|
|
| Dondoo
za Saikolojia
MARADHI YA KISAIKOLOJIA:
VOYEURISM Na. Abu Halima Sachangwa KATIKA makala zangu zilizopita, nilikuwa nikizungumzia matatizo ya kisaikolojia kuhusu uoni wa watu katika masuala mbalimbali. Leo nitaanza kuangalia maradhi ya kisaikolojia ambayo yameivamia jamii yetu na yanaendelea kuwaathiri watu kwa kasi ya ajabu, hasa wanapokuwa nje ya kanuni na maadili ya Kiislamu. Maradhi haya hujulikana kama Paraphilia ambapo mtu anakuwa na tabia za ajabu na mbaya,kama tutakavyoziona. Paraphilia zote hukithiri katika jamii ambayo watu wake wamezama kwenye zinaa. Zinaa siku hizi katika jamii yetu imekuwa sio dhambi, na imekuwa ni jambo la kawaida lisilo hata na kificho. Matokeo yake watu wengi wamekuwa na maradhi haya ya kisaikolojia ya Paraphilia . Baadhi ya Paraphilia nitakazozingumzia katika makala zangu ni hizi zifuatazo. 1. Voyeurism. 2. Sexual sadism. 3. Frotteurism. 4. Exhibitionism. 5. Fetishism. 6. Transvexualism. 7. Transvestism. 8. Pedophilia. 9. Sexual Mosochism. 10. Homosexualism/Lesbianism. Usitishike na majina hayo kwa lugha ya kigeni. Kila kimoja tutajitahidi kukielezea kwa ufasaha wake katika lugha ya Kiswahili. Voyeurism: Tukianza na maradhi ya kwanza, Voyeurism ni maradhi ya kisaikolojia ambapo mwenye maradhi haya anakuwa na tabia ya kupenda kuangalia watu wasio na nguo. Mtu mwenye maradhi haya huitwa kitaalamu Voyeur (inasomwa vouya). Kwa Kiingereza cha kawaida, mtu huyu huitwa Peeping Tom, Waswahili humwita kozimeni. Mara nyingi Voyeur huwa na tabia ya kuchungulia watu walio kwenye faragha, na yeye roho yake hufurahi kuwaona watu walio wazi bila nguo, na furaha yake hufikia kilele kama atawaona mke na mume wako katika kitendo cha ndoa. Katika jamii yetu leo, maradhi haya yameingia kwa kasi. Tunao watu wengi waliozama hapa, na iko haja ya kupambana na maradhi haya, na hakuna anayeweza kupambana nayo bali Waislamu. Siku hizi, wenye maradhi haya huwezi kuwakuta wanachungulia madirishani au sehemu nyingine, kwa sababu wanaweza kushikwa na kuchomwa moto. Kuna mbinu mpya za kukidhi haja ya wenye maradhi haya. Zamani kulikuwa na senema za X. Siku hizi kuna kanda za video, hawa akina Peeping Toms hujifungia ndani na kuanglia kanda hizi. Hawa ni wagonjwa mahututi. Kuna wagonjwa wengine ambao sio mahututi, lakini nao pia ni ma Voyeur. Kwa mfano, binti wa Kiislamu anaweza akaomba avae hijabu shuleni, lakini wapo watu hawakubali binti huyu afunike viungo vyake. Utamkuta mwalimu anakuwa mkali kabisa, kwani na yeye ni miongoni mwa watu ambao roho zao haziridhiki mtu, hasa mwanamke anapojihifadhi. Hawa ndio wale wale ambao huandaa kile kinachoitwa "mashindano ya uzuri" na kuwapitisha mabinti waliovaa "vichupi" mbele ya kadamnasi, na mwisho huwapa zawadi. Kwa bahati mbaya sana, wenye maradhi hawa ni pamoja na viongozi wa nchi. Wao hufungua na kushiriki katika mambo haya ya kukodolea macho watu walio uchi. Mtume amesema: "Jinsi mlivyo, ndivyo mtakavyotawaliwa", kwa hivyo, kama viongozi wetu ni ma Peeping Tom na ma Voyeur, au Makozimeni, je wanaoongozwa. Kiboko ya maradhi haya hakuna zaidi ya Uislamu kwani ndio unaotekeleza
maamrisho ya Mwenyezi Mungu yasemayo: "Wala msiikurubie zinaa hakika hiyo
ni uchafu na njia mbaya kabisa". (Qur. 17:32)
|
YALIYOMO
Maoni Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani? Wananchi waingiwa na hofu kuhusu silaha Serikali yagwaya kwa wafugaji
nguruwe
Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo:
Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Muhammad (s.a.w.) katika
Unabii wa Isaya (a.s.)
Ijue SUA Madrasa Moro
Kiteto wakosa darsa kwa kupinga Ramli Ustadh ayeyuka na saruji ya Msikiti mjini Arusha Akina mama Muheza waungana kufanya
Daawa
Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata
uongozi
Je, hivi tuendelee kushika amri
za Mungu tena? - 2
Njia ya uzima ni nyembamba,
waionao ni wachache - 2
Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Sheikh Jongo aichachamalia
Uwawaru
Waamriwa kurejesha Mali ya
Mirathi
Waislamu Mlimba Moro mashakani
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|