AN-NUUR 
Na.179 Shaaban  1419, Desemba 11 - 17, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya 
 
  • Asema kuna kutokuelewana
MKUU wa Idara ya Habari na Mambo ya Nje wa Bakwata, Sheikh Yahya Hussein amekanusha kuwepo njama za kupinduliwa uongozi wa Baraza hilo. 

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake mtaa wa Kagera Mwembechai Jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo wa Bakwata amesema kuwa tuhuma hizo si za kweli na kwamba zimelenga kujenga hofu isiyo na msingi. 

Sheikh Yahya amezihusha tuhuma hizo na mtafaruku uliomo Bakwata hivi sasa baina ya viongozi wake na kusema kwamba huenda ni baadhi ya viongozi wa baraza hilo walioneza uzushi huo. 

"Hizi ni njama zimefanywa na baadhi ya uongozi wa Bakwata ili kuleta hofu kwa Mufti na akubaliane na uongozi huo juu ya ubaya wa wale wasiotakiwa", amesema Sheikh huyo. 

Aliongeza kusema kuwa hakuna njama hizo na kama zingalikuwepo yeye angelifahamu mapema. 

Hata hivyo, alikiri kupigiwa simu na mtu ambaye hakumfahamu kutoka mahali alipokuita "nyeti" akieleza kuhusu njama hizo. 

Aidha alisema, Waislamu wanaelewa wazi njia ya kuichukua Bakwata si kuivamia bali kuitikia wito wa Mufti Hemed bin Juma wa kujiunga na Bakwata na kushiriki uchaguzi. 

Alituhumu kuwepo kwa njama zinazopangwa na baadhi ya viongozi wakuu wa baraza kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wakubwa serikalini dhidi yake na Mufti. 

Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuhojiwa kwa baadhi ya Masheikh jijini kuhusiana na tuhuma zilizodaiwa kuwepo polisi juu ya mpango wa kupindua uongozi wa Bakwata makao makuu. 

Hata hivyo, haikuweza kufahamika tuhuma hizi zilifikaje polisi na kwa vipi Masheikh waliotajwa walihusika na mpango huo. ndani ya Bakwata 

Juu 
 

YALIYOMO 
 

Maoni
Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani?

Wananchi waingiwa na hofu kuhusu silaha

Serikali yagwaya kwa wafugaji nguruwe 
Na Muhibu Said

Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Na. Abu Halima Sachangwa

Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Na Maalim Mwalimu

Adabu katika swala

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo: Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Na Ally Said

Muhammad (s.a.w.) katika Unabii wa Isaya  (a.s.)
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa, Korogwe

Ijue SUA Madrasa Moro
Na Mussa Ally, Morogoro

Kiteto wakosa darsa kwa kupinga Ramli

Ustadh ayeyuka na saruji ya Msikiti mjini Arusha

Akina mama Muheza waungana kufanya Daawa
Na B. Mwakangwale

Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata uongozi
Na B.  Mwakangwale

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 2
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

Njia ya uzima ni nyembamba,  waionao ni wachache - 2
Na Yasin Valerian Massawe

Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Na Mwandishi Wetu

Sheikh Jongo  aichachamalia Uwawaru
Na Badru Kimwaga

Waamriwa kurejesha Mali ya Mirathi
Na Njuki  A.

Waislamu Mlimba Moro mashakani
Na Q. Mataita

Sayansi na Teknolojia 
[Ielewe Modem yako] 
 
Mafundisho ya Quran

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Futari ya Tende] 
 
Tangazo
Vitabu na Mihutasari ya Maarifa ya Uislamu

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita