu, na miezi ilosalia,
Kwa kutafuta elimu, na swala kujiswalia,
Zaka na hija kutimu, kila ovu kuondoa,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Kama unalazimika, mwezi ukiusikia,
Ufunge bila mashaka, hadi siku kutimia,
Viwanjani kufurika, Iddi kwenda jiswalia,
Karibu mgeni wetu, mtukufu Ramadhani.
Juma M. Bwanakheri,
(Ustaadh),
S.L.P. 45245,
DAR ES SALAAM.
|
YALIYOMO
Maoni
Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani?
Wananchi waingiwa na hofu kuhusu
silaha
Serikali yagwaya kwa wafugaji
nguruwe
Na Muhibu Said
Hakuna njama za kupindua Bakwata -
Sheikh Yahya
MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Na. Abu Halima Sachangwa
Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Na Maalim Mwalimu
Adabu katika swala
Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo:
Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Na Ally Said
Muhammad (s.a.w.) katika
Unabii wa Isaya (a.s.)
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa, Korogwe
Ijue SUA Madrasa Moro
Na Mussa Ally, Morogoro
Kiteto wakosa darsa kwa kupinga
Ramli
Ustadh ayeyuka na saruji ya
Msikiti mjini Arusha
Akina mama Muheza waungana kufanya
Daawa
Na B. Mwakangwale
Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata
uongozi
Na B. Mwakangwale
Je, hivi tuendelee kushika amri
za Mungu tena? - 2
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu
Njia ya uzima ni nyembamba,
waionao ni wachache - 2
Na Yasin Valerian Massawe
Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Na Mwandishi Wetu
Sheikh Jongo aichachamalia
Uwawaru
Na Badru Kimwaga
Waamriwa kurejesha Mali ya
Mirathi
Na Njuki A.
Waislamu Mlimba Moro mashakani
Na Q. Mataita
Sayansi na Teknolojia
[Ielewe Modem yako]
Mafundisho ya Quran
Masomo ya Dini ya Kiislamu
Barua za Wasomaji
Mashairi
Chakula na lishe
[Futari ya Tende]
Tangazo
Vitabu na Mihutasari ya Maarifa ya Uislamu
|