|
|
|
MADRASATUL Maamury Islamiya ipo nyumbani kwa mlezi wa madrasa hiyo marehemu Abdurahmani Mkambi, Sinza madukani mkoa wa Dar es Salaam. Madrasa hii ilianzishwa na Maustaadh watano lakini wawili ndio ambao wamepatikana mmoja aitwaye Ramadhani Khamisi (Kwangaya) mwalimu mkuu na Habibu Kidodi msaidizi. Madrasa hii ilianzishwa mnamo mwaka 1994 ikiwa na wanafunzi 23 wavulana kwa wasichana kwa kipindi hicho walimu walifanya kazi kubwa ya kuwafundisha wanafunzi na wakawa wanaongezeka siku hadi siku. Mpaka hivi sasa wapo wanafunzi 86, wasichana kwa wavulana, masomo yanayotolewa madrasani hapo ni Tawhiid, Sira, Lugha ya Kiarabu, Akhlaq, Fiqh na Qur’an na tafsiri yake. Kwa sasa madrasa hii imesajliwa na Jumuiya ya Walimu wanaosomesha Qur’an Tanzania (JUAKUTA) na inafuata silabasi zao. Mpaka sasa madrasa ina walimu kumi na wameanzisha kitendo cha chekechea ikiwa ni miongoni mwa masomo yanayofundishwa madrasani hapo. Madrasa hii imebahatika kuwapata viongozi wa madrasa ukiachilia mbali walimu waliotajwa hapo awali, viongozi hao ni Mama Rashidi ambaye ni mama wa madrasa, Ihsani Ramadhani Mwenyekiti na Chande Ibrahim Katibu. Hata hivyo, walimu hao wamelalamika sana mahudhurio kwa wanafunzi wakiwa wakubwa wanaamua kuacha chuo bila ya sababu maalumu. Matarajio yao wanataka kujenga chuo ili kiwe cha kujitegemea kwa sababu mpaka hivi sasa chuo bado kipo hapo hapo kilipokuwa awali. Hivyo, wito umetolewa kwa Waislamu wote na makampuni mbalimbali wajitokeze kwa wingi kutoa misaada yao ya hali na mali ili kufanikisha mikakati hiyo. |
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|