|
|
|
WANAWAKE Waislamu wilayani Muheza wameunganisha juhudi zao kwa lengo la kuimarisha harakati za Kiislamu wilayani hapo halikadhalika kujiletea maendeleo ya kiuchumi. Habari zaidi zimeeleza kwamba akina mama hao Waislamu wa Muheza mjini wamefanikiwa kuwaunganisha akinamama kutoka Misikiti mbalimbali pamoja na wale walioko mitaani wanaofanya biashara ndogondogo. Katika kuimarisha mtandao wao, wanawake hao wameshavitembelea vijiji vya Mkuzi, Kwamhosi, Tingeni, Ubembe, Magila, Tanganyika, Kisiwani na Mkumbi. Zaidi ya kuwaunganisha akina mama Waislamu kwa lengo la kuwapa elimu; mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na juhudi hizi mpya ni pamoja na kuwaita wengine katika Uislamu. Tayari wanawake hao wameshawasilimisha wanawake saba ambao walikuwa Wakristo. Jingine ambalo laweza kutajwa kama ni mafanikio ni moyo wa kujitolea
ambapo wanapoandaa semina zao hawangoji mfadhili. Bali huja na vyakula
vyao toka majumbani na kujigharamia mahitajio mengine.
Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata uongozi
WANAFUNZI wa Kiislamu wanaosoma katika shule za sekondari na vyuo mbalimbali mkoani Mbeya wamefanya uchaguzi wa viongozi upya na wakati huo huo wamezindua rasmi Jumuiya mpya ya wanafunzi wa Kiislamu mkoani humo imefahamika. Jumuiya hiyo inayojulikana kama TAMSA tawi la Mbeya, inaundwa na taasisi zipatazo kumi na tisa ikijumuisha sekondari na vyuo vilivyopo katika Manispaa ya Mbeya na baadhi yake viko katika wilaya. Baadhi ya vyuo na shule hizo ni shule ya sekondari Iyunga, Loleza, Sangu, Meta, Mbeya, Mbalizi,Ivumwe, Itende, Meta shule ya ufundi, pamoja na vyuo vilivyomo ni Jakaranda chuo cha ufundi, Chuo cha Uganga - Mbeya M.M.T.C., Chuo cha Kilimo Uyole. Vingine ni Chuo cha Uhasibu DSA, Chuo cha Ufundi Mbeya M.T.C. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, mwanafunzi muhitimu katika Chuo cha Ufundi Mbeya Hamisi Mikidadi alizitaja baadhi ya taasisi na shule zilizo wilayani kuwa ni Chuo cha Ualimu Tukuyu, sekondari ya Kipoke, Ndembele, Lutungano pamoja na sekondari ya Mwakalelinzi. Aliongeza kusema zoezi la kusajili shule na vyuo vingine bado linaendelea. Aidha, muhitimu huyo alisema, zito zaidi ni ukosefu wa vijana wa Kiislamu katika shule na vyuo mkoani humo hii ilitambulika muda mchache baada ya kufanyika kikao kikuu cha viongozi wote mashuleni na vyuoni hapo Oktoba 10, mwaka huu katika chuo cha ufundi Mbeya M.T.C. Kabla ya tawi la TAMSA Mbeya, zamani ilitambulika kama MUWAKI - Mbeya, yaani Muungano wa Wanafunzi wa Kiislamu Mbeya. Akieleza kwa ufupi MUWAKI ilivyoanzishwa mwaka 1986. Wazo la kuanzishwa lilitolewa na mwanafunzi Ramadhani Sanze wa M.T.C. Jumuiya zilizounda MUWAKI kipindi hicho zilikuwa ni MTC Loleza pamoja na Uyole. Alipohojiwa zaidi na mwandishi wa habari hizi ni sababu zipi zilizopelekea kubadilisha MUWAKI na kuwa TAMSA, alisema kuwa MUWAKI ilikuwa haina katiba na wakati wa likizo MUWAKI , haina matamko rasmi, kutokamilisha majukumu yake, pia ilikuwa haitambuliki nje ya mkoa pamoja na wilayani. Vile vile uongozi wa TAMSA - Mbeya ulikubaliana pawe na uongozi wa kudumu, kwa kufanya hivyo itasadia endapo wanafunzi wamalizapo shule na vyuo, TAMSA isiweze kuyumba kwa kukosa kumbukumbu. Pia TAMSA tawi la Mbeya ina mlezi wake ambaye ni Msafiri Njelambala, katika kamati ya Da’awah wapo Ustaadh Sudi, Ally Hashim, Fundi pamoja na Abdulrahamani. Akielezea matatizo ya TAMSA Mbeya alisema ofisi ya muda iliyoko M.T.C pindi chuo kinapofungwa kumbukumbu hupelekwa kwa Katibu Mtendaji ambaye ni mfanyakazi wa TAMSA - Mbeya, haina miradi na kuwa michango ya wanafunzi haitoshelezi mahitaji muhimu. Mfano kuzitembelea taasisi zilizopo nje ya mji pamoja na upungufu wa vitabu vya elimu ya dini pamoja na misahafu. |
YALIYOMO
Maoni Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani? Wananchi waingiwa na hofu kuhusu silaha Serikali yagwaya kwa wafugaji
nguruwe
Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo:
Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Muhammad (s.a.w.) katika
Unabii wa Isaya (a.s.)
Ijue SUA Madrasa Moro
Kiteto wakosa darsa kwa kupinga Ramli Ustadh ayeyuka na saruji ya Msikiti mjini Arusha Akina mama Muheza waungana kufanya
Daawa
Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata
uongozi
Je, hivi tuendelee kushika amri
za Mungu tena? - 2
Njia ya uzima ni nyembamba,
waionao ni wachache - 2
Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Sheikh Jongo aichachamalia
Uwawaru
Waamriwa kurejesha Mali ya
Mirathi
Waislamu Mlimba Moro mashakani
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|