|
|
|
NIKIWA Mwinjilisti katika Kanisa la Waadventista wa Sabato, mara
nyingi sana nimekumbana na swali hili, tena kwa watu mbalimbali, kwa nafasi
hii naitumia kutoa majibu ya swali hili kwa kirefu. Tafadhali nifuatilie
kwa makini katika sehemu hii ya pili ya majibu yangu. Swali hili limekuwa
kubwa kwa watu mbalimbali, hata limegawa watu katika makundi mawili, wanaokubali
na kushika amri za Mungu. Na wanaokataa kwamba sasa hauna amri, ziliishia
msalabani tena amri zilikuwa za Musa na wana wa Israeli. Kwa makala hii
fuatana ili kupata hatima ya swali hili. Kwanza kabisa kwa msomaji ama
kwa mwenye swali hili apendaye kupata jibu sahihi yampasa amfahamu kwanza
huyo Mungu anayemwabudu kwamba ni Mungu yupi katika sehemu hii ya pili.
Endelea...
Tena kwa sababu ya kuvunja sheria ya Mungu walijiona wako uchi, Mungu akatoa Injili tena. Mwanzo 3:21 "Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi akawavika". Unaweza kuona upendo wa Mungu jinsi ulivyo mkuu. Mifano ya sheria katika Agano jipya: Mathayo 5:17 "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii la, sikuja kuitangua bali kuitimiliza". Unaweza kuona hapo Yesu anaweka wazi jambo hili kwa wote wanaotatanika na sheria. Pia Mathayo 21:12-14 "Yesu akaingia ndani ya hekalu akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipundua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa, akawaambia imeandikwa nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi. Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni akawaponya". Pia unaweza kuona hapo Yesu anawatimua mbio mle hekaluni, kisha anaketi na kuanza kuponya wagonjwa wao. Yote hayo ndiyo sheria ya Injili. Kumbuka kwamba utakatifu wa Mungu unapokutana na dhambi ndipo unapogeuka na kuwa hasira na hukumu na dhambi maana yake ni uvunjaji wa sheria. Sasa tuangalie kidogo hizi sheria za Mungu. Mungu anazo sheria na maagizo mengi. Lakini yote hayo yamefungwa katika Amri zake kumi zilizoandikwa katika kitabu cha Kutoka 20:3-17 pia kwenye Kumbukumbu la Torati 5:7-21. Hizi ndizo amri za Mungu ambazo ndicho kiini cha swali letu tunaloendelea nalo. Pengine zingekuwa ni sheria za nchi tungesema ndiyo katiba yenyewe yaani sheria kuu, Yesu pia aliulizwa aeleze sheria kuu ni ipi? Mathayo 22:35 "Mwalimu, katika Torati ni amri ipi iliyo kuu? Yesu akajibu, Mathayo 22:37 "Akamwambia, mpende Bwana Mungu Wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na akili zako zote, hii ndiyo amri iliyo kuu tena ya kwanza na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii mpende jirani yako kama nafsi yako". Hapa Yesu alikuwa anazieleza kama zilivyoandikwa katika mbao mbili za mawe. Kwamba amri 1-4 Kutoka 20:3-11 au Kumbukumbu la Torati 5:7-15 zinatuhimiza tumpende na kumheshimu Mungu wetu aliye mtakatifu na muumbaji nazo zimefungwa katika amri moja. Na amri ya 5-10, Kutoka 20:12-17 au Kumbukumbu la Torati 5:16-21 nazo zinatuhimiza tuonyeshe tabia ya Mungu ya upendo kwa kupendana sisi kwa sisi nazo zimefungwa katika amri ya pili. Hivyo ndivyo mambo yalivyo wazi bila utatanishi wowote. Kosa kubwa linalofanyika kwa wasomaji wengi wa Biblia hata kuibua maswali yasiyo na sababu ni la Kutokutofautisha kati ya amri kumi za Mungu zilizoandikwa Kutoka 20:3-17 au Torati 5:7-21 na sheria za Musa Malaki 4:4. Tofauti ya Amri hizi ni hii: Amri za Mungu alizindika Mungu mwenyewe kwa kidole chake. Kutoka 31:18. Amri za Mungu ziliandikwa juu ya mbao mbili za mawe. Kumbukumbu la Torati 5:22, Kumbukumbu la Torati 4:12. Amri kumi za Mungu ziliwekwa ndani ya sanduku la agano. Kumbukumbu la Torati 10:5. Amri kumi za Mungu ni za milele kwa vizazi vyote. Kumbukumbu la Torati 4:40, Zaburi 111:6-9), Zaburi 119:44. Sheria za Musa tofauti yake ni hii: Zinaitwa za Musa kwa sababu aliziandika Musa. Kumb. 31:9, Malaki 4:4. Ziliandikwa katika chuo. Kumb. la Torati 31:24. Ziliwekwa kando ya sanduku la agano. Kumb. 31:26. Zilikuwa kivuli cha mambo yajayo Ebrania 10:1-4 Kolosai 2:17. Ndani ya sheria hizo kulikuwepo na sadaka za upatanisho, Law 23:17-32, sadaka za vinywaji, Hesabu 15:5, 24 Sabato za miezi na miaka Lawi 25:4, 8, miandamo ya miezi, sheria za kimwili, vyakula na vinywaji na kutawadha n.k. Ndiyo maana Paulo katika Wakolosai 2:16 anasema: "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi au Sabato". Akijua wazi kwamba mambo hayo yalikuwa kivuli cha mambo yajayo. Ndiyo maana leo kwa mwenye dhambi hahitajiki tena kubeba mnyama ama ndege na kupeleka kwa kuhani kwa ajili ya dhambi, Yesu ndiye mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu Yohana 1:29. Sheria hizo ndizo zilizoishia msalabani. Sheria ya amri kumi Kutoka 20:3-17 ndiyo sheria ya milele na ndiyo amri kuu. Kumbukumbu la Torati 4:40. Warumi 3:20 "Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria, kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria". Soma pia Warumi 7:7. Maandiko haya yanafafanua wazi kazi ya sheria kwamba ni kuonyesha dhambi tu. Wala sheria haiokoi mfano wake ni sawa na kioo. Kazi ya kioo siyo kuondoa uchafu, bali ni kuonyesha jinsi ulivyo, ukijiona una uchafu, nenda katafute maji na sabuni. Uoge ama ufue. Sheria inaonyesha dhambi. Na ukiona umechafuka na dhambi nenda kwake yeye atusafishaye na udhalimu wetu. Yesu Kristo. Watu wengi wamekuwa wakisema kwamba tumeokolewa kwa neema hivyo hatuna haja ya kushika sheria. Je huku kuokolewa kwa neema ni nini? Neema ama rehema ni upendeleo wa bure unaotolewa bila sharti lolote. Na ndipo tunapozungumzia suala la kuokoka yatupasa kuzungumza katika awamu tatu. Awamu ya kwanza ni wokovu kwa ulimwengu wote, yaani wanadamu walipofanya dhambi, Mungu alitayarisha mpango wa wokovu kwa wote kupitia katika Yesu. Na kifo chake pale msalabani kilihitimisha mpango huo. Na kila mmoja wetu duniani akawa ameokolewa na kufanywa mlokole! Hapo ndipo tulipookolewa kwa neema Tito 2:11 "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa". Awamu ya pili ni pale mmoja wetu duniani anapomkiri na kumpokea Bwana wetu Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wake. Hapo ndipo anaokoka na kuanza safari ya wokovu. Na safari hii huhesabiwa mwishoni jinsi unavyomaliza. Wengi walianza vizuri, wakamaliza vibaya, hivyo wokovu na kuokoka kwao kukawa si chochote si lolote, kama akina Yuda, na wengi wetu leo. Awamu ya tatu na ya mwisho ni hapo atakaporudi mara ya pili Bwana Yesu akukute umelala - mauti ama uhai ukiendelea kuchuchumilia wokovu kwa kuwa na tabia yake ya utakatifu na upendo hapo utaokolewa na kuokoka milele. Mathayo 24:13 "Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka". Hivyo neema ama rehema haitupi hati yoyote ya kuvunja sheria ama kukataa amri, Tito 2:11-12. Maandiko yanazidi kutusisitiza kuheshimu utakatifu wa Mungu kwa kushika sheria zake. Mhubiri 12:13 "Hii ndiyo jumla ya maneno yote yamekwisha sikiwa, mche Mungu nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu".Jumla ya mtu ni kumwabudu na kushika amri zake, na siyo kumwabudu tu. Tena ni kumwabudu kwa kushika amri zote bile marekebisho wala ukarabati. Na tukivunja moja ni sawa na tumevunja zote. Yako 2:10. Na waraka wa kwanza wa Yohana 5:3 "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake wala amri zake si nzito". Kusema kwamba tunampenda Mungu huku tunakataa amri zake, maandiko yanatutia hatiani kwamba sisi tu waongo wala hatuna kweli yoyote (1 Yohana 2:3-4) "Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake". Ndiyo maana tabia ya Walokole (watu wa Mungu) watakaonyanyuliwa na Bwana
imetajwa katika Ufunuo 14:12 "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao
wazishikao amri za Mungu, na Imani ya Yesu". Huo ndio ukweli wa maandiko
na jibu la swali letu. Amina.
Nabii wa ishirini na nne (24) alisema alitabiri kusita ujumbe wake. Akasema: Sikuja kutengua Torati wala Manabii. (Mathayo 5:17-19). Mafunzo haya si yangu, ila ni yake Yeye aliyenipeleka (Yohana 7:16, 5:30, n.k.). Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotoa wa nyumba ya Israel. (Mathayo 15:21-26, 2:2, 2:6, 7:6, 10:23, 10:5-7 n.k.). Jihadharini watakuja wengi kwa jina langu na watapoteza wengi. (Mathayo 7:15-27, Luka 13:24-30 n.k.). Mtaliona lile chukizo la uharibifu lililonenzwa na Daniel limesimama patakatifu. (Mathayo 24:15). Naye Daniel alitabiri. Akasema: Masihi (Yesu) ajaye atakataliwa mbali, atakuwa hana kitu. (Daniel 9:26-27). Atajitokeza ‘mfalme’ mmoja atakayenena kinyume cha Aliye Juu (BWANA) ambapo atawashusha (atawaangusha) wafalme watatu. (Daniel 7:25). Baada ya Yesu kuondoka, Paulo ambaye alikuwa adui wake mkuu na ambaye kazi ilikuwa kuwatesa na kuwaua na kuwakufurisha wanafunzi wa Yesu, ajitokeza na kudai ametokewa na Yesu. Aanza kusababisha yale aliyotabiri Yesu: Ahubiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Mwanafunzi wa Yesu wamwogopa na kumhofia. Wayahudi wakimbizana naye kwa kushangaa mafundisho yake. Wadai anafundisha kinyume na desturi za Taifa la Israel n.k. Wayahudi wadai anavunja Torati ya Musa. Wayahudi wadai anavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria. Adai kuwa ameambiwa na Mungu apeleke habari Rumi (Italia). Yote haya ni kwa mujibu wa Matendo 9:1-30, 21:27-31, 22-23, 17:18-20, 18:12-13 n.k.). Yazuka elimu mpya kuhusu Roho Mtakatifu, Mwana na Baba. Yesu alikwisha kutahadharisha kwamba "... Mtawatambua kwa matunda yao ... mtu hawezi kuchuma zabibu kwenye miiba..." Sasa je! Huyo aliyemtokea Paulo ni Yesu kweli? Na je! Huyo Yesu angemtokea Paulo kama nani? Na je! Paulo alifundisha kama Yesu alivyofundisha? Paulo hakufundisha lolote kama Manabii ila habari zake binafsi za "Yesu Mfufuka". Na je! Mbona wale Wakristo ambo hutoa ushuhuda kama wa Paulo (kwamba Yesu kawatokea) hawakubaliwi na wenzao? Hii ni kwa sababu Wakristo wamejichanganya nafsi zao kwa kuamini juu ya Mwenyezi Mungu yasiyokuwa ndiyo. (Wamejichanganya kwa mbegu za wanaadamu) (Daniel 2:42-43). Paulo ndiye aliyewapoteza Wakristo anwani sahihi ya Mwenyezi Mungu lakini ni wachache waonao. Mtu yeyote aliyesoma na mwenye upana wa mawazo anajua kwamba Paulo, akina Petro n.k. walipotosha, hivyo ujumbe haukuwa ujumbe wa Yesu bali ujumbe batili wa akina Paulo chini ya jina la Yesu. Mafundisho ya Yesu yalitupiliwa kando, na watu wakajivika mamlaka chini ya kivuli cha dini, hivyo kufanya mambo yao waliyoyataka. Hivyo Paulo aliwauza watu wa Mataifa. Watu wa Mataifa walihubiriwa ‘Injili’ bandia ambayo matokeo yake imelemaza akili, mioyo na kuua ufahamu wa wengi. Matokeo yake wale waliopotea njia ndiyo wanajiona wako katika njia ya salama. Mathayo 7:13-14 - "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionayo ni wachache". Kumbuka Yesu kasema nini katika Marko 12:28-34 na fikiria kwa nini alisisitiza sana kuhusu manabii wa uongo kisha angalia Yohana 20:17 - "...Naapa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu". Mathayo 7:24-27 - "Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kufanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga ile nyuma, isianguke, kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga ile nyumba, ikaanguka, nalo anguko lake likawa kubwa". Kuyashika maneno ya Yesu maana yake ni kumkiri yeye kwamba katumwa na BWANA na ameumbwa na BWANA na kwamba BWANA ni mmoja. Hana mshirika. Kupitia mlango mwembamba maana yake ni kuiga mwenendo wa manabii (maisha adili). Tukirudi nyuma, baada ya Daniel kumtaja ‘mfalme’ atakayenena kinyume cha Amri ya Aliye Juu (BWANA), umetajwa ufalme wa mamlaka na ukuu wa ufalme chini ya mbingu zote (Daniel 7:26-28) Ufalme huu ni yule Nabii wa ishirini na tano (25) katika Manabii ishirini na watano wakuu ambaye ni Mtukufu wa Daraja katika viumbe, Jemadari Muhammad (s.a.w.). Ufalme wake ni Agano Jipya la Milele litakalovunja falme zote za awali (Daniel 2:44-45). Kwa kuonyesha wale wasioona, ni ufalme wa: Yule mwenye haki ya urithi (Mathayo 21:33-34). ‘Msaidizi yule’ atakayenena kwa shauri la BWANA (Yohana 14:26, 16:13-14 n.k.). Yule aliyenenwa na Isaya 29:9-12. "Atamfundisha nani maarifa"? Mteule wa BWANA (Isaya 42:1-14). Jemadari wa vita (Isaya 21:13-17). Yule atakayeleta amri juu ya amri - na lugha mpya katika jina la BWANA (Isaya 28:9-22). Mmoja wa ndugu wa wana wa Israel (Kumb. 18:18-19). Yule aliyeteuliwa kuwaamsha mataifa na kuwaonya viumbe (Isaya 5:26-30, 60:1-14 n.k.). Bwana wa Mabwana na mfalme wa wafalme (Ufunuo 19:11-16). Kulingana na Isaya 42, 60, 21, 28 na 29, na mwenendo mzima wa utabiri huu, haya yote ni masalia katika uzao wa mfalme huyu ambaye ni wa kutoka katika uzao wa Ishmael katika kizazi cha Kedari. Ni Ufunuo mkuu kabisa kutoka Parani (Hijazi) Makkah (Kumb. 33:1-3), (Habakuki 3:3-6, Hagai 2:6-9 n.k.). Mtu yeyote aliyesoma yaani anayefahamu mambo hata kama hana dini, hata kama ni Mkristo, lakini anafahamu kuwa Nabii wa Mwisho ni Muhammad. Asiyejua aulize na akitaka atafahamu jinsi Nabii Muhammad alivyotajwa Jina, Heshima yake, Atatokea (upande gani), Atakavyoangamiza sanamu, Atakavyomuondolea Yesu maoni ya uongo, Atakavyonena mambo mazito n.k. Yeyote awe msomi (anayejiona msomi) awe hakusoma, na mwingine awaye yote anayedhani au mwenye hoja kwamba Muhammad si Nabii wa Mwenyezi Mungu, Jawabu ni kwamba "Hajui". Ni nani awezaye kufasiri maandiko (unabii) kama hamjui Mungu? Ni nani mpumbavu kuliko au mjinga kuliko yule aambiwaye kisha badala ya kusikiliza anafunga masikio ili asisikie? Masikio ulipewa ya nini? Hakuna kitu chochote alichosema Yesu Muhammad akapinga wala alichosema Muhammad ambacho Yesu anapinga isipokuwa juu ya Yesu ni sahihi kama Yesu mwenyewe alivyotabiri kwa kusema "...Ataniondolea mimi maoni yote ya uongo...". Kama ni kusoma dini wamesoma wengi, kama ni imani wanayo wengi, lakini waelewa si wengi. Itaendelea toleo lijalo
|
YALIYOMO
Maoni Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani? Wananchi waingiwa na hofu kuhusu silaha Serikali yagwaya kwa wafugaji
nguruwe
Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo:
Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Muhammad (s.a.w.) katika
Unabii wa Isaya (a.s.)
Ijue SUA Madrasa Moro
Kiteto wakosa darsa kwa kupinga Ramli Ustadh ayeyuka na saruji ya Msikiti mjini Arusha Akina mama Muheza waungana kufanya
Daawa
Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata
uongozi
Je, hivi tuendelee kushika amri
za Mungu tena? - 2
Njia ya uzima ni nyembamba,
waionao ni wachache - 2
Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Sheikh Jongo aichachamalia
Uwawaru
Waamriwa kurejesha Mali ya
Mirathi
Waislamu Mlimba Moro mashakani
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|