|
|
|
KATIKA makala yetu ya chakula na lishe ya wiki iliyopita tulijifunza kwa ujumla kwamba chakula ni silaha inayoweza kumsaidia mtu kupunguza kama sio kuondoa kabisa uwezekano wa kupata ugonjwa wa kansa. Kwa maneno mepesi anaweza kusema kuwa tukifuata kanuni na taratibu za chakula na lishe tunaweza kwa kiasi kikubwa kuepuka ugonjwa wa kansa. Makala yetu ya wiki hii ni mwendelezo wa somo la wiki iliyopita. Kansa ya titi (Breast Cancer) ambayo tutajifunza wiki hii ni moja ya aina ya ugonjwa wa kansa. Ugonjwa huo ni tatizo linalowasumbua mamilioni ya watu hasa wanawake katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni. Kwa upande wa wanawake, ugonjwa wa kansa ya titi unachangiwa na sababu kadhaa, baadhi yake ni zile ambazo hatuwezi kuzidhibiti. Kwa mfano historia ya wazazi (ukoo) kama walikuwa na ugonjwa huo, kuanzia siku za mwezi (Menstruation) katika umri mdogo na kutokuzaa. Sababu nyingine (ambayo tunaweza kuidhibiti) ya titi ni aina ya vyakula tunavyokula na matokeo ya vyakula hivyo. Kwa mfano vyakula vyenye mafuta (Cholesterol) ni kichocheo kikubwa cha kansa ya titi. Vile vile kuwa na uzito mkubwa (matokeo ya vyakula) ni kichocheo cha kansa ya titi. Makala zetu za nyuma zilieleza kwa kina sababu na njia za kudhibiti uzito wa miili yetu, hivyo basi katika makala hii sitarudia maelezo hayo. Baada ya utangulizi huo, ni vyema sasa tukapata ushauri nasaha wa lishe juu ya njia za kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya titi. Kwanza watu wajitahidi kupunguza kula vyakula vyenye mafuta. Kama vile mayai ni chanzo kikubwa cha mafuta yajulikanayo kama "Cholesterol" ambayo ni kichocheo kikubwa cha kansa na magonjwa mengine kama yale ya moyo, ni vyema pia watu wakapunguza kiwango cha kuyala. Baadhi ya watafiti wanashauri katika kukabiliana na kansa, mtu ale yai moja au mayai mawili kwa wiki. Pili, watu waongeze kula vyakula vyenye vitamini A na C. Wataalamu wanasema kuwa wanawake wenye virutubisho hivyo mwilini wana uwezekano mdogo wa kupata ugonjwa wa kansa ya titi. Tatu, watu wale vyakula vyenye madini joto (Iodine) na madini ya selenium. Utafiti umeonyesha kwamba upungufu wa madini hasa ya madini joto unazifanya chembe chembe hai (cells) za kwenye matiti zikuwe vibaya na hivyo kuleta ugonjwa wa kansa ya titi. Madini joto na yale ya Selenium yanapatikana kwa wingi katika vyakula vinavyotoka baharini (samaki, dagaa, n.k.) na vyakula vya punje punje (mahindi, mchele, n.k.) Nne, watu wale zaidi maharage badala ya nyama. Maharage yana vitu vinavyoitwa "Proteanse inhibitors" ambavyo vinazuia kutokea kwa kansa. Tano, watu wajiepushe na vyakula na vinywaji kama vile kahawa, chai, cola na chocolate. Vyakula hivyo vina vitu vinavyoitwa ‘methylxanthines’ ambavyo vinahusishwa na ugonjwa wa ‘Fibrocystic’. Zaidi ya hayo, watu hasa wanawake wanashauriwa kwamba: Kila siku japo mara moja wakae faragha na wajichunguze matiti yao kama yana dalili za kansa ya titi. Baadhi ya dalili hizo ni kama vile kutokwa damu, usaha, maji maji n.k. katika matiti. Pia kujisikia maumivu au dalili yoyote ile katika matiti ambayo unaiyona
siyo ya kawaida kama umegundua hali yoyote ile mfano wa maelezo ya hapo
juu au nje ya hayo, haraka wahi hospitalini kwa ushauri nasaha au tiba.
Ukichelewa tatizo litakuwa kubwa kwa hiyo si rahisi kupata ufumbuzi wake.
|
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|