|
|
|
IMAM wa Msikiti Mujahidiin uliopo Mburahati Jijini, Sheikh Juma Mbukuzi amesema kabla ya kukamatwa usiku wa manane Jumanne wiki iliyopita aliamriwa kutoka nje ya nyumba yake ambako askari polisi walitanda kuzunguka nyumba hiyo. Sheikh Mbukuzi alieleza hayo katika kongamano la Waislamu lililoandaliwa na baraza kuu la jumuiya na taasisi za kiislamu ambalo lilifanyika Temeke Jumapili iliyopita. "Niligongewa usiku wa manane, nilipochungulia dirishani niliwaona askari wakiwa wametanda, alieleza kwa ufasaha Sheikh Mbukuzi huku akisikilizwa kwa makini na Waislamu waliofurika katika kongamano hilo. Sheikh huyo maarufu Jijini, aliendelea kusema kwamba walichukuliwa yeye na mwenzie kisha wakapelekwa kituo cha polisi cha jirani ambako waliamriwa kuvua viatu na kuswekwa ndani hadi kulipopambazuka. Sheikh Mbukuzi alisema kutoka kituo hicho walipelekwa kituo kikuu cha Polisi (Central Police) ambako walielezwa sababu za kukamatwa kwamba wanatuhumiwa kuhusika na kutishia maisha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Luteni Yusuf Makamba. Alisema alipohoji ni kwa vipi ahusishwe na tishio hilo, alionyeshwa "barua" inayodaiwa kuwa na tishio hilo aliyoandikiwa bw.Makamba na watu wasiojulikana. Aidha Polisi walimtaka yeye binafsi afikirie ni kwa vipi ahusishwe na jambo hilo. "Niliwaeleza labda kwa vile nilikamatwa kuhusiana na kadhia ya Mwembechai", alisema Sheikh Mbukuzi. Hata hivyo alisema polisi hao waliikana sababu hiyo na kumtaka afikirie sababunyingine. Aliwaambia kwamba huenda amefitiniwa na baadhi ya watu wa eneo lake ambao hawakufurahishwa na yeye kushinda uchaguzi uliofanyika eneo hilo. "Niliombwa na vijana pamoja na akinamama wa pale mtaani nigombee Uenyekiti wa NGO moja ya eneo letu nikakubali, ulipofanyika uchaguzi mimi niliibuka mshindi kwa kura nyingi, alieleza Sheikh Juma. Kwa hiyo alieleza Imam huyo kuwa huenda kutokana na ushindi huo baadhi ya watu wamejenga chuki dhidi yake. "Nadhani ni kutokana na chuki hii baadhi ya watu wameamua kunifitini, ni demokrasia gani hii? Alieleza na kuhoji Sheikh Mbukuzi. Kwa mujibu wa maelezo yake shauri hilo bado liko polisi hivi sasa na yeye yuko nje kwa dhamana. Jitihada za kumpata msemaji wa polisi kuhusiana na suala hili hadi gazeti hili linakwenda mitamboni hazikuweza kufanikiwa. |
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|