AN-NUUR 
Na.169 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 2 - 8, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Historia: Form IV 

Uongozi wa Dola ya Kiislamu baada ya Mtume (s.a.w) 

 

Kutawafu kwa Mtume(s.a.w) 

Mtume (s.a.w.) ametawafu Jumatatu mwezi kumi na mbili Rabiul awwal jioni mwaka wa 632 au mwaka wa 11 Hijria, akiwa na miaka 63. Pamoja na kuwa Mtume aliumwa tangu miezi michache lakini ugonjwa uliokuwa sababu ya kifo chake ulichukua siku kumi na tatu hivi, akazidiwa na kutawafu siku hiyo. 

Vitabu vya historia vina maelezo yanayosema kuwa wapo Waislamu waliobisha kuwa Mtume hakufa ila alikwenda kwa Mola wake kama alivyokwenda Mussa (a.s.), kuna walio nakili maneno yasemayo kuwa hata Umar ibn Khattab hakuamini kifo cha Mtume na alidiriki kusema kuwa, "atakaesema kuwa Mtume amekufa nitamkata kichwa".1 Imeandikwa kuwa hali ilikuwa ya kuchanganyikiwa mpaka alipokuja Abu Bakar akaingia ndani akafunua uso wa Mtume na kumbusu. Alipotoka nje aliwaambia Waislamu, kama kuna mtu alikuwa anamuabudu Muhammad basi amekufa lakini wanaomuabudu Allah (s.w.) yeye yuko hai milele. Aya yenye maudhui haya iliwapelekea Waislamu kuamini kuwa kweli Mtume amekufa. 

Pengo la Uongozi baada ya kutawafu Mtume 

kifo cha Mtume kiliacha pengo la kiongozi wa Dola. Muhammad alikuwa Mtume wa mwisho hakuwa na Naibu wala Mtume mwingine baada yake. Hivyo kabla ya kuzikwa Mtume, wazo la kupatikana kiongozi wa Dola ndilo lililotawala huzuni ya kila Sahaba. Mtume (s.a.w.) hakuacha usia wowote wa nani awe kiongozi baada ya kifo chake, sio kauli wala ishara. Kule kumuachia Abubakar kuongoza swala asipokuwepo na pale alipokuwepo siku chache kabla ya kifo chake kamwe sio vielelezo vya kumtawaza Abubakar. Ingawa inaweza kuchukuliwa kuwa ni dokezo la kiongozi anaefaa. 

Uchaguzi wa Khalifa wa kwanza 

Mara tu habari za kutawafu kwa Mtume zilipoenea maswahaba ambao ni wajumbe wa Shura wakati wa uhai wa Mtume walisahau wajibu wao wa kudhibiti pengo lililojitokeza, hali hii ikatoa nafasi kwa Waislamu miongoni mwa Ansari kukutana katika ukumbi ulioitwa Saqifah Bani Saidah na kuanza kuzungumzia uongozi. Omar na Abubakar walipopata taarifa hii nao wakaenda kujiunga katika holi hilo, halikadhalika walikuwepo pia Abu Ubaidah Al-Jarrah n.k; lakini wakati huo huo Bani Hashim nao walikuwa wanakutana katika nyumba ya Fatma kuzungumzia Ukhalifa. Mjadala mrefu ulipita, wapo walio taka Khalifa atoke upande wa Ansar, wapo waliotaka ukhalifa utoke upande wa Muhajirina, wapo waliopendekeza kuwa na Khalifa na Naibu wake hatimae walikubaliana pawe na Khalifa mmoja ndipo Abubakar akampendekeza umar upande wa muhajirina na Saad Ubaida upande wa Ansar. Wote kwa pamoja (Umar na Saad) wakasema katika jambo hili hatuwezi kuwa badala yako.2 

Baada ya kauli hii Omar hakuchelewa akampendekeza Abubakar na kumpa mkono na ahadi ya utii. Ndipo wote waliokuwepo wakampa Abubakar mkono wa ahadi ya utii na hivyo Abubakar kuchaguliwa na wengi kuwa Khalifa wa kwanza wa Dola ya Kiislamu. Siku ya pili jambo hili lilipelekwa msikitini na wale ambao walikuwa hawajafanya hivyo basi walimpa ahadi ya mkono wa utii msikitini humo humo. karibu watu thelathini na tatu elfu walichukua ahadi na kumpa mkono wa ahadi ya utii ndani ya msikiti .3 Lakini Ali aliendelea na kikao chake hakuwepo mkutanoni, na alichukua miezi kabla ya kumpa Khalifa ahadi ya utii na kutambua Ukhalifa wake. Wapo wanaodai kuwa aliathiriwa sana na kifo cha Mtume na alishughulika sana na mazishi. Katika tukio hili tunaona msingi wa uislamu ambao tumeshaueleza ulivyofuatwa katika kupata kiongozi wake, watu wenyewe ndio wanaomchagua kiongozi kama ilivyo msikitini waumini wanavyomchagua imamu wao, basi Kitaifa ni hivyo hivyo. 

Pengine pia hapa ni mahali pekee kuondoa yale mawazo yasiyo sahihi kuwa Omar ndie aliyepelekea Abubakar awe Khalifa, hivyo kusingiziwa tukio la Kartasi n.k. Hili si sahihi. Abubakar amepewa ofisi ya ukhalifa sio kwa sababu yoyote zaidi ya kuwa ndiye aliyestahili kwa wakati ule. Na miongoni mwa mambo yaliyopelekea achaguliwe ni kama ifuatavyo: 

Kwanza alikuwa anasifa zote za kuwa kiongozi wa dola kama zilivyotajwa katika kitabu hiki sehemu ya siasa na uendeshaji wa dola katika Uislamu. 

Pili ni kuwa Abubakar alikuwa karibu zaidi na Mtume pengine kuliko swahaba yoyote. Hili linadhihirika zaidi katika msimamo wake wa kufuata hatua kwa hatua kila ambalo Mtume (s.a.w.) amelifanya au kuliruhusu katika uhai wake alipoendesha Dola ya Kiislamu. Usahibu wa Mtume na Abubakar umetajwa kwenye Qur’an na hivyo Abubakar kutajwa kwenye Qur’an wakati wa Hijra, kama ilivyo katika sura (9:40). 

Kama hamtamnusuru (Mtume), basi Mwenyezi Mungu alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru, alipokuwa (Mmoja tu na Mwenziwe) wa pili yake, (peke yao); walipokuwa wote wawili katika pango (Mtume) alipomwambia sahib yake; "Usihuzunike kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi" Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, akafanya neno la wale waliokufuru kuwa chini; na neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Anayeshinda na Ndiye mwenye Hikima. 

Si hivyo tu, lakini Abubakar ndie aliyekuwa Imam aliyeteuliwa na Mtume (s.a.w.) kuendesha swala alipokuwa anaumwa karibu na siku za kutawafu kwake baada ya Hija yake ya kwanza na ya mwisho (Al-Hijjatul wadah) Dr. Majid Ali Khan katika kitabu chake The Pious Caliphs of Islam Abubakar; anaeleza takio linaloonyesha nafasi ya Abubakar ilivyokuwa ni ya kuhesabika mbele ya Mtume na Waislamu kwa jumla. Katika siku hizo ambazo Abubakar ndie aliyeteuliwa kuwa Imam ilitokea kuwa Abubakar hakuwepo wakati wa swala ya jamaa. Mtume aliposikia sauti isiyokuwa ya Abubakar (aliyeswalisha alikuwa Omar Ibn Khattwab) aliulizia juu ya Imam (Abubakar) ambae hakuwepo. Mtume hakupendezewa na akasema. "Asiswalishe mtu mwingine ila Abu Qahafu (Abubakar). Baada ya hapo akaitwa Abubakar lakini wakati huo Imam alikwishamaliza swala. Mtume aliamuru swala ile irudiwe4 na ikaswalishwa na Abubakar. Abubakar alikuwa mtu mashuhuri anaekubalika, anaejiamini, mtaratibu, mwenye istiqama, ikhlaswi, mpevu wa uwoni na mwenye uamuzi na mfuasi wa nyayo za Mtume (s.a.w.). Yote haya ukiyachanganya na umri, kwa wale waliokuwa kwenye ukumbi wa mkutano, Abubakar ndiye aliyewazidi kiumri, hivyo kuchaguliwa kwa Abubakar kulitokana na kuwa na uwezo wa sifa za kuwa Khalifa. Kwa maelezo haya, kutupilia mbali madai ya ukoo wa Hashim ilikuwa lazima. Hotuba ya Abubakar nayo ina umuhimu wake katika uwongozi wa Uislamu kwani inaonyesha wajibu wa kiongozi pale aliposema: 

"Enyi watu mmenichagua niwe mdhamini wenu ingawa mimi sio bora kuliko wengi miongoni mwenu. Nikiwa sahihi nitiini. Nikipotoka nirekebisheni, kwani ukweli ni uaminifu na uwongo ni kutoaminika, aliyedhaifu atakuwa na nguvu mbele yangu mpaka nishindwe kumpatia haki zake Insha-Allah; na mwenye nguvu (Uwezo) mbele yangu atakuwa dhaifu mpaka alipe haki za wengine. Insha-Allah. Allah huteremsha nakama kwa watu walioacha Jihad katika njia yake. Vile vile Mwenyezi Mungu huteremsha maafa kwa watu ambao hufanya maovu." 

Alipomaliza alitokea mtu mmoja aliyesema kama hutafuata haki tutakunyosha kwa ncha ya upanga. Angalia uhuru wako! Yule raia hakuogopa wala Khalifa hakukasirika. 


Islamic Knowledge for "A" Level 

Tawhiid Form V 

Islam: A Complete Way of Life 

‘But Islam has a still further service to render to the cause of humanity. It stands after all nearer to the real East than Europe does, and it possesses a magnificent tradition of inter-racial understanding and co-operation. No other society has such a record of success in uniting in an equality of status, of opportunity, and of endeavour so many and so various races of mankind....Islam has still the power to reconcile apparently irreconcilable elements of race and tradition. If ever the opposition of the great societies of East and West is to be replaced by co-operation, the mediation of Islam is an indispensable condition. In its hands lies very largely the solution of the problem with which Europe is faced in its relation with the East. If they unite, the hope of a peaceful issue is immeasurably enhanced. But if Europe, by rejecting the co-operation of Islam, throws into the arms of its rivals, the issue can only be disatrous for both. 

Universality and Humanism 

The message of Islam is for the entire human race. God, in Islam, is the God of all the world (al-Qur’an, 1:1) and the Prophet is a Messenger for the whole of mankind. In the words of the Qur’an: 

‘O people! I am the Messenger of God to you all.’ (al-Qur’an, 7:158). 

‘One who comes as a warning to all the nations.’ (al-Qur’an, 25:1) and ‘We have not sent thee but as a (source of) mercy for all the nations’ (al-Qur’an, 21:107). 

In Islam all men are equal, whatever be their colour, language, race or nationality. Islam addresses itself to the conscience of humanity and banishes all false barriers of race, status and wealth. There can be no denying the fact that such barriers have always existed, and do exist even today in this so-called enlightened age. Islam removes all these impediments and proclaims the idea of the whole of humanity being one family of God. 

The Holy Prophet said: 

‘All creatures of God form the family of God and he is the best loved of God who loveth best His creatures.’ 

‘O Lord! Lord of my life and of everything in the universe! I affirm that all human beings are brothers to one another.’ 

‘Respect God and be affectionate to the family of God.’ 

Islam is international in its outlook and approach and does not admit barriers and distinctions based on colour, clan, blood or territory such as were prevalent before the advent of Muhammad (peace be upon him) and which are rampant in different forms even in this modern age.It wansts to united the entire human race under one banner. 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 TAHARIRI 
Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? 

Nyumba ya Wakfu yageuzwa  Baa Dar 
Na Mwandishi Wetu 

‘VAT’ yaingia Bakwata Same 
 Na Mwandishi Wetu 

Mchungaji asema hakuna mihadhara ya kashfa 
 Na Muhibu Saidi 

Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa 

Safari yangu Ufini 
Ustaadh Ka-Batembo 

Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni ukomeshwe 
Na Abuu Afahah 

Wanaume toeni haki za wanawake 
Na Zabibu Iddi Ng’onda Box 78, Mwadui 

MAONI: Yesu ni yule yule Isa 
Na Saleh Ngoi 

Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii 
Na Elia Batendi, S.L.P. 538, DSM 

Ukoloni mwingine unaingizwa nchini? 
Sheikh Thabit H. Mbago,S.L.P. 21486,DSM 

Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine? 
Na Athman Rajab 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

AN-NUUR  lina chuki na Wakristo 
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara 

Msiiparamie ovyo Biblia 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu ya idadi ya watu 1989 
Na Rajab Rajab 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 

Waislamu Moro watakiwa kutoyumba 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Wanawake Masasi wawataka Masheikh kutangaza sheria za Allah 
Na Muhibu Saidi, Masasi 

Ugaidi na Uislamu siyo kitu kimoja – Sheikh Jongo 
Na Bakari Musa 

Sheikh Abbas awataka wananchi Dodoma waepuke upuuzi 
Na Abu Zubair, Dodoma 

Vijana watakiwa kujiepusha na ‘vijiwe’ 
Na Badru Kimwaga 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya   261-263 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Magonjwa yanayoathiri lishe 
   

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita