AN-NUUR 
Na.169 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 2 - 8, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Mchungaji asema hakuna mihadhara ya kashfa 

Asema Imani ya Waislamu haiwezi kuwa kashfa 

Adai haiwezi kuleta machafuko 

Na Muhibu Saidi 

MCHUNGAJI wa Kanisa la Kilutheri Temeke Bw. Msafiri Chabulilo amesema kwamba imani za Waislamu na Wakristo kamwe haziwezi kuitwa kashfa wala kuleta machafuko nchini. 

Pamoja na kuibuliwa propaganda ya mihadhara ya kashfa; Mchungaji Chabulilo amesema hajaona mabadiliko yoyote katika ushirikiano wa mambo mbalimbali kati ya Waislamu na Wakristo uliokuwepo toka zamani. 

Ameyasema hayo kufuatia onyo la Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. John Chiligati (Capt.) kwamba serikali itapambana na wanaoendesha mihadhara inayokashifu dini nyingine. Katika kikao chake na viongozi wa kidini Septemba 28 ofisini kwake, Kapteni Chiligati alidai kwamba watu wanaoendesha mihadhara hiyo ni watu wachache ambao alidai kuwa wanafanya hivyo kutokana na kusumbuliwa na njaa. 

Kapteni Chiligati alisisitiza kuwa iwapo watu hao wataachwa waendelee na mihadhara hiyo watasababisha mapigano kama yale yanayoendelea katika Jamhuri ya Congo ambapo alisema hali hiyo itasababisha pia Misikiti na Makanisa kutokuswaliwa. 

Akizungumzia suala la kuchanganya dini na siasa, Kapteni Chiligati alishutumu kitendo cha Misikiti na Makanisa kutumika kama viwanja vya siasa, jambo ambalo alisema ni hatari tupu inayoweza kuiletea nchi matatizo. 

"Makanisa na Misikiti ni mahali pa swala tu. Inashangaza kuona watu wanaacha vyama wanatumia Misikiti na Makanisa. Hali imefikia leo watu hao wanatangaza kwamba mwaka 2000 Rais awe Muislamu au Mkristo, tuwe macho na hili litatuharibia", alisema Mh. Chiligati na kuongeza kuwa anashukuru sana kuona mambo hayo hayapo katika wilaya yake. 

Alidai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Luteni Yusufu Makamba alikwisha wahi kuwatahadharisha wakuu wake wa wilaya kuhusiana na kitendo cha Msikiti mmoja uliopo Konondoni cha kugawa kadi za chama cha CUF ndani ya Msikiti. Hata hivyo Mh. Chiligati hakuutaja Msikiti huo. 

Mapema akitoa mchango wake katika mkutano huo, mmoja wa wadhamini wa ALMALLID, Mzee Amani Mushi alimwambia Mkuu wa Wilaya kwamba suala la mihadhara inayoitwa ya "kashfa" limekwisha wahi kuzungumzwa Ikulu baina ya Masheikh na Maaskofu chini ya Uenyekiti wa Rais mstaafu wa pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, lakini halikupatiwa ufumbuzi kwa kashfa hizo kuwekwa bayana. 

Mzee Mushi aliongeza kuwa pia kikao kingine kama hicho kimewahi kufanyika katika Hoteli ya Forodhani, Jijini chini ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani Mh. Ernest Nyanda na hivi karibuni, kilifanyika kikao kama hicho katika ukumbi wa Karimjee chini ya Uenyekiti wa Waziri wa sasa wa Mambo ya Ndani, Mh. Ali Ameir Mohamed ambapo Wakristo na Waislamu walikubaliana kwa kauli moja kuvumiliana katika imani zao za msingi. 

Aidha, Mzee Mushi alisema wakati huo huo serikali ilikwisha sema kupitia kwa Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma kuwa haitangilia tena mambo ya dini badala yake itawaachia wana dini wenyewe. 

"Leo tunashangaa kuona tunaitwa na Mkuu wa Wilaya kurudia suala lile lile", alishangaa Mzee Mushi. 

Akizungumza katika kikao hicho, Sheikh Omar Matata alisema kwamba mahali popote ambapo haki haitendeki basi hakuna amani na akatahadharisha kwamba kama serikali itawadhulumu na kuwaonea Waislamu basi ijue amani haitakuwepo. 

Aidha, Sheikh Matata amesisitiza kwamba Waislamu hawako tayari kumtii kiumbe yeyote kwa kuacha kuhubiri mafundisho ya Uislamu kwamba Yesu si Mungu, na kwamba hakufa msalabani wala kufufuka. Alisema kufanya hivyo itakuwa ni kumuasi Mwenyezi Mungu. 

Akijibu madai ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Temeke kwamba baadhi ya waliotoka rumande wanatamba kuendeleza mihadhara ya kashfa na kwamba serikali itawakamata, Sheikh Matata alisema pamoja na kuwepo mkakati huo, lakini hakuna hata kesi moja ya watuhumiwa hao imekwishafika mwisho wake zaidi ya usumbufu na uonevu. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 TAHARIRI 
Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? 

Nyumba ya Wakfu yageuzwa  Baa Dar 
Na Mwandishi Wetu 

‘VAT’ yaingia Bakwata Same 
 Na Mwandishi Wetu 

Mchungaji asema hakuna mihadhara ya kashfa 
 Na Muhibu Saidi 

Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa 

Safari yangu Ufini 
Ustaadh Ka-Batembo 

Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni ukomeshwe 
Na Abuu Afahah 

Wanaume toeni haki za wanawake 
Na Zabibu Iddi Ng’onda Box 78, Mwadui 

MAONI: Yesu ni yule yule Isa 
Na Saleh Ngoi 

Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii 
Na Elia Batendi, S.L.P. 538, DSM 

Ukoloni mwingine unaingizwa nchini? 
Sheikh Thabit H. Mbago,S.L.P. 21486,DSM 

Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine? 
Na Athman Rajab 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

AN-NUUR  lina chuki na Wakristo 
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara 

Msiiparamie ovyo Biblia 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu ya idadi ya watu 1989 
Na Rajab Rajab 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 

Waislamu Moro watakiwa kutoyumba 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Wanawake Masasi wawataka Masheikh kutangaza sheria za Allah 
Na Muhibu Saidi, Masasi 

Ugaidi na Uislamu siyo kitu kimoja – Sheikh Jongo 
Na Bakari Musa 

Sheikh Abbas awataka wananchi Dodoma waepuke upuuzi 
Na Abu Zubair, Dodoma 

Vijana watakiwa kujiepusha na ‘vijiwe’ 
Na Badru Kimwaga 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya   261-263 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Magonjwa yanayoathiri lishe 
   

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita