|
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekumbushwa kutekeleza ahadi iliyoitoa huko nyuma ya kujiunga na Shirika la OIC.
Akiwasilisha taarifa ya Baraza Kuu katika kongamano la Waislamu lililofanyika
Jumapili Novemba 1, 1998, Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikh Abas Kilima
alisema kwamba ni muda mrefu sasa tangu Serikali iahidi kujiunga na OIC
kwa hiyo kwa niaba ya Baraza lake angeikumbusha Serikali kutekeleza ahadi
hiyo. Endelea...
SERIKALI haijathibitisha mahakamani ukweli wa tuhuma yake dhidi ya Waislamu kumi miongoni mwa Waislamu kadhaa inayowashitaki kwamba walihusika na ghasia za Mwembechai hapo Februari 29, mwaka huu, ambapo Waislamu wawili waliuliwa na polisi kwa risasi na wengine wengi kujeruhiwa. Endelea...
|
|
|