|
|
| Maoni
yetu
Masheikh tupeni Fatwa
MTU akifa amali zake zote zimekatika ila Swadaqatul-Jaaria, Masheikh wanatwambia. Swadaqa hii huendelea kumpatia thawabu maiti muda wa kudumu swadaqa ile. Maana yake ni kwamba kama mtu amechimba kisima kadri watu watakavyoendelea kunufaika na maji ya kisima hicho naye hupata thawabu, ila tu kitakapokuja kukauka. Hivyo kama mtu alijenga nyumba akaiweka Wakfu isaidie yatima au kulipa mshahara wa Mwalimu wa Madrasa, ataendelea kupata thawabu mpaka hapo nyumba hiyo itakapoanguka. Lakini je, kama mtu amechimba kisima akatokea mtu kwa sababu zisizoeleweka akaelekeza mtaro wa maji machafu ndani ya kisima hicho ili watu wasifaidike na maji hayo; je nini hukumu ya mtu huyu; na je, yule marehemu ataendelea kupata thawabu zake? Watu wengi kwa kuzingatia mafundisho ya Uislamu na kwa kuzingatia nasaha za Masheikh wao, wamekuwa wakitoa Sadaqatul-Jaaria kwa kujenga Misikiti, Madrasa na kuweka nyumba zao Wakfu. Kodi inayopatikana kutokana na nyumba hizo hulipa gharama za kuendesha Msikiti, mishahara ya walimu wa madrasa, Maimamu n.k. Kwanza tungependa Masheikh wetu watukufu watueleze nini jukumu lao katika kuilinda mali hii ya Wakfu. Nini jukumu la Taasisi, Jumuiya na Mabaraza ya Kiislamu katika kudumisha ‘amana’ hii iliyoachwa na Waislamu wema. Na nini jukumu la Waislamu wote kwa ujumla kuzitunza Sadaqa hizi ambazo ni za thamani kubwa kuliko chochote katika hii dunia kwa waliotangulia mbele za haki. Pili nyumba ya Wakfu inapogeuzwa Baa bado ni Wakfu? Masheikh tupeni jibu. Na nini hukumu ya yule aliyeitoa kama Sadaqatul-jaaria mbele ya Allah. Bado ataendelea kupata thawabu wakati badala ya nyumba hiyo kuunufaisha Msikiti na Uislamu imegeuzwa danguro na kilabu ya kangara na ‘taska’! Nini hukumu ya Allah kwa wale wanaoingia Misikitini wakaswali wakatumia mali zao na nguvu zao kupigania viwanja vyao vinapoporwa lakini wakawa hawafanyi lolote amana za Allah (sw) zinapohujumiwa. Masheikh wetu watukufu tunaomba Fatwa juu ya jambo hili. Kitabu cha Allah (sw) na Sunnah ya Mtume (saw) inasemaje. Fatwa hii ni muhimu kwa sababu haitakuwa na maana Masheikh kutuhimiza tuwekeze katika swadaqatul-jaariah wakati sadaqa hiyo inakoma mara tu tuingizwapo katika mwanandani. Jaalia waliokwenda mbele za haki na kuacha nyumba zao Wakfu wanafufuka na kukuta zimeuzwa na kugeuzwa madanguro na vilabu ya ‘dengelua’ la Kizungu na gongo, vipi wangejihisi. Leo ni nyumba ya Bint Omar kesho itakuwa ya Mwinshehe. Tunadhani ni muhimu Masheikh watupe Fatwa juu ya suala hili kabla ya kuendelea kutuhamasisha kuweka mali zetu Wakfu. Ni bora tuziuze wenyewe tukiwa hai tule na kunywa vya halali kwa wasaa kuliko kuziacha Wakfu zije kuwa vilabu vya ulanzi.MTU akifa amali zake zote zimekatika ila Swadaqatul-Jaaria, Masheikh wanatwambia. Swadaqa hii huendelea kumpatia thawabu maiti muda wa kudumu swadaqa ile. Maana yake ni kwamba kama mtu amechimba kisima kadri watu watakavyoendelea kunufaika na maji ya kisima hicho naye hupata thawabu, ila tu kitakapokuja kukauka. Hivyo kama mtu alijenga nyumba akaiweka Wakfu isaidie yatima au kulipa mshahara wa Mwalimu wa Madrasa, ataendelea kupata thawabu mpaka hapo nyumba hiyo itakapoanguka. Lakini je, kama mtu amechimba kisima akatokea mtu kwa sababu zisizoeleweka akaelekeza mtaro wa maji machafu ndani ya kisima hicho ili watu wasifaidike na maji hayo; je nini hukumu ya mtu huyu; na je, yule marehemu ataendelea kupata thawabu zake? Watu wengi kwa kuzingatia mafundisho ya Uislamu na kwa kuzingatia nasaha za Masheikh wao, wamekuwa wakitoa Sadaqatul-Jaaria kwa kujenga Misikiti, Madrasa na kuweka nyumba zao Wakfu. Kodi inayopatikana kutokana na nyumba hizo hulipa gharama za kuendesha Msikiti, mishahara ya walimu wa madrasa, Maimamu n.k. Kwanza tungependa Masheikh wetu watukufu watueleze nini jukumu lao katika kuilinda mali hii ya Wakfu. Nini jukumu la Taasisi, Jumuiya na Mabaraza ya Kiislamu katika kudumisha ‘amana’ hii iliyoachwa na Waislamu wema. Na nini jukumu la Waislamu wote kwa ujumla kuzitunza Sadaqa hizi ambazo ni za thamani kubwa kuliko chochote katika hii dunia kwa waliotangulia mbele za haki. Pili nyumba ya Wakfu inapogeuzwa Baa bado ni Wakfu? Masheikh tupeni jibu. Na nini hukumu ya yule aliyeitoa kama Sadaqatul-jaaria mbele ya Allah. Bado ataendelea kupata thawabu wakati badala ya nyumba hiyo kuunufaisha Msikiti na Uislamu imegeuzwa danguro na kilabu ya kangara na ‘taska’! Nini hukumu ya Allah kwa wale wanaoingia Misikitini wakaswali wakatumia mali zao na nguvu zao kupigania viwanja vyao vinapoporwa lakini wakawa hawafanyi lolote amana za Allah (sw) zinapohujumiwa. Masheikh wetu watukufu tunaomba Fatwa juu ya jambo hili. Kitabu cha Allah (sw) na Sunnah ya Mtume (saw) inasemaje. Fatwa hii ni muhimu kwa sababu haitakuwa na maana Masheikh kutuhimiza tuwekeze katika swadaqatul-jaariah wakati sadaqa hiyo inakoma mara tu tuingizwapo katika mwanandani. Jaalia waliokwenda mbele za haki na kuacha nyumba zao Wakfu wanafufuka na kukuta zimeuzwa na kugeuzwa madanguro na vilabu ya ‘dengelua’ la Kizungu na gongo, vipi wangejihisi. Leo ni nyumba ya Bint Omar kesho itakuwa ya Mwinshehe. Tunadhani ni muhimu Masheikh watupe Fatwa juu ya suala hili kabla ya kuendelea kutuhamasisha kuweka mali zetu Wakfu. Ni bora tuziuze wenyewe tukiwa hai tule na kunywa vya halali kwa wasaa kuliko kuziacha Wakfu zije kuwa vilabu vya ulanzi. |
YALIYOMO
TAHARIRI Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? Nyumba ya Wakfu yageuzwa Baa
Dar
‘VAT’ yaingia Bakwata Same
Mchungaji asema hakuna mihadhara ya
kashfa
Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa Safari yangu Ufini
Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni
ukomeshwe
Wanaume toeni haki za wanawake
MAONI: Yesu ni yule yule Isa
Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii
Ukoloni mwingine unaingizwa
nchini?
Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine?
Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo
kwa maneno
AN-NUUR lina chuki na
Wakristo
Msiiparamie ovyo Biblia
Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu
ya idadi ya watu 1989
Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 Waislamu Moro watakiwa kutoyumba
Wanawake Masasi wawataka Masheikh
kutangaza sheria za Allah
Ugaidi na Uislamu siyo kitu
kimoja – Sheikh Jongo
Sheikh Abbas awataka wananchi
Dodoma waepuke upuuzi
Vijana watakiwa kujiepusha
na ‘vijiwe’
Mafundisho ya Quran
Chakula na Lishe
|