|
|
|
TUNAVYOJUA na ndio hakika yenyewe wananchi wana shida ya huduma bora za afya, kilio chao ni maji safi na salama, shida yao ni barabara mbovu, ukosefu wa umeme wa kuaminika lakini wenye gharama kubwa. Kilio cha vijana ni ukosefu wa ajira, kwa wastaafu na wapunguzwa ni mafao haba tena yenye kucheleweshwa. Kilio na shida ya wauguzi ni vifaa hasa malipo duni sawa na wenzao waalimu ambao pamoja na kupata kichele kinachowafanya wauze ubuyu darasani badala ya kusomesha, wakati mwingine hukopwa hicho kichele chenyewe. Hizi ndizo baadhi tu ya kero za wananchi ambazo serikali ilitangaza na kuahidi kuziondoa. Hatujasikia kwamba wapo wananchi wamekabiliwa na kero kubwa ya kupata majambia kwa saabu ya ukiritimba wa biashara ya silaha. Maduka ya kaya ya sembe na chumvi yalileta kero kubwa na mateso kwa wananchi. Hatukushuhudia watu kupanga foleni za mawe kusubiri mgao wao wa kununua bastola wala leo hatusikii wananchi wakiilalamikia serikali kwamba ukata na njaa inazidi kwa sababu silaha zimekuwa adimu. Wema huu wa kuwarahisishia wananchi kupata silaha mbona hatuuoni kwenye mambo mengine ? Mbona hatuuoni kwenye kumrahisishia mkulima kupata mbolea pembejeo na huduma bora za usafirishaji kwa wakati na kwa bei nafuu ! Leo kijana kwa sababu hana ajira anastukia kaangukia shingo ya mtu na kuondoka na mkufu, je, akiwa na kasilaha kake ! Katika mazingira haya ya rushwa, njaa na kuanguka kwa maadili silaha zimejaa mitaani mpaka zile nzito nzito zisizoruhusiwa ila jeshini, je, itakapokuwa biashara huria. Hoja kwamba sheria na taratibu zitatumika kudhibiti upatikanaji wa vibali vya kununua silaha haina mashiko yoyote. Sheria hizo mbona zisifanye kazi leo wakati mwananchi wa kawaida hajui hata kama kuna maduka ya silaha. Hivi sasa serikali inadhibiti vibali na biashara yenyewe, lakini silaha zimetapakaa kwa majambazi, je, ukiingiza hisia ya kupata pesa kupitia biashara hiyo. Kama sababu ya serikali kurahisisha upatikanaji wa silaha ni kukidhi mahitaji ya wenye mali na mahekalu yao, hao tayari wanazo na kila anayehitaji kwa utaratibu uliopo anapata. Kutokana na hali ya uchumi duniani kote hivi leo biashara mbalimbali zimedoda, sikwambii ya silaha ambayo huhitaji kuwepo kwa ugomvi na migogoro mbalimbali. Wasiwasi wetu isije kuwa yote haya ni shinikizo la kunusuru biashara ya ‘nchi’ iliyododa. Sambamba na hilo pengine wapo wenye ‘amari’ zao kwa ajili ya ujambazi, ujangili na matumizi mengine haramu, hatua hii ya serikali haitahalalisha ‘amari’ hizo ? Kama tulivyokwisha sema awali tumezoea kusikia kuondolewa kwa kero za wananchi, je, tuna kero ya silaha leo ? Sisi kero yetu njaa; kama ni kero ya silaha labda tuambiwe yupo ‘mwekezaji’ anayetafuta soko la silaha zake ‘zilizododa’. |
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|