|
|
| Mafundisho
ya Quran
Aya ya 268 na 269
Shetani anakuogopesha ufukara na anakuamrisheni ubakhili; na Allah anakuahidini msamaha utokao kwake na ihsani. Na Allah ni Mwenye wasaa mkubwa na Mwenye kujua. Humpa hekima amtakaye na anayepewa hikima bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. Mtiririko tuliokuwa tunaendelea nao hapo juu kwenye aya zilizotangulia ilikuwa umejikita na suala la kutoa. Bado aya hii na inayofuatia ziko kwenye maudhui hiyo hiyo ya kutoa ingawa kwa namna njia tu. Hapa Allah anakwenda kwenye chimbuko la watu kuwa wagumu wa kutoa mali zao kwenye njia ya Allah au kufanya jambo jengine ambalo kwa uoni wake halimpatii mapato au tija ya haraka haraka inayoweza kufanyiwa hisabu ya faida na hasara. Ni katika maumbile ya binadamu kukimbia kila anachokihisi kuwa kitakuwa ni chimbuko la hasara au matatizo kwake. Kwa mtu anayeona dunia mwisho wake ni kifo na hakuna maisha baada ya haya kutoa bila ya kuingiza kwake hakuna tofauti na kujitia kwenye ufakiri au umasikini wa kujitakia. Ukweli wa mambo ni kuwa anayetoa ni Allah na anayenyima au kumpokonya aliyempa ni Yeye na siyo binadamu yeyote. Hata hivyo hii ni daraja ya imani hivyo kwa wengi bado wasiwasi wa kufilisika upo wakati wa kutoa isipokuwa tu akiona yapo manufaa ama ya dhahiri au yaliyofichikana. Mpangilio wa Allah ni kila mtu anaptoa ndipo anapojiongezea hivyo hapana haja ya wasiwasi wa kufilisika. Kujiongezea huko kuna maana zote mbili – kuongeza kwa mali hapa hapa duniani au kukuta malipo huko akhera ambayo yatakuwa mengi mno kama tulivyokwisha sema au kuelezea huko nyuma. Utaratibu wa Allah ni kulipa kumi kwa kila jema moja; jambo hili limethibitishwa katika maisha ya binadamu wa zama tofauti. Kutokana na sababu ya kuogopa kufilisika ni katika mbinu ya shetani
ya kuwazuilia binadamu kufanya mema. Mbinu za shetani ni nyingi na miongoni
mwao ni hii na nyingine ni zile alizozielezea Allah katika Suratul Nisaa
(aya ya 117 hadi 119):
|
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|